MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

"ONYO LA MWISHO" SEHEMU YA KWANZA

 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, 4na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. 

5Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; 6kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. 7Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa


 

Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako: na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanzaa kuwapo taifa hata wakati huo huo, na wakati huo watu wako wataokolewa: kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile”. Daniel 12:1.

MUNGU hajawahi kuadhibi wanadamu bila kutoa maonyo , Wakati wa galika MUNGU alitoa maonyo kupita watu wake mbalimbali kama vile, ENOKA, METUTHELA,NA NUHU akatoa neema ya miaka 120 kwa wakaazi wa dunia kuweza kutubu ili wasiangamia matokeo yake kwa waakazi takribani zaidi ya bilioni moja watu 8 wafamiliya moja tu ndiyo waliokolewa wengine wote waliangamia kwa sababu ya kiburi cha ujuaji  mwanzo 6,7 na 8

Vivohivo wakati wa RUTU maovu katika miji ya sodoma, sidim, soari na gomora yalifikia kiwango cha juu MUNGU akaazimu kuangamiza hiyo miji na wakaji wake, lakini kabla ya hapo alitoa neema kwa wakazi hao, Rutu alipewa taarifa ya kwenda kuwapasha habari juu ya uangamivu uliokuwa uanaenda kutokea, lakini maadiko yanasema alionekana kama mtu achezaye mbele za wakweze. "mwanzo 6".

Kurudi kwa Kristo kutawaghafdisha walimu wa uongo. Kwa wale wote wenye kuufanya ulimwengu huu kuwa makao yao siku ya Mungu itawapata kama mtego unasao, na kama mwizi ajaye usiku. Ulimwengu ukiwa umezama katika machafuko na anasa za ufedhuli, umelala katika utulivu wa mauti. Watu huyacheka maonyo; “Na kesho itakuwa kama leo, sikukuu kupita kiasi.” Isaya 56:12. Tutatazama zaidi katika ya maisha ya anasa. Lakini Kristo asema: “Naja kama mwivi.” Ufunuo 16:15. Wakati wenye dhihaka wanapoende-lea kwa kiburi wakati watafula mali wanaendelea katika kupata mali bila kujali kanuni, wakati mwanafunzi anajitahidi kutafuta kila elimu, isipokuwa Biblia, Kristo atakuja kama mwiz.

                             YESU ANASEMA

Kristo aliendelea kusema: “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika, Safina, wasitambue hata Gharika ikaja ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.”

 Siku za Nuhu zilikuwaje? “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani, na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni haya tu siku zote,” (Mwanzo 6:5). Watu wa siku za Nuhu walifuata dhana zao ovu na mawazo yaliyopotoka. Kwa sababu ya uovu wao waliangamia. Leo ulimwengu unashika njia ile ile.Waasi wa sheria ya Mungu wanaujaza ulimwengu na maovu. Uchezaji wa kamari, ufedhuli, tamaa mbaya na ahiki zisizozuilika, yote hayo yanaujaza ulimwengu kwa maasi

. Kila kitu ulimwenguni kinachemka. Dalili za nyakati zinaogofya. Roho wa Mungu anaondolewa duniani taratibu, na ajali zinafuata moja baada ya nyingine katika nchi na bahari. Kuna tufani na tetemeko, mioto, mafuriko, mauaji ya kila namna. Nami awezaye kuzisoma nyakati? Usalama uko wapi? Hakuna uhakika katika cho chote kile cha mwanadamu au ulimwengu. 

Wako wale wanaongojea, wakikesha na kutenda kazi kwa ajili ya kurudi kwa Bwana wetu. Kundi jingine linasimama katika mstari wa yule mwasi mkuu wa kwanza. 

Hatari inatujia pole pole. Jua linang’aa mbinguni, likiendelea na mzunguko wake wa kawaida juu mbi-nguni. Watu wanaendelea kula na kunywa, wakipanda na kujenga majumba. Wafanya biashara wanaendelea kuuza na kununua. Watu wanagombea madaraka. Wenye kupenda anasa wanajazana katika majumba ya starehe zao mashindano ya Farasi michezo yakamali. Ashiki kuu hutawala, na huku saa ya mlango wa rehema kufungwa inaharakisha na kila jambo karibu linakatwa kwa milele. Shetani amewaweka wakala wake wote shughulini ili wanadamu wadanganywe, na kupotoshwa, mpaka mlango wa rehema umefungwa milele. 

“Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu

WAKATI HUU KUNA MAMBO MATATU YANAYOENDELEA MBINGUNI ILI  KUKAMILISHA MCHAKATO WA MWISHO WA DUNIA MAMBO HAYO NI 

1. HUKUMU YA UPELELEZI,  HII INAFANYIKAJE MBINGUNI

Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye Mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji na nywele za kichwa chake kama sufi safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto; na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa” Daniel 7:9-10.

Haya ndiyo maono aliyopewa Daniel ya siku ile kuu ya hukumu ambayo maisha ya kila mtu yatakapopitishwa katika uchunguzi wa Hakimu wa dunia yote. Mzee wa siku ni Baba Mungu. Yeye ambaye ndiye asili ya maisha yote ya kila kitu, chemichemi ya sheria zote, ndiyo atakuwa mwenye kiti katika hukumu. Na malaika watakuwa wahudumu na mashahidi. 

“Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja na mawingu ya mbinguni akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa” Daniel 7:13-14. 

Kuja kwa Kristo kunakoelezwa hapa siko kurudi kwake mara ya pili duniani. Anakuja kwa Mzee wa siku huko mbinguni ili kupokea ufalme atakaopewa mwisho wa kazi yake ya uombezi. Kuja huko ndiko kulitokea mwaka 1844, wala si kurudi duniani mara ya pili. Hivyo ndiyo ilikuwa mwisho wa unabii wa siku 2300. Kuhani wetu Mkuu anaingia katika patakatifu pa patakatifu ili kufanya kazi yake ya mwisho ya kuwaombea wanadamu. 

Katika huduma ya hema takatifu hapa duniani, watu ambao dhambi zao zilihamishiwa kutoka patakatifu, ndivyo waliofaidi siku ya upatanisho. Hali kadhalika katika siku kuu ya uchunguzi wa mwisho, watu ambao yao yataangaliwa ni wale watu wa Mungu tu. Hukumu ya waovu itakuwa wakati mwingine. “Hukumu lazima ianzie katika nyumba ya Mungu” 1Petro 4:17. 

Vitabu vya kumbukumbu vya mbinguni vitahusika na uamuzi wa kesi ya kila mtu. Kitabu cha uzima kimeandikwa majina ya watu wote walioingia katika huduma ya Mungu. Yesu aliwaagiza wanafunzi wake, “Furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni”. Paulo anasema kuhusu wakazi wenzake, “ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima” Danieli asema kuwa watu wa Mungu wataokolewa, “Kila mmoja atakayeonekana ameandiwa kitabuni” Na mwandishi wa ufunuo “asema kuwa wale watakaoingia katika mji wa Mungu, ni wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana Kondoo” Luka 10:20 Wafilipi 4:3; Danieli 12:1; Ufunuo 21:27. 

Katika kitabu cha ukumbusho yamo majina ya matendo mema ya wale wamchao Bwana, na kulitafakari jina lake; Kila jaribu linapingwa, kila uovu unashindwa, kila neno la fadhili linalosemwa, kila tendo la kujinyima, na kila tendo la kusikitisha lililovumiliwa, kwa ajili ya Kristo, huandikwa. “Umehesabu kutangatanga kwangu, uyatie machozi yangu katika chupa yako. Je, hayamo katika kitabu chako?” Malaki 3:16; Zaburi 56:8.

                             WITO WA MUNGU LEO {YEREMIA 51:6-9}

Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha Bwana, atamlipa malipo.

7  Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Bwana; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.

8  Babeli umeanguka na kuangamia ghafula; mpigieni yowe; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.

9  Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni.

RAFIKI MPENDWA, USIKOSE SEHEMU YA PILI, ILI UWEZE KUJIANDAA  KWA AJIRI YA KUMPOKEA YESU KRISTO ANAYEKUJA MDA SI MREFU BARIKIWA SANA, KWA MASWALI,DUKUDUKU NA MAJIBU KARIBU KWA 0763371047 BY 24GOSPELNEWS.

 


Subscribe to receive free email updates: