MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

BABELI NINI?, NI KITU GANI NA KILIANZA LINI NA KWANINI BABELI ?

 ILI UELEWE LAZIMA UKUBARI KUJIFUNZA, NA ILI UJIFUNZE LAZIMA KWANZA UONDOWE MISAMO AMA ITAKAIDI FULANI FULANI EIDHA YA KIDINI AMA YA KIELIMU HAPO UTAKUWA MWANAFUNZI MZURI UTAKAYE JUWA MENGI "BY SHIBITA.COM"                                :

SWALI LA KUJIULZA,   BABELI NI NINI?, NI  KITU GANI NA KILIANZA LINI  NA KWANINI BABELI  IMETAJWA SANA AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA KUNA NINI HAPA?  HAPANA    RAFIKI KARIBU TUJIFUNZE HABARI ZA BABELI MAANA KUNA SIKU BABELI ITAANGUKA WALA HAITA SIMAMA TENA 

                        UFUNUO18:21.

Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana tena.

                     MWANZO WA BABELI.

Jina Babeli lina maana kuu mbili,maana ya kwanza ni MACHAFUKO  Mwanzo 11:1-9  na maana ya pili ni   LANGO LA MIUNGU AU MASHETANI kwanini ni lango la miungu kwa sababu chanzo cha ibaada ya kumwabudu shetani kilianzia pale mfano ilikuwa na mahekalu 300, madhabahu 905 ilikuwa na miumgu zaidi ya 500,chanzo soma habari za herodotus juu ya babeli anasema babeli kilikuwa ni kituo kikuu cha dini kisicho na upinzani dunia.

           WAANZILISHI WA BABELI YA KALE {NIMROD MWAKA 1751 bc }

 Biblia kitabu cha mwanzo kinasema mwanzo 10:8-10

 Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.

           LENGO LA KUUJENGA MNARA WA BABELI.

Walitaka wakae sehemu moja kinyume na matakwa ya MUNGU.Ikumbukwe MUNGU alimuagiza Nuhu waende wakatawanyike mbele ya uso wa nchi,lakini wao wakaamua kufanya kinyume na amri ya MUNGU ili wajitwalie utukufu wao wenyewe (KIBURI).

Dhambi kubwa iliyofanya MUNGU awachafulie usemi wao ilikuwa "Na tujifanyie jina wenyewe",Je wakati huo kulikuwa nchi ambayo walikuwa wanataka kushindana nayo?je walitaka nani awasifu?kulikuwa na nchi ya jirani? ila walikuwa  wanashindana na MUNGU mwenyewe.

             NIMROD ALIKUWA NA MAKUNDI MATATU.


1.Kundi la kwanza lilikuwa kwa ajiri ya kumuua MUNGU
2.kundi la pili walikuwa na kazi ya kutengeneza mishalie kwa ajiri ya kumuua MUNGU
3.Kundi la mwisho kwa ajiri ya ujenzi wa babeli 
 Tembelea (skiba 2012) kwa mapitia .

Hapo ndipo utakapogundua kuwa Nimrodi alitaka kwenda kukaa kwenye kiti cha enzi cha MUNGU.
Hayo yote ndiyo yaliyomchukiza MUNGU na kuamua kuwachafulia usemi wao ili wapate kujifunza na kuwalazimisha kugawanyika  mbele ya uso wa MUNGU.

HII INAENDA SAMBAMBA KABISA NA ANGUKO LA SHETANI KWA KUTAKA KUWA KWENYE KITI CHA ENZI CHA MUNGU


Chini ya nimrodi mambo mengi ya kishetani yaani ibaada za kishetani nyingi zilianzishwa mfano ibaada ya kuabudu jua, mwezi, sayari, wafu na masanamu mbalimbali, vile vile sherehe mbalimbali zilianzishwa kama vili ISHTAR ambyo imetoholewa na kuitwa EASTER, CHRISMASS PIA IMETOKEA HUKO NA SHEREHE NYINGINE NYINGI.

       NABII EZEKIELI 8:9-16  ANAELEZA MUUNDO HUU ULIVYOASIRI WATU.
Naye akaniambia, “Wewe mtu, toboa ukuta huu.” Nami, nikatoboa, nikaona kulikuwa na mlango. 9Naye akaniambia, “Ingia ndani ukaangalie machukizo mabaya wanayofanya humo.” 10Basi, nikaingia, nikaona sanamu za wadudu na za wanyama wa kila aina ya kuchukiza na vinyago vyote vya miungu ya Waisraeli, vimechorwa kuuzunguka ukuta. 11Na mbele ya sanamu hizo walisimama wazee sabini wa watu wa Israeli pamoja na Yaazania mwana wa Shafani. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi, na moshi wa ubani ulipanda juu. 12Kisha Mungu akaniambia, “Wewe mtu, umeona wanayotenda wazee wa Waisraeli gizani, kila mtu katika chumba chake cha sanamu. Wanadai ati Mwenyezi-Mungu hatuoni. Mwenyezi-Mungu ameiacha nchi.” 13Tena akaniambia, “Bado utaona machukizo makubwa zaidi wanayotenda.”
14Kisha akanichukua mpaka lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko kulikuwa na wanawake wameketi wakimwombolezea Tamuzi. 15Mungu akaniambia: “Wewe mtu, umeyaona hayo? Bado utaona machukizo mengine makubwa kuliko hayo.”
16Kisha akanipeleka mpaka ua wa ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Huko mlangoni mwa hekalu, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwapo wanaume wapatao ishirini na watano, wakilipa kisogo hekalu, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki. Walikuwa wanaabudu jua wakielekea upande wa mashariki.

"KUNA SWALI KWANINI MUNGU ANATOA WITO KAMA HUU"
                             YEREMIA 51:6-8
Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo. 7Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu. 8Babeli umeanguka na kuangamia ghafula; mpigieni yowe; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.

SWALI! LA KUJIULIZA KWA NINI BABEL IMETUHUMIWA NA MUNGU SANA NA WITO WA KUKIMBIA UNATOLEWA JE KUNA NINI?  BABELI YA LEO NI IPI NA IKO WAPI? NA INASHIDA GANI? SOMO HILI LITAENDELEA SEHEMU YA PILI RAFIKI  USIKOSE KUSOMA SEHEMU YA PILI YAMKINI MIMI NA WEWE TUKAWA BADO TUKO BABELI." KARIBU SANA SEHEMU YA PILI.?


Subscribe to receive free email updates: