MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

MGUSO WA IMANI : SEHEMU YA KWANZA.

Je! kuna matatizo yanayokutesa na umekosa majibu, umeenda hospitari, kwa waganga mbalimbali, umetafuta msaada kwa wanadamu lakini umekosa na umekataa tama, mpaka sasa umeacha iwe itakavyo kuwa! usikate tamaa leo nina habari njema kwako.

WANADAMU WANAMIPAKA, KWASABABU WAO NI WAO , LAKINI  HABARI NJEMA NI HII
YUPO MUNGU ASIYEZUILIWA NA KITU CHOCHOTE NA ANAWEZA KUFANYA CHOCHOTE KWA KUWA HAKUNA NENO LISILOWEZEKENA KWA MUNGU LUKA 1:37.


Kuna wakati kama binadamu, tumefikia hatua ya kuona kuwa hakuna tumaini la kuisha, eidha kwa sababu ya MAGOJWA yaliyokosa majibu, matatizo ya NDOA,UCHUMI MBOVU,VITA ISYOKOMA NA MENGINE MENGI, NO! hapana rafiki usikate tamaa bado lipo tumaini  kubwa la mafanikio na solution ya matatizo yako, Solution hii inatolewa na SHUJA WA KARINE ZOTE, YEYE NI MFALME WA AMANI YA KWELI IDUMUYO MILELE , Hebu tuone habari zake huyu shuja wa karine zote.


Yesu aliporudi upande wa Magharibi wa ziwa kutoka Gergesa, aliwakuta makutano yamekusanyika wakimngojea. Alikaa pwani muda kitambo, akiwafundisha watu na kuponya maradhi yao. Kisha akaenda nyumbani kwa Lawi Mathayo ili kuhudhuria katika karamu. Hapo Yairo mkuu wa sinagogi alikutana na Yesu. Akiwa na masikitiko makubwa, alimwambia, “Binti yangu yumo katika hali ya kufa. Nakuomba uje uweke mkono wako juu yake ili apone; naye aishi.”

Yesu akaondoka mara moja kwenda kwa Yairo. Wanafunzi wake walistaajabu kwa ukubali wake wa kwenda kwa Rabi huyu, walakini walifuatana na Mwalimu wao, na kundi la watu pia. Yesu na wanafunzi wake waliendelea pole pole sana, maana makutano walikuwa wakimsonga pande zote. Baba wa mgonjwa alikuwa na wasiwasi kwa kusimama mara kwa mara kwa Yesu ili kuwasaidia wenye dhiki, au kuwafariji wenye mashaka.

Wakati walipokuwa wangali njiani, mjumbe alifika na kutoa habari kuwa binti wa Yairo amekwisha kufariki. Yesu alisikia hivyo, akasema: “Usiogope, amini tu, binti yako atapona.

Basi wakaenda kwa haraka mpaka nyumbani kwa mkuu huyo. Waombolezaji walikuwako tayari wamejaza mji na makelele. Yesu alijaribu kuwayama-zisha, akisema: “Mbona mnafanya ghasia hiVi? Msichana hakufa, ila amelala.” Walichukizwa kwa maneno ya mgeni huyu. Wamemwona kijana akifa wazi. Yesu alipotaka waondoke wote, aliwachukua babaye na mamaye, pamoja na Petro, Yakobo na Yohana, wakaingia pamoja katika chumba alimolala marehemu.

Yesu alikaribia kitanda cha maiti, akaukumbatia mkono wake kama deaturi yao, akasema: “Msichana, nakauagiza ondoka.”  Akaondoka mara moja kwa kutetemeka, akapita katika watu wenye kushangaa, macho yake yamekodolewa sawa na mtu atokaye usingizini, akiangaliwa kwa mshangao mkubwa na watu wote waliokuwa hapo. Wazazi wake wakamkumbatia kwa furaha isiyosemeka.

Walipokuwa njiani wakienda kwa mkuu huyu, Yesu alikutana na mwanamke maskini, ambaye alikuwa amesumbuliwa na ugonjwa kwa muda wa miaka kumi na miwili. Alikuwa ametumia mali yake yote kwa waganga bila kupona. Lakini aliposikia kuwa kristo yuko, akawa na matumaini. Kama angemfikia tu angepona. Kwa shida akajikokota polepole mpaka pwani. Yesu alipokuwa akifundisha watu, akajaribu kumsogelea, asiweze. Akamfuata katika nyumba ya Lawi Mathayo, lakini hata huko hakuweza kumfikia kwa asababu ya makutano. Alikuwa katika kukata tamaa, wakati Yesu aliposogea karibu naye. 

Alikuwa karibu na Mganga Mkuu! Lakini kwa ajili ya ghasia nyingi na fujo kubwa, hakuweza kusema naye, wala kutazamana naye. Akiwa na hofu na wasiwasi wa kutokubaliana naye na kumweleza hali ya matatizo yake, alijisogeza kuelekea kwake, huku akijisemea mwenyewa: “Nikimgusa pindo la vazi lake, nitapona.” Yesu alipokuwa akipita, mwanamke huyu alinyosha mkono wake, akaweza kugusa upindo wa vazi lake. Katika mguso huo, ndipo alipoweka tumaini lake lote. Wakati huo huo udhaifu wake na ugonjwa wake ukapona kabisa.

Akajaribu kuondoka katika mkutano huo kwa furaha ya moyo wake, lakini wakati huo huo Yesu alisimama. Akiangalia huku na huku, aliuliza kwa sauti ya kusikika: “Nani amenigusa?” Swali hilo lilionekana kuwa ni swali la kigeni, maana alikuwa akisongwasongwa na makutano pande zote.

Petro aliyekuwa tayari kusema, alisema: “Bwana makutano yanakusonga-songa, nawe wauliza: “Nani amenigusa?” Yesu alisema, “Maana naona nguvu zimenitoka”. Mwokozi aliweza kutambua mguso wa imani, na miguso-guso tu ya kawaida. Mguso wa imani hauwezi kupita ovyo tu. Angesema mwanamke huyu maneno ya faraja yataka yodumu mpaka mwisho wa dunia.

Akiwaangalia watu, Yesu aliweza kutambua yule aliyemgusa. Alipoona kuwa amefahamiwa, mwanamke alijitokeza wazi, akaja akitetemeka, akaeleza habari za ugonjwa wake, na jinsi alivyopata waokovu kwa Yesu. Ndipo Yesu akasema. “Binti.... Imani yako imekupnya, nenda zako kwa amani.” Hakumpa nafasi ya kueleza kwamba kuponywa kwake kumetokana na mambo ya ushirikina ya kugusa nguo na kupata uwezo wa kupona kimwujiza. Imani kamili ya kutegemea uwezo wa Mungu ndiyo imemponya.

                                                    IMANI HAI HUPONYA.

 Kuzungumzia dini kwa njia ya bahati nasibu tu, kuomba vivi hivi bila kusikia haja rohoni, ni kazi bure. Imani ya juu juu ambayo ni ya jina tu, inayomtaja kristo kuwa ni Mwokozi wa ulimwengu basi, haiwezi kuleta uhai wa roho ya mtu. Imani siyo elimu ya kujua kawaida za dini tu, wala haitoshi kusema kuwa namwamini Yesu Kristo. Yatupasa tumwamini na kumtegemea. Imani ya kweli ni hali ya kazi ya maagano ya lweli ya muungano kati ya Mungu na mtu. Kuwa na uhusiano halisi kati ya Mungu na sisi. Imani ya kweli ni kutumaini kwa kweli, kunakofanya ushindi katika maisha ya mtu.

Baada ya kumponya mwanamke yule, Yesu alitaka akiri mibaraka aliyopokea. Kipaji kinachotolewa na injili si cha siri. Ungamo letu la uaminifu wake ni chombo cha mbinguni cha kumdhihirisha Kristo ulimwenguni. Mambo muhimu katika dini yetu ni ule uaminifu wetu wa kweli katika kanuni za Mungu. Isaya 43:12. Ukubali wa neema yake unapoungwa na hali yetu ya kikristo katika maisha yetu, huwa uwezo unaoleta wokovu kwa watu.

 Watu wenye ukoma kumi walipomjia Yesu wakitaka kuponywa, waliponywa. Lakini ni mtu mmoja tu aliyerudi kushukuru. Ni watu wangapi leo hufanya mambo kama hayo? Bwana humponya mgonjwa, huwatoa watu katika hatari, huwaagiza malaika zake wawaepushe watu na hali za lika namna, na kuwalinda na uharibifu wa maradhi, (Zaburi 91:6); ni hivyo hawajali upendo huo ulio mkuu. Kwa kutokuwa na shukrani hufunga mioyo yao isiione neema ya Mungu. Ni kwa ajili ya faida yetu tu, kulinda vipawa vya Mungu anavyotupatia. Hivyo imani ni nguvu inayoimarishwa. Basi tukumbuke upendo wa Mungu na fadhili zake kwetu. Tunapojikumbusha fadhili za Mungu, na jinsi anavyotntendea, husema: “Nimrudishie Bwana nini, kwa ukarimu wake wote alionitendea?” Zaburi 116:1.

Subscribe to receive free email updates: