MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

BADILIKO LILITOKA WAPI? -SEHEMU YA KWANZA:

                                


   Moja kati ya kitu kigumu sana kwa mwanadamu, nikuukubali ukweli unaobadilisha msimamo fulani juu ya maisha yake,kama itikadi ya dini ambayo kalisi kutoka kwa wazazi wake au mafundisho fulani kutoka shuleni ama chuuoni, Leo nina hoja nahaitaji tujifunze kwa lengo la kupata ukweli uliofichwa chini ya pazia la "DINI" hoja hii inasema badiliko lilitoka wapi, ikiwa ukristo awali ulikuwa ni dini moja? nini kilitokea hadi kikaleta mabadiliko ya kuwa na madhehebu mbalimbali duniani?.      

                                                         "chukua hii itakusaidia "

Inakadiriwa kwamba Duniani kuna madhebu ya Kikristo yasiyopungua 46,000, na haya madhehebu Yote, kila dhehebu linadai kuwa lipo sahihi kuliko lingine, mbaya zaidi ni kwamba asilimia kubwa ya madhehebu haya yote hutumia Biblia moja.

      Wakorintho 1:12-13.

Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo .   

                                         WAEFESO 4:5-6

Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; na Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya wote, anayefanya kazi katika yote na aliye ndani ya yote. 

                                                 YOHANA17:10-12

Yote niliyo nayo ni yako, na yako ni yangu; na utukufu wangu umeonekana ndani yao. 11 Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.

Mathayo 5:37
‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.
SWALI, kuna nini nyuma ya pazi kilichofichika?, ukweli ni upi!
Matendo ya Mitume 20:28-30.
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.
miaka 600 kabla ya KRISTO kuzaliwa nabii Daniel alionyeshwa habari ya badiriko hili ambalo lingetokea wakati wa mitume yaani baada ya KRISTO kuzaliwa, kufa na kufufuka soma. Daniel 7:25 na daniel 8:12-14
Baada ya Mitume wengi kufa kanisa lilianza kuingiliwa na mbwa mwitu ambao Paulo aliwatabiri; Kuanzia mwaka wa 100-313BC Kanisa la Kristo lilianza kupitia Mateso makali kutoka kwa Wapagani wa Kirumi, Wapagani hawa waliona watu wanazidi kupungua kwenye upagani na kujiunga na Ukristo, na hivyo njia pekee ya kudhoofisha Ukristo ilikuwa ni kuwauwa. Miongoni mwa wafalme katili waliotesa kanisa la awali ni kama NERO, Gnaeus Domitius ,Claudius,Flavia Domitilla,Vespasian, Tito na wengine wengi.

Hii ni sehemu ya kwanza, karibu sehemu ya pili tujue kwanini leo tuko hapa nini kilitokea na badiriko hili lina madhara gani kwa mkristo wa leo :sawa" kuna mengi ya kujifunza  juu ya hili badiriko. MUNGU akubariki sana kwa maswali na mjibu piga simu 0763371047 by punda wa Yesu.

Subscribe to receive free email updates: