MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

"SIO MBALI NA NYUMBANI YESU ANAKUJA TENA". SEHEMU YA KWANZA.

                                                            UFUNUO 14:6-7

Kisha, nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote na watu wa lugha zote na rangi zote. 7Naye akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na dunia, bahari na chemchemi za maji.”         

                                        Ufu 21:1-7

Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. 

Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

Ishara za mbingu na nchi zinatuonyesha kuwa Yesu anakuja tena. Na kwa sababu ya kifo chake msalabani ni lazima arudi kuwapatia waliomwamini tunu za imani zao.

Tunauhakika kuwa Yesu anakuja tena, tunarejea kauli yake 

mwenyewe alisema,


Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.” Yohana 14:3.
Ebrania 9:28 anasema, “kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu

Ufunuo 22:12 

Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake

ATAWATUMA MALAIKA ZAKE
Atawatuma Malaika zake nao watawakusanya wateule wake toka pande kuu nne za dunia, na waliokufa katika krito watafufuliwa kwanza, kisha sisi tulio hai tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu. Mathayo 24:31; 1Watesalonike 4:16,17.


KUJA KWA YESU NI UHAKIKA JIWEKE TAYARI NO MORE TIME


Subscribe to receive free email updates: