MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

"TUMAINI PEKEE KWA MWANADAMU"

 



Kuna wakati kama binadamu, tumefikia hatua ya kuona kuwa hakuna tumaini la kuisha, eidha kwa sababu ya MAGOJWA yaliyokosa majibu, matatizo ya NDOA,UCHUMI MBOVU,VITA ISYOKOMA NA MENGINE MENGI, NO! hapana rafiki usikate tamaa bado lipo tumaini  kubwa la mafanikio na solution ya matatizo yako, Solution hii inatolewa na SHUJA WA KARINE ZOTE, YEYE NI MFALME WA AMANI YA KWELI IDUMUYO MILELE , Hebu tuone habari zake huyu shuja wa karine zote.

                               MATHAYO 11:28-30

Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu. Maana, nira 
niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

                     ISAYA 9:6

NABII ISAYA Alizaliwa mnamo mwaka 760 k.k na aliitwa rasmi katika huduma ya kinabii mnamo mwaka 742 Wakati huo taifa la kiyahudi lilikuwa limesambaa kiasi ambacho kumbukumbu za uwepo wa MUNGU zilikuwa zimefifia kwa kiwango kikubwa sanaa, watu walikuwa wamekosa tumaini lakuishi na hatima yao ya baadae ilikuwa ni giza, totoro ndipo nabii wa MUNGU Isaya akaja na ujumbe wa matumaini kwao na kwetu

Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu, tumepewa mtoto wa kiume. Naye atapewa mamlaka ya kutawala. Ataitwa: “Mshauri wa Ajabu”. “Mungu Mwenye Nguvu”, “Baba wa Milele”, “Mfalme wa Amani”

Rafiki haijarishi magumu kiasi gani unapitia leo wewe siyo wa kwanza wapo waliopitia magumu kiasi cha kufa lakini walisimama imara sana na hatima yao ilikuwa ni furaha ya kushangaza.

Ombi langu kwako rafiki mpendwa, usikate tamaa tunaye shujaa wa karine zote ni "YESU KRISTO" AMBAYE KABURI LAKE LIKO WAZI HATA LEO, MAANA MAUTI HAIKUWAEZA KUMSHINDA Yeye alishinda kila changamoto aliyokutana nayo hata wewe leo ukimwani USHINDI NI "HAKIKA"

Haijarishi utakufa leo hata ukifa leo kesho atakufufua, chagua leo kumwani KRISTO ili kesho uapate uzima milele MIMI NIMEMCHAGUA KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WANGU WEWE JE?.

Mwanzo 18:14 " Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?" Biblia inajibu Luka 1:37 "kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.". 

 KWA MASWALI, USHAULI NA MJIBU PIGA 0763371047

Subscribe to receive free email updates: