Binadamu
awezaje kuhesabiwa kuwa ni haki mbele ya Mungu ? Mwenye dhambi awezaje
kusahihishwa na kuwa kama asiyo na makosa machoni pake ? Kristo ndiye njia tu
ya kutupatanisha na Mungu na kutuweka katika hali ya usafi. Lakini twawezaje
kufika kwake Kristo ? Watu wengi wangali wakisema kama walivyosema wengine siku
ile ya Pentekota: “Tufanya je ?” Jibu la Petro lilikuwa hivi: “Tubuni.” Pengine
pia alisema hivi, “Tubu-ni basi, mre jee, ili dhambi zenu zifutwe.” Matendo
2:38; 3:19.
Kutubu
maana yake ni hivi: kuhuzunika kwa ajili ya dhambi, tena na kujitenga nayo
mbali. Katuwozi kuacha kufanya makosa mpaka tumetambua ubaya wake; tena hali
yetu katika maisha yetu haitabadilika kamwe mpaka tumeitenga dhambi mbali na
mioyo yotu.
Kuna
watu wengine ambao hawafahamu asili ya kutubu jinsi ilivyo halisi. Wengi huhuzunika
kwa ajili ya makosa yao, tcna hujaribu kuongoka katika mwenendo wao mbolo ya
watu, kwa kuwa wanaogopa adhabu ambayo watajipatia kwa ajili ya matendo mabaya.
Lakini huku si kutubu kama Mungu anavyotaka. Wao hufikiria adhabu zaidi ya
ubaya wa makosa yao. Hivyo ndiyyo alivyofanya Esau alipoona kwamba amepotewa
kabisa na urithi wake. Balaam pia, alipotiwa hofu sana kwa ajili yr kumwona
malaika aliyesimama mbele yake na upanga mkononi, akakubali kutiwa hatiani
asije akauawa; walakini hakutubu kwa kweli, hakugouka moyo, hakuchukizwa na
maovu. Yudas Iskeriota, aliponsaliti Bwana, alisema, “Nalikosa nilipoisaliti
damu isiyo na hatia.” Matt .27:4.
Alishurutishwa
kukiri makosa yake alipoona moyoni mwake jinsi alivyostahili kuhukumiwa na
Mungu kwa kosa lake. Lakini kitu kilichomtia hofu kilikuwa hukumu na adhabu ya
Mungu; hakuhuzunika sana moyoni na kuingiwa majuto kwa kuwa amemsaliti yule
mtakatifu Mwana wa Mungu, au kwa kuwa amemkana Mtakatifu wa Israeli. Farao pia,
alipoona maumivu ya Mungu alikiri makosa yake ili apate kuepuka na adhabu;
lakini mapigo yalipokoma, alizidi kufanya kiburi. Watu hao wote walililia mambo
yaliyotokea kwao kwa ajili ya makosa yao, lakini hawakuwa wakihununika na
kujuta kwa ajili ya makosa yenyewe na ubaya wake.
Lakini
kama mwenye dhambi anajitoa kuwa chini ya utawala wa Roho Mtakatifu, ndipo
dhamiri yake itakaposafisbwa, ataona barabara jinsi alivyo katika hali ya
kufanya dhambi, atafahamu maana na usafi wa amri za Mungu ambazo ndizo msingi
wa utawala wake. “Kulikuwako nuru halisi, intiayo nuru kila mtu ajaye katika
ulimwengu.” Ych.1:9. Nuru ile, ndiye Kristo, humtia mtu nuru moyoni, mambo ya
siri hufunuliwa, na yule mwenye dhambi hujiona jinsi alivyo na hatia machoni pa
Mungu mwenye haki kabisa. Pia huelewa upendo wa Mungu na uzuri wa kuwa katika
hali ya usafi na utakatifu; hutamani kusafishwa na kupatana na walio mbinguni.
Sala
ya Daudi baada ya kuanguka kwake dhambini hutudhihirishia vizuri namna ya kweli
ya kuhuzunika na kujutia maovu. Hakutaka kuli- punguza kosa lake, wala kuepuka
na hukumu iliyokuwa stahili yake. Daudi aliona kosa lake jinsi lilivyokuwa
kubwa mno; akaona unajisi wa moyo wake; akachukizwa sana na kosa lake. Hakuomba
ili apate kuachiliwa tu, akamba pia apate kusafishwa moyoni mwake. Akatamani
kuingia katika hali ya usafi na kuwa mmoja na Mungu. Akaomba hivi:-
“Heri
aliyesamehewa makosa, aliyestirikiwa dhambi,
Heri
mwanadamu, Bwana asiyemhesabia hatia,
Rohoni
mwake isipokuwa hila.”
Zaburi
32:1,2.
“Unirehemu,
Ee Mungu, kwa jinsi ulivyo mwema;
Rehema
zako zilivyo kuu, ufute makosa yangu.
Unioshee
kabisa hatia yangu, unitakasie dhambi zangu.
Kwani
nayajua makosa yangu: na dhambi yangu mbele
yangu
daima.........
Unisafishe
kwa ezobu, nami nitakuwa safi;
Unioshe,
nami nitakuwa mweupe kuliko theluji......
Uniumbie
moyo safi, Ee Mungu,
Ufanye
ndani yangu roho aminifu.
Usinitupe
usoni pako;
Usiniondolee
roho yako takatifu.
Unirudishe
furaha ya wokovu wako:
Unichukue
kwa roho bora……
Uniponye
kwa damu, Ee Mungu, Mungu wa wokovu wangu;
Na
ulimi wangu utaiimba haki yako.”
Zaburi
51:1-14.
Kutubu
namna ile hakuwezekani kwetu sisi kwa uwezo wetu wenyewe; kunawezekana katika
Kristo tu. Hapo ndipo wengi hupotea katika kudhani kwamba hawawezi kuja kwake
Kristo isipokuwa kwanza wamekwisha kutubia dhambi zao. Ni kweli mtu lazima
kutubia dhambi zake kwanza, ndipo Mungu atamwachilia; kwani bila masikitiko
moyoni kwa ajili ya makosa, mwenye dhambi hawezi kufahamu jinsi anavyomhita ji
Mwokozi. Je, mwenye dhambi hana budi kungo ja kumfikia Kristo mpaka ametubu ?
Katika
Biblia, Neno la Mungu, hatusomi kwamba mwenye dhambi hana budi kutubu kabla ya
kukubali mwito wa Kristo aliyesema,“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na
wenye mizigo, nami nitawapumzisha. “Matt.ll:28. Ni uwezo wa Kristo unaowezesha
watu kutubu kwa kweli. Petro ameeleza mambo hayo dhahiri aliposema, “Mtu huyo
Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli
toba na masamaha ya dhambi.” Matendo 5:31. Kwa kadiri tusivyoweza kusamohewa
dhambi bila Kristo, hivyo ndivyo tusivyoweza kutubu pasipo nguvu za Roho ya
Kristo mioyoni mwetu. Kristo ndiyo asili ya kila fikara njoma. Yoye tu ndiyo
awezaye kuutia moyo fikara ya kushindana na maovu. Kila aonaye noyoni mwake
haja ya kuwa na kweli na usafi, kila asadikiye hali yake ya dhambi, huwa
anashuhudia kwamba Roho Mtakatifu yumo moyoni mwake.
Yesu
amesema, “Nami nikiinuliwa juu ya nchi nitavuta wote kwangu.” Yoh.12:32. Mwenye
dhambi hana budi kumwona Yesu kama Mwokozi wetu aliyekufa kwa ajili ya dhambi
za ulimwengu; nasi tukimwona msalabani kwa macho ya kiroho, tutazidi kufahamu
mambo ya wokovu, tena wema wa Mungu utatuongoza ili tutubu. Hatuwezi kufahamu
barabara upendo wa Kristo jinsi ulivyomshurutisha afe kwa ajili yetu; lakini
upendo huo huivuta mioyo yetu kwake.
Pengine
watu huona aibu kwa ajili ya matendo mabaya yao, nao huacha kufanya mabaya
mengine, kabla hawajajua kwamba Kristo Yesu ndiye anawavuta kwake. Naye akizidi
kuwavuta macho ili wamwangalie msalabani na jinsi alivyopata maumivu kwa dhambi
zao, wao nao huzidi kufahamu ubaya wa mwenendo wao wanyewe, na kujua namna ya
haki yake Kristo. Nao huwa wanaanza kusema, “Je, dhambi ni kitu gani, ikiwa
imetakiwa dhabihu kubwa namna hii kwa kumwokoa mwenye dhambi ? Je, upendo wa
namna hii, maumivu haya yete, udhilifu huu, hivi vyote vilikuwa ni lazima ili
sisi tusipotee mbali, bali tupewe uzima wa milele ?”
Isipokuwa
mtu amekataa kuvutwa kwake Kristo, Roho yake itazidi kuugeuza moyo wake mpaka
ametubu na kuongoka moyo. Mambo ya kidunia hayawezi kutuliza moyo wa binadamu.
Furaha ya kweli hupatikana katika kumjua Kristo tu. Kwa njia nyingi,
zinazojulikana na zisizojulikana, Mwokozi hutumia sana kuwavuta watu kwake ili
waitoe mioyo yao mbali na anasa ya kidunia na kujua mibaraka ya Mungu isiyo na
mwisho. Wewe ambaye umetamani moyoni mwako kupata kilicho bora zaidi ya vyote
vya kidunia, heri ujue kwamba kutamani huko ni ile sauti ya Mungu anayosema
kwako.
Pengine
tumejisifu kwamba maisha yetu yamekuwa safi, dhamiri yetu imekuwa barabara,
hatuna haja ya kujitweza moyo mbele ya Mungu kama wabaya wengine; lakini nuru
ya Kristo ikituangaza roho zetu, tutaona hali yetu halisi, jinsi tunavyokuwa na
unajisi machoni pake; ndipo tutafahamu jinsi haki yetu inavyokuwa kama vitambaa
vichafu, tena ni damu yake Kristo peke yake ambayo huweza kutusafisha mioyo
unajisi wa dhambi na kutengeneza mioyo yetu tena kuwa katika hali ya kufanana
naye.
Mwonzi
mmoja wa nuru ya utukufu wa Mungu ukifikilia moyo ndani, umetosha
kutudhihirishia hali yetu katika dhambi, udhaifu wetu na upungufu wetu. Hivyo
twatambua tamaa zetu zisizo safi, jinsi tunavyomkana Mungu mioyoni mwetu, na
jinsi midomo yetu inavyotoa maneno yasiyofaa. Roho ya Mungu ikiupenya moyo
ndani, na kumjulisha mtu hali yake ya kumwasi Mungu, hapo ndipo hujichukia sana
akijilinganisha na Kristo jinsi alivyo safi bila mawaa yo yote.
Nabii
Daniel alipouona utukufu wa mjumbe wa Mungu aliyetumwa kwake, akabaini moyoni
mwake jinsi udhaifu na ukosefu wake ulivyokuwa mkubwa. Akasema, “Kazikusalia
nguvu ndani yangu: kwani uzuri wangu umebadilika mwangu kuwa uharibifu, wala
sikuwa na nguvu.” Daniel 10:8. Mtu akijiona hivyo kuwa si safi, ndivyo
atakavyotaka kuwa na moyo safi na kuingia katika hali ya kupatana na amri za
Mungu na kufanana naye Kristo.
Paulo
alipojichunguza aliona kwamba katika matendo ya nje alikuwa hana makosa; lekini
alipotambua matakwa ya sheria kwa njia ya kiroho, alijiona kuwa ni mwenye
dhambi kabisa. Kama alijipima kwa maneno ya sheria za Mungu jinsi wanavyopima
binadamu kwa matendo ya nje, Paulo alijiona kwamba amekuwa katika hali ya
kutofanya makosa, hakuwa na hatia; lakini alipoichunguza na kujua maana hasa ya
sheria, akajiona jinsi Mungu alivyomwona yeye, kuwa ni mwenye dhambi kabisa,
naye akajishusha moyo na kuungama makosa yake. Alisema, “Na mimi nalikuwa hai
hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, na mimi
nikafa.” Warumi 7:9. Alipoona asili ya sheria, jinsi ilivyokuwa ya kiroho,
ndipo aliona dhambi jinsi ilivyokuwa ya uovu, naye hakujiona tena kuwa ni bora.
Mungu
hazioni dhambi zote kuwa ni sawa; zinakadirika mbalimbali machoni pa Mungu kama
vile zinavyokadirika machoni pa binadamu pia. Lakini tendo baya liwalo lo lote,
ingawa linaonekana kuwa ni dogo machoni pa binadamu, hakuna dhambi
inayobesabiwa kuwa ni ndogo machoni pa Mungu. Hukumu ya kibinadamu si kamili,
kwa kuwa huona sehemu moja tu; hawezi kujua nia ya ndani ya mtu; walakini Mungu
hujua moyo tena hukadiri mambo jinsi yalivyo halisi. Mlevi hudharauliwa na
wenziwe na kuambiwa kwamba dhambi yake itamwacha asiingie mbinguni; lakini mara
nyingi makosa kama kufanya kiburi, kujifikiria mwenyewe bila kufikiri wengine,
kuwa na choyo, na mengineyo kama hayo hayakadirikiwi na binadamu. Lakini makosa
kama hayo yanachukizwa sana na Mungu; kwa kuwa yamekuwa kinyume kabisa cha sifa
yake Mungu mwenyewe. Yule ambayo hufanya dhambi zinazohesabiwa na binadamu kuwa
ni mbaya sana - yaani ulevi, kuiba, uzinzi na nyinginezo - mtu kama huyo huona
aibu na namna anavyomhitaji Kristo; lakini mwenye kufanya kiburi haoni lazima yake,
naye humfungie Kristo asiingie moyoni mwake, na kwa hivyo hukosa kupata
mibaraka yake.
Yule
mtoza ushuru aliyeomba, “Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi,” alijiona
kwamba yu mtu mbaya sana, na wengine pia wakamwona hivyo; lakini yeye alijua
shida yake, naye alimletea Mungu mzigo mzito wake wa dhambi kwa haya, ili Mungu
amrehemu na kumtoa katika utumwa wa dhambi. Luka 18:13. Yule Mfarisayo
aliyefanya kiburi na kujifanya mwenye haki katika sala zake, akaonyesha kwamba
amemfungia Roho Mtakatifu mlango wa roho yake, asiingie. Kwa hivyo. hakujiona
jinsi alivyo na unajisi; hakuona jinsi anavyouhitaji msaada wa Kristo, naye
hakupata kubarikiwa kamwe.
Ukitambua
hali yako jinsi ulivyo katika dhambi, usingojee kumwendea Kristo mpaka ume
jaribu mwenyewe kujitengeneza kuwa safi. Wengi hufikiri kwamba hawawezi
kumfikia Kristo kwa kuwa ni wabaya. Je, unafikiri utapata kuwa mwema kwa uwezo
wako mwenyewe ? “Aweza Mkushi kubadili ngozi yake, au chui madoadoa, ndipo
nanyi mtaweza kutanda moma, mliofundishwa kutenda mabaya.” Yer.13:23. Kakuna
msaada kwetu ila kwa Mungu tu. Sisi wenyewe hatuwazi kitu. Imetulazimu kwenda
kwake Kristo kama tulivyo.
Hata
hivyo tusijidanganyo katika kufikiri kwamba Mungu, kwa neeraa yake, atawaokoa
hata wale wanaotupia mbali neema yake na rehema zake. Afikiriye hivyo, afadhali
aitazame Kalwari. Kwa kuwa hakuna njia nyingine ya kuwaokoa watu, kwa kuwa bila
dhabihu aliyoifanya Kristo katika kufa kwake msalabani. binadamu asingeweza
tena kuwa katika hali ya kupatana na watakatifu wa mbinguni - kwa hivyo Kristo
alichukua mwenyewe dhambi za wakosaji, akaadhibiwa kwa ajili yao. Upendo wa
Mwana wa Mungu, maumivu yake, na kufa kwake, hivi vyote hushuhudia jinsi dhambi
inavyokuwa kubwa mno machoni pa Mungu; pia mambo hayo yatudhihirishia kwamba hakuna
njia ya kuokoka na kutoka katika utawala wa uovu, hakuna matumaini ya uzima
bora wa milele, ila kwa kujiweka chini ya mamlaka yake Kristo na kumtii. Wenye
mioyo migumu wasiotubu, pengine hujisingizia wakisema hivi juu yao wanaojisifu
kuwa ni Wakristo, “Hata mimi ni mtu mwema kwa kadiri wanavyokuwa wema wale, Wao
hawajinyimi zaidi ya mimi; mimi najiweza jinsi wafanyavyo. Wao pia hupendezewa
na anasa ya kiaunia kama nipendezewavyo mimi.” Hivyo watu kama hao hujisingizia
kwa ajili ya makosa ya wengine ili wasifanye wajibu wao. Lakini kujisingizia
hivyo hakufai kitu; kwa kuwa Bwana ametuwekea mfano usio wa kibinadamu, bali
Mwana wa Mungu, asiye na ila wala kosa lo lote, yeye ndiye mfano wetu. Wale
ambao hunung unika kwa ajili ya mwenendo mbaya wa wengine wanaojisifu kuwa ni
Wakristo, imewapasa kufuatisha maisha na matendo ya Kristo, na kuwatolea
wengine namna ya mfano ulio bora. Wamejua namna iwapasavyo Wakristo kufanya;
hivyo wakikosa wenyewe kufanya yaliyo mema, makosa yao ni makubwa zaidi.
Tuangalie
tusifanye usiri. Tusichelewe kuziacha dhambi zetu na kutaka usafi wa moyo
katika Yesu. Watu wengi hukosa katika jambo hilo; hukawia katika kujitoa kuwa
wa Kristo; wafanyao hivyo wanachagua kuishi katika hali ya kufanya dhambi. Kitu
ambacho tunakosa kukishinda, kitatushinda sisi na kutuangamiza.
Adam
na Hawa walijidanganya kwamba kula matunda yaliyokatazwa si kosa kubwa
linaloweza kuadhibiwa kama Mungu alivyosema. Lakini katika jambo hilo dogo
walihalifu amri takatifu ya Mungu, amri isiyobadilika; kwa hivyo binadamu
akatengwa mbali na Mungu, tena kifo na taebu viliingia duniani mwetu. Kufa
kwake Yesu katika Kalwari, kama dhabihu, kulikuwa njia ya pekee ya kufanya
upatanisho tena kati ya Mungu na binadamu. Tusidhanie dhambi kwamba si kitu
sana.
Kila
tendo baya, kila mara unapoidharau na kuitupia mbali neema ya Kristo, moyo wako
huzidi kuwa ngumu, nia yako huzidi kuwa mbaya, nawe huzidi kuwa katika hali ya
kutosikia maombezi ya Roho Mtakatifu moyoni mwalco.
Watu
wengi huwa wakijituliza dhamiri na mawazo yanayowasumbua, wakidhani kwamba
wataweza kugeuza mwenendo wao mbaya wakati wo wote watakapo; wao hufikiri
kwamba waweza kutupa na kutosikia wito wa Roho siku nyingine, tena watakuwa
wakichomwa moyo mara kwa mara baadaye. Lakini sivyo. Hata tabia mbaya moja tu,
ama namna moja ya tamani isiyofaa, ikidumu moyoni itathibitisha moyo katika
kutopenda Mungu. Kwa maonyo yote katika Biblia juu ya kuchezacheza na maovu,
lile la kututiisha zaidi ndilo hili, linalose, “Maovu yake yatamkamata mwovu
mwenyewe, naye atashikwa kwa kamba ya dhambi yake. Methali 5:22.
Kristo
amekuwa tayari kutuweka huru kwa dhambi, lakini ha- lazimishi watu kwa nguvu;
kama mtu amekusudia kufanya dhambi, naye hataki kupata uhuru katika Kristo,
Kristo angefanya nini tena ? Mtu akifanya hivyo amejiharibu mwenyewe kwa ajili
ya kukana upendo wake Kristo. Tumeambiwa, “Sasa ndio wakati uliokubalika sana;
tazama, sasa ndio siku ya wokovu.” “Leo, kama mtasikia sauti yake, msifanye
migumu mioyo yenu.” 2 Wakor.6:2; Waeb,3:7,8.
“Wanadamu
hulitazama umbo la nje, lakini Bwana hutazama moyo.” 1 Sam.l6:7. Mungu
huutazama moyo wa kibinadamu jinsi ulivyo ukaidi, panapokuwa unajisi na
udanganyifu. Mungu hutujua kabisa, moyo wetu, dhamiri yetu, makusudi yetu na
maazimio yetu. Nenda kwake jinsi ulivyo na moyo usio safi, na mwambie,
“Unitafutetafute, Ee Mungu, uni jue moyo; unijaribu, uni jue mawazo; utazame
kama njia ya kukasiri sha mwangu, unichukue kwa njia ya milele.” Zaburi
139:23,24.
Watu
wengi hukubali dini katika akili zao tu, na kufanya matendo matupu ya nje tu,
bila kugeuzwa moyo. Imekupasa kuomba hivi, “Uniumbie moyo safi, Ee Mungu;
ufanye ndani yangu roho aminifu.” Zab.51:10. Heri ujitahiai ili usipotewe na
uzima wa milele kwa jinsi watu wafanyavyo kujiokoa maisha ya sasa wakiwa
hatarini. Heri ufanye bidii katika kusoma Neno la Mungu pamoja na kuomba.
Katika Neno hilo, kwa njia ya amri za Mungu na maisha yake Kristo, tumeonyeshwa
asili ya utukufu, “ambao hapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao.”
Waeb.12:14. Neno lile husadikisha watu kuwa ni wenye dhambi, tena huonyesha
njia ya kupata wokovu. Heri ulisikilize kama sauti ya Mungu inayosema nawe
moyoni mwako.
Kama
umefahamu dhambi jinsi ilivyo mbaya sana, na kujiona mwenyewe jinsi ulivyo
katika hali ya kufanya dhambi, usikate tamaa. Kristo alikuja ili awaokoe wenye
dhambi. Si juu yetu kufanya patanisho kati ya Mungu na sisi, lakini katika
Kristo Mungu mwenyewe alifanya patanisho. “Mungu alikuwa ndani ya Kristo,
akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” 2 Wakor.5:19. Hakuna hata mzazi wa
kibinadamu ambaye angefanya saburi juu ya makosa ya mwanawe jinsi Mungu
anavyofanya kwa wale atakao kuwaokoa. Ahadi zake zote, hata na maonyo yake
yote, ni kwa ajili ya upendo wake tu, upendo usioelezeka hasa jinsi ulivyo.
Kama
Shetani anakuambia kwamba wewe ni mwenye dhambi, mwangalie Mwokozi wako na
kuongea juu ya tabia na sifa zake. Ziungame dhambi zako na mwambie adui kwamba
“Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi.” 1 Tim. 1:15. Yesu
alimwuliza Simon swali juu ya wadeni wawili. Mmoja alikuwa anamwia bwana wake
pesa kidogo, na mwingine mapesa mengi, naye bwana yule aliwaachilia wote
wawili; na Kristo akamwuliza Simon ni nani atakayempenda bwana wake zaidi.
Simon alimjibu, “Nadhani ni yule aliyesamehewa naye mengi.” Luka 7:43
Sisi
tumekosa sana, lakini Kristo alikufa ili tupate kuachiliwa dhambi. Wale ambao
amewaachilia zaidi, wao ndio watakaompenda zaidi na kukaa karibu naye, tena
kumsifu zaidi katika ufalme wake kwa ajili ya upendo wake na dhabihu
aliyoifanya kwa ajili yao. Tukifahamu sana upendo Mungu jinsi ulivyo, ndivyo
tutakapozidi kufahamu dhambi jinsi ilivyo mbaya mno. Na jinsi tunavyozidi
kufahamu kama Kristo alivyojinyima kwa ajili yetu, ndivyo tutakavyozidi
kuchomwa moyo na kujitoa kwake kuwa watu wake kabisa.
Nilikupa
wewe
Damu
ya moyoni,
Ili
wokolewe,
Winuke
ufuni:
Nimekunyimani
wewe;
Umenipa
nini ?
Nilikupa
myaka
Yangu
duniani;
Upate
inuka,
Kuishi
mbinguni;
Nimekunyimani
wewe;
Umonipa
nini ?
Nimekuletea,
Huku
duniani,
Pendo
na wokovu,
Zatoka
mbinguni;
Nimekunyimani
wewe;
Umenipa
nini ?
NDUGU ZANGU TUACHE DHAMBI MAANA HATIMA YAKE NI MOTONI TUU
UJUMBE HUU UMELETWA KWENU NA CHARLRES SHIBITA PUNDA WA YESU
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NUMBER 0763371047