MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

UKWELI JUU YA UMIZIMU{MALAIKA WAOVU}.

Swali la kujiuliza ambalo limekuwa changamoto kwa binadamu wengi ni! "UMIZIMU" Nikitu gani je ni kiumbe kama viumbe wengine ama ni roho kama roho nyingine kwa swali hilo na mengine mengi 
juu ya mizimu, Rafiki karibu upate ukweli juu ya umizimu na kazi zake, katika ulimwengu wa ROHO
.
HISTORIYA YA UMIZIMU ILIVYOINGIZWA KWA BAADHI YA MADHEHEBU.
Kwa miaka mingi watu wameamini kwamba wafu wanaweza kuwaongoza walio hai. Hadithi moja ya kale iliyoandikwa na mshairi Mgiriki Homer kuhusu Odysseus, ambaye pia anaitwa Ulysses inaunga mkono wazo hilo. Shujaa huyo anayesimuliwa na Homer alitaka kujua jinsi angerudi kwenye kisiwa cha nyumbani cha Ithaca, kwa hiyo, akaenda kwenye ulimwengu wa wafu kutafuta ushauri wa mbashiri aliyekuwa amekufa.

. Dini nyingi kubwa hufundisha kwamba inawezekana kuwasiliana na wafu. Kitabu Encyclopedia of Religion kinasema kwamba “ufundi au zoea la kuinua na kuwasiliana na nafsi za wafu, ni aina fulani ya uaguzi.”

 Kisha kinaongeza kusema kwamba zoea hilo “limeenea sana.” Kitabu New Catholic Encyclopedia kinathibitisha jambo hilo kwa kusema kwamba “ufundi au zoea la kuinua na kuwasiliana na nafsi za wafu, katika njia mbalimbali, limeenea ulimwenguni pote.” Hivyo haishangazi kwamba baadhi ya wafuasi wa dini nyingi wamejaribu kupata habari kutoka kwa ulimwengu wa roho!

Kitabu New Catholic Encyclopedia kinasema kwamba ingawa zoea hilo la kuwasiliana na wafu “lilishutumiwa vikali na Kanisa, maandishi mengi yanaonyesha kwamba zoea hilo liliendelezwa katika Enzi za Kati na katika kile Kipindi cha Mwamko.” Biblia inasema nini kuhusu mambo hayo?


                          SWALI MAANDIKO YANASEMAJE?

Mafundisho yahusuyo kutokufa kwa roho kwanza yalitokana na imani ya wapagani, na wakati wa giza la kiroho mafundisho haya yaliingizwa katika imani ya kikristo na kuhesabika kuwa ni mojapo ya ukweli, na yakashika mahali pa Maandiko yasemayo kuwa, “wafu hawajui neno lo lote” Mhubiri 9:5. “Watu wengi huamini kuwa roho za wafu ndizo zile, zisemwazo kuwahudumu wale watakaourithi wokovu” Waebrania 1:14.

Imani ya kuwako roho za wafu kuja kuwahudumia watu wanaoishi, imeandaa njia ya kuingizia mambo ya kisasa ya kuongea na wafu. Kama watu wanaoufahamu unaozidi ule waliokuwa nao wakati walipoishi, mbona hawaji tu kiwazi na kuwaelimisha watu? Ikiwa roho za wafu huwazungukia jamaa zao walioko duniani, mbona hawakai na kuongea nao? Mbona wanaoamini kuwa mtu akifa huwa anajua mambo, hukataa nuru ya Mungu inayoeleza mambo ya roho? Hapa ndipo Shetani hufanyia kazi yake. Malaika waovu huonekana kama wajumbe katika ulimwengu wa roho.

 Mkuu wa uovu yaani shetani anao uwezo wa kuleta sura za watu waliokufa ambao ni jamaa. Maigizo ya watu hao ni kamili kabisa. Huonekana kama wao halisi. Watu wengi hufarijika kuwa ndugu na rafiki zao wako wanaishi huko mbinguni. Bila kujihadhari na hatari yo yote, hutega masikio kwa “roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani” 1 Tim. 4:1.

 Waliokufa bila kujitayarisha, yaani bila kujitoa kwa Kristo, hudai kuwa wako katika furaha kuu huko mbinguni. Watu hawa bandia wanaojidai kuwa wanakaa rahani mbingu, mara nyingine husema maneno ambayo huwa ya kweli. Wakishakuaminiwa, hutoa mafundisho yaliyo kinyume cha Biblia. Kwa kuwa mara nyingine husema maneno ya kweli na kutabiri mambo fulani ambayo hutokea kuwa kweli, hivyo mafundisho yao ya uongo hukubaliwa kama mafundisho ya kweli ya Biblia. Sheria ya Mungu imewekwa kando, na Roho wa neema amedharauliwa. Hiyo ndiyo mizimu, na roho za mashetani. Roho hizi hukataa Uungu wa Kristo na kumhesabu Mwumbaji kuwa na hali sawa na yao.

 Wakati matokeo ya udanganyifu huo hukubaliwa kama ukweli, hutokea ishara ambazo ni kazi za yule mwovu huwadangaya watu wakaziamini kama ishara za Mungu. Watu wengi huamini kuwa hali ya kuongea na wafu. Au mizimu ni ujinga wa kibinadamu. Wanapokabiliwa na maonyesho ya wazi ambayo hawawezi kuyakanusha, hukubali kuwa hayo kutoka kwa Mungu.

 Kwa msaada wa shetani wachawi wa Farao waliigiza kazi ya Mungu na kufanya miujiza. Soma Kutoka 7:10-12. Paulo ashuhudia kuwa kuja kwa Bwana kutatanguliwa na “Kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na maajabu za uongo, na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea” 2Tes. 2:9-10. Yohana naye anasema, “Naye, afanye ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya” ufunuo 13:13-14. Hapa sio ujanja wa kibinadamu unaoelezwa. Watu hudangaywa na shetani kwa ishara ambazo wajumbe wake huzifanya, sio wanazojifanya kuzifanya.

                           KWA MAANDIKO ZAIDI

                             Isaya 8:19 Biblia inasema.

''Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai    

    Katika nyakati za kale, Yehova Mungu aliwaamuru hivi watu wake: “Asipatikane ndani yako . . . yeyote anayeuliza habari kutoka kwa wafu.” (Kumbukumbu la Torati 18:9-13) Kwa nini Yehova alitoa amri hiyo? Ikiwa ingewezekana kwa walio hai kuwasiliana na wafu, je, halingekuwa jambo lenye upendo kwa Mungu wetu kuruhusu jambo hilo? Lakini kwa kweli, haiwezekani kuwasiliana na wafu. Tunajuaje hilo?

Maandiko yanafundisha tena na tena kwamba wafu hawana fahamu. Ona kile Mhubiri 9:5 inasema: “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe.” Zaburi 146:3, 4 inasema: “Msiweke tegemeo lenu katika watu wenye vyeo, wala katika mtu wa udongo, ambaye hana wokovu wowote. Roho yake hutoka, naye hurudi kwenye udongo wake; siku hiyo mawazo yake hupotea.” Na pia nabii Isaya alisema kwamba wafu ‘hawajiwezikatika kifo.’—Isaya 26:14                  

 MIZIMU NI,KINANI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

1; Mizimu ni malaika walioasi mbinguni baada ya shetani kutupwa na theluthi ya malaika hawa malaika waasi walipo tupwa duniani waligawanyika vitengo mbalimbali moja waponi kitengo cha umizimu.

 2;Mizimu  ni  wapelelezi na ni  usalama wa taifa wa shetani, kazi hii wanaifanya kwa uaminifu mkubwa sana, kuwa makini sana mshikilie YESU mda wote. 

3;Mizimu inauwezo wa kutoa nyaraka au taarifa ya mtu.

4;Mizimu  inafanya kazi kupitia wafu.

 waebrania 9;27 ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu''

5;Mizimu  inafanya  kazi kupitia waganga  wa kienyeji. 

6;Mizimu inauwezo wa kutunza taarifa za mtu, ukoo au kabila.

Kwa kadiri siku zinavyokwende FUNDISHO juu ya kuomba watu waliokufa na kuamini kuwa wako hai limeshika kasi sana, na fundisho hili ni mbinu ya shetani kuuhada ulimwengu kuwa wafu wanaweza kuongea na walioko hai, ambapo kimsingi lilianzia pale kwenye bustani ya edeni, wakati MUNGU aliposema siku mtakayo kula matunda ya mti wa katikati mtakufa hakika, Shetani yeye alisema hakika hamtakufa 

 Na hii imepelekea leo baadhi ya madhehebu kufundisha watu waombe kupita wafu mfano, mtakatifu fulani tuombee, tumekumbuka na tunakuombea fundisho hili ni kinyume na utaratibu wa maandiko matakatifu{biblia"}

 MUNGU ANACHUKIA SANA JAMBO HILI LA KUOMBA WAFU{UMIZIMU}

Biblia inaeleza kwamba baada ya Mfalme Sauli wa Israeli kukataliwa na Yehova kwa sababu ya kutomtii, Sauli alijaribu kumtumia mwanamke aliyewasiliana na pepo ili azungumze na nabii Samweli aliyekuwa amekufa. Sauli alipokea ujumbe kutoka katika ulimwengu wa roho, lakini ujumbe huo haukutoka kwa Samweli. Kwa kweli, Samweli alikuwa amekataa kumwona mfalme huyo, na aliwapinga wale waliokuwa wakiwasiliana na pepo. Kwa hiyo, Sauli alipokea habari kutoka kwa roho mwovu ambaye alijifanya kuwa Samweli.—1 Samweli 28:3-20.

Roho waovu ni adui za Mungu, na ni hatari kuwasiliana nao. Kwa sababu hiyo, Maandiko yanaamuru hivi: “Msiwaendee wenye kuwasiliana na pepo, wala msitafute shauri la wajuzi wa kubashiri matukio, ili kutiwa unajisi nao.” (Mambo ya Walawi 19:31) “Yeyote anayeuliza habari kutoka kwa wafu,” inaonya Kumbukumbu la Torati 18:11, 12, “ni chukizo kwa Yehova.” Kwa kweli, moja kati ya mambo yaliyomfanya Mfalme Sauli akose uaminifu na hivyo auawe na Yehova ni “kuuliza [habari] kutoka kwa mwenye kuwasiliana na pepo.”—1 Mambo ya Nyakati 10:13, 14.

Kwa mawasiliano zaidi,maswali na majibu piga simu number 0763371047 by @24gospelnews Charles Shibita. punda wa yesu.

BARIKIWA SANA RAFIKI.

Subscribe to receive free email updates: