MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

HOFU, UGONJWA MBAYA SANA SEHEMU YA PILI.

 Mnamo mwaka  1912 meli ya titanic Ilipangwa kuzunguka kwenye Atlantiki kati ya Uingereza na Marekani.

Kwenye safari yake ya kwanza iligongana na siwa barafu yaani ice beg  tar. 14 Aprili 1912, hofu kuu ilitanda miongoni mwa abilia waliokuwemo  na mnamo saa sita kasorobo usiku ikazama baada ya masaa 2 na dakika 40 katika usiku wa tar. 15. Aprili, Watu 2200 walikuwepo kwenye meli, Katika maji baridi takriban 1500 walikufa ni 700 waliookolewa na meli zilizokimbia kuokoa watu. na ni kina mama na watoto hao ndio waliookolewa

Katika ajari hiyo kuna watu walikufa bila tumaini la kutubu dhambi zao, mbele za MUNGU muumbaji wa mbigu na nchi, hii ni kwa sababu ya hofu ya kifo, hofu hii huletwa na adui mkuu Shetani, akiwa na lengo moja tu, mwanadamu afe bila kuwa na tumaini la kupata uzima wa milele.

Wakati ulimwengu ukihangaika na majanga mbalimbali kama vile ugaidi, magonjwa majanga ya asili, vita vya wenyewe kwa wenyewe, Shetani anaingiza  kombola kuu kwa wakaazi wa sayri dunia na kombola hili ni HOFU ambayo imewafanya binadamu kuishi kwa hatia,kukosa matumainina hatimaye kukataa tamaa.

Wazazi wa kwanza yaani adamu na hawa, walipoigia kwenye hatia ya dhambi mwanadamu hakuwa na uwezo wa kuishi milele maana mwili wa kuishi milele uliondolewa na kisha wakabaki na mwili wa kufa na hivyo suala la kifo kwa mwanadamu halikwepeki lakini ikumbukwe ya kwamba kifo  kilicho tangazwa pale Bustanini Eden siyo hichi kifo ambacho watu wanakufa leo la hasha hapana hapa watu wanakuwa wamelala usingizi wakisubiri kifo cha milele au uzima wa milele siku ile KRISTO ATAKAPO HUKUMU ULIMWENGU.

MAANDIKO MATAKATIFU YANASEMA

Ayubu 22:21

Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; ndivo mema yatakavyokuijia.
YOHANE 16:32-33
32 Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


Subscribe to receive free email updates: