SIYO MPANGO WA MUNGU KUWEPO KWA MADHEHEBU MENGI DUNIANI.
MOJA KATI YA MADA TATA NA CHANGAMOTO KWA WATU WENGI NI UWEPO WA MADHEBU MENGI DUNIANI NA CHANZO CHAKE LEO, TUTAJIFUNZA JUU YA CHANZO CHA KUWEPO KWA MAHEHEBU MENGI DUNIANI.
SWALI LANGU NA LAKO, #KWANINI KUNA #MADHEHEBU #MENGI?
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili #DHEHEBU ni kikundi cha dini Fulani chenye mwelekeo tofauti na kikundi kingine cha dini hiyo hiyo. Inakadiriwa kwamba Duniani kuna madhebu ya Kikristo yasiyopungua 46,000, na haya madhehebu Yote, kila dhehebu linadai kuwa lipo sahihi kuliko lingine, mbaya zaidi ni kwamba asilimia kubwa ya madhehebu haya yote hutumia Biblia moja, Ukweli ni kwamba uwepo wa madhehebu mengi sio mpango wa Mungu hata kidogo. Lakini wakati wa mitume kanisa lilitaka kuanza kugawanyika na kuunda madhehebu, na mitume walikemea vikali sana juu ya mgawanyiko huo:
1 #Wakorintho 1:12-13 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? Kanisa la Kristo huko Korintho lilitaka kuanza kugawanyika katika makundimakundi(madhehebu) na Paul akakemea vikali sana kwamba tabia ya kugawanyika katika makundi sio sahihi, je Kristo amegawanyika? Nasi hebu tujiulize leo tabia ya kusema mimi kanisa langu ni KKKT, EAGT, ANGLIKANA,SDA, TAG, RC, FULLGOSPLE FREE PENTECOSTE,JESHI LA WOKOVU NK.
Je, hayo madhehebun yalikufa pale msalabani? Jibu ni hapana, au Je, Kristo amegawanyika hata aongoze kila dhehebu likawa sahihi? Watu wengi siku hizi tumebaki kukumbatia madhehebu hata kama fundishi ni lakipagani, mtu hayupo ladhi kuliacha, kisa anaogopa kuliacha dhehebu lake, Yaani kanakwamba mbinguni watu wanaenda kwa tiketi za madhehebu yao. Wapendwa mbinguni hatuendi kwa sababu unasali dhehebu Fulani, Bali tunaenda mbinguni kwa kutii kweli ya Mungu inayofundishwa katika dhehebu. Kwa hiyo Dhehebu hata liwe zuri vipi, lakini kama halifundishi kweli ya Biblia achana nalo unapoteza muda tu.
#NB: Ogopa Sana dhehebu linalomilikiwa na mtu binafsi au Familia, dhehebu lolote linalomilikiwa na mtu, hilo sio kanisa wala dhehebu, kamwe kanisa la kweli halimilikiwi na mtu. Mitume walikemea vikali Sana suala la Madhehebu.
Wakati mtume Paul akiwa Efeso na ikiwa ni ukingoni mwa huduma zake za utumishi, Paulo alitoa angalizo juu ya mpasuko katika kanisa la Mungu: #Matendo ya Mitume 20:28-30. Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Paul akaweka pia msisitizo katika kanisa la Efeso:
#Waefeso 4:3-6 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
Kinachoonekana siku hizi ni tofauti na kile kiliochokuwa kipindi cha Mitume, siku hizi utasikia mtu anakwambia kila mtu na imani yake, kila dhehebu lina imani yake na ubatizo wake. Ni wapi umepata fundisho Kama hili ya kwamba kila mtu na imani yake? Ina maana kama kila mtu na imani yake, basi pia kila mtu ana Mungu wake na Yesu wake na Roho wake.
Fundisho la Biblia IMANI NI MOJA TU. Paulo alishaanza kuona Dalili za ukengeufu kwa kanisa la Mungu, na ndio maana akatoa angalizo litakalo jitokeza baadaye. Na Yuda anapotazama Kanisa la Mungu anaona tayari kuna ukengeufu unataka kuingia kanisani, na ndipo Yuda akasema
#Yuda 1:3-4 .Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.
Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Yuda anaona tayari kuna mbwa mwitu wameanza kujiingiza kwa siri ndani ya Kanisa la Mungu lengo ni kutawanya kondoo wa Bwana, na hivyo anaweka msisitizo kwamba waishindanie IMANI waliokabidhiwa Watakatifu, ina maana kwamba kuna imani ngeni zilianza kuinuka, kama ilivyo siku hizi kila mtu anasema ana imani yake. Baada ya Mitume wengi kufa kanisa lilianza kuingiliwa na mbwa mwitu ambao Paulo aliwatabiri;
Kuanzia mwaka wa 100-313BC Kanisa la Kristo lilianza kupitia Mateso makali kutoka kwa Wapagani wa Kirumi, Wapagani hawa waliona watu wanazidi kupungua kwenye upagani na kujiunga na Ukristo, na hivyo njia pekee ya kudhoofisha Ukristo ilikuwa ni kuwauwa. Lakini jitihada za kuua hazikuzaa matunda Kwa sababu Kwa kadri walivyowauwa Wakristo ndivyo watu walizidi kujiunga na Ukristo na hivyo ikabidi hawa wapagani wabuni mbinu nyingine; ambayo ni kuingiza UPAGANI ndani ya Ukristo, ili baadala ya kumuabudu Mungu watu wauabudu upagani wa Rumi humo humo kwenye makanisa yao.
Kwa hiyo kuanzia mwaka wa 313 wapagani wakatangaza malidhiano kati yao na Wakristo na mauaji yakakoma, na wapagani wakiongozwa na Kostantino Wakadai wapo tayari kubatizwa ili na wao wawe Wakristo. Kwa muono wa haraka lilionekana ni jambo jema, lakini ndipo ulipoanzia Ufa wa Upagani kuingia ndani ya kanisa. Kikundi hiki cha wapagani walipoingia tu ndani ya kanisa, haraka sana wakalitawala Kanisa, Na ndipo wakaanza taratibu kuchukua upagani wao na kuuingiza Kanisani na ili ukubarike ilibidi wabadili majina, #Mfano; Ili waingize masanamu ndani ya kanisa ilibidi majina yatumike ya Kikristo, Sanamu ya #Tamuzi wakaiita ni Yesu, Sanamu ya #Semilamis wakaiita Mariamu, Sanamu ya# Nimrodi wakaiita Yusufu. Ibada za wafu zikaingia, sikukuu za kipagani zikaingia, lakini pia hata Ibada ya siku ya Jumapili ikaingia.
Na watu wengi hawafahamu chimbuko la ibada ya jumapili, wanadanganywa kwamba ilianza kipindi cha mitume hapana, chimbuko lake ni hapa kwa hawa wapagani, Katika kitabu cha Romani Catholic kinachoitwa HISTORIA YA KANISA KATIKA VIPINDI VYAKE SABA. UK. 24, wanasema “Mwaka 313 Kaisaria Kostantino hakukawia kutangaza uhuru wa kanisa kwa “Tangazo la Milano”. Basi Wakristu walipata uhuru uleule wa dini kama wapagani. Walirudishiwa makanisa na mali waliyokuwa wamenyimwa wakati wa udhalimu.
Kaisaria alitangaza pia Jumapili iadhimishwe kama “Siku ya Bwana”, na watu waukumbuke ufufuo wa Kristu” Ni dhahiri kabisa kwamba Wakristo waliteswa mwanzo kuanzia mwaka wa 100, na sasa baada ya kubuni njia nyingine ndipo makanisa yaliyokuwa yametekwa na wapagani yakarudishwa na uhuru wa kuabudu ukarejeshwa, na ndipo Jumapili ikaanza kuadhimishwa kama siku ya Bwana, na watu wakaanza kupumzika na kuto kufanya kazi, kwa hiyo kwa kadri watu walivyozoea kupumzika
Jumapili, na taratibu siku ya Sabato ikaanza kufanywa ya kazi mwisho Jumapili ikafanywa pia iwe siku ya Ibada mpaka leo. Jumapili ilikuwa ni siku ya pekee sana kwa wapagani wa Kirumi, maana waiitenga kama siku yao maalumu ya kumuabudu mungu jua, na hivyo haingewezekana waabudu Jumamosi na Jumapili pia waabudu, Maana wangegundulika mapema, na hivyo ilibidi waiondoe kwanza Sabato na kuisimika Jumapili ambayo ni yakumuabudu mungu jua. Kuanzia hapo Mapokeo mengi yakaingizwa Kanisani na wale waliojaribu kuhoji juu ya mapokeo walishughulikiwa ipasavyo, wengi waliuawa kwa kuchomwa moto na kufungwa magerezani na wengine wakakimbilia maporini. Kuanzia mwaka 538 Kanisa lilikuwa gizani Ukweli wote ulimezwa na wapagani wa Kirumi.
Biblia zilifichwa, ibada ziliendeshwa kupitia vitabu vilivyoandikwa na wanadamu na sio Biblia. Mtu akitenda dhambi baadala ya kuungama kwa Yesu, waliungama kwa Viongozi wa Dini au waliuziwa vitambulisho vya msamaha, na wengine ili kusamehewa Dhambi ilibidi wapate adhabu. Kwa ufupi kanisa lililofanya hayo yote ni Kanisa la Kirumi/ Roman Cathoric ambalo mwanzo ulikuwa ni Upagani. Ukweli ni kwamba Romani Cathoric sio Dhehebu la Kikristo, bali ni Upagani uliovaa vazi la Kikristo.
#CHANZO CHA #MADHEHEBU MENGI #KUTOKEA.
Baada ya giza hili la kiroho kudumu kwa muda mrefu: Mungu ikabidi aangaze Nuru, Kupitia makasisi na mapadre. Waliinuka watu na kuanza kuhubiri ujumbe wa kweli, lakini waalimbulia kuchomwa moto na kufungwa magerezani: Baadhi ya watumishi hao ni: JOHN WYCLIFFE(1321-1384) alichomwa moto JOHN HUSS(1365-1415) alichomwa moto JEROME(1365-1416) alichomwa moto. Ijapokuwa walichomwa kwa moto kwa kuitetea kweli lakini hadi wanateketea sauti zao zilipazwa kwa kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu.
Walikuwa na ujasiri wa kukabiri kifo kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa ndani yao. Lakini Mungu hashindwi na jambo lolote, ijapokuwa watumishi hao walikufa Mungu alimuinua #Martin #Luther aliyekuwa Kasisi katika Kanisa Katoliki, na akaongozwa na Roho Mtakatifu kujua mafundisho potofu katika kanisa Katoliki.
#Martini Luther alikuwa ni miongoni mwa Makasisi waliokuwa na nia ya dhati ya kuujua ukweli, na alijitahidi kuhakikisha matendo yake yanakuwa mema tu, Lakini bado moyoni hakuwa na amani kutokana na vitendo vilivyokuwa vikiendelea katika Majumba ya Watawa, maana kulikuwa na anasa zilizopitiliza, Fedha walizotozwa watu kwa msamaha wa dhambi ndio zilitumika katika Anasa.
Martin Luther alibahatika kupata Biblia na akagundua suala la kuuza na kununua Msamaha ni makosa, maana Biblia inasema Tunaokolewa kwa kwa Neema kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Kitendo hiki kilimfanya Martin Luther aanze kupingana na baadhi ya viongozi juu ya kuwauzia watu msamaha wa dhambi, Na kutokea kwa Luther watu wengi ndipo wakaanza kufumbuka macho juu ya mapokeo yaliyomo katika Kanisa la Katoliki. Siku moja Martini Luther aliandaa orodha ya hoja 95 za kupinga Uuzaji wa Msamaha, kisha akabandika kwenye Mlango wa Kanisa, Watu wengi walivutiwa na zile hoja.
Tangu hapo Martini Luther akapata wafuasi waliounga mkono hoja zake, Kisha uongozi ulimuita Martin Luther ili akane hoja zake, lakini Martini Luther alihitaji ushahidi kwenye Biblia ni wapi #Papa, #Maaskofu na #Mapdri wamepewa jukumu la kuuza msamaha wa dhambi!! Bahati mbaya hakukuwa na majibu yoyote kutoka kwenye Biblia.Kuanzia hapo Martini Luther na Wafuasi wake wakaitwa #WAPRONTESTANT, Yaani #WAPINZANI WA #KATOLIKI.
Baada ya Martini Luther kujitenga ndipo mwanga ulianza kuonekana kwa watu wengine kugundua upagani uliomo Katoliki. Baadhi ya Madhehebu yaliyojitenga na Katoliki ni 1. LUTHERANI. Ni Kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa Martini Luther. 2. ANGLIKANA. Lilianzishwa na Mfalme Henry. Baadaye likazaliwa Kanisa la METHODIST 3. PRESBYTERIAN. Lilianzishwa na John Calvin na baadaye likazaliwa kanisa la MASHAHIDI WA YEHOVA 4. MEMONITE. Lilianzishwa na Zwingli, ambaye alikuwa mkatoliki na walikuwa kundi moja na Martin Luther, lakini baadaye walitofautiana na yeye akaanzisha Kanisa hilo. 5. MORAVIANI ni Kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa John Huss ambaye alichomwa moto na kanisa Katoliki. 6. BAPTISTI.
Wao walijitenga na kanisa Katoliki kwa kusimamia fundisho la Ubatizo, Kigezo kikubwa cha kujitenga ni kwamba walipinga ubatizo wa watoto wadogo na ubatizo wa kunyunyiza, Kwa hiyo hata jina la Dhehebu lao ikabidi liendane na msingi wa fundisho lao la Ubatizo. Kupitia hayo madhehebu na mengine mengi ambayo hayajatajwa, ndio chimbuko la madhehebu yaliyopo na yanayoendelea kuongezeka Duniani.
Kiufupi ni kwamba chanzo cha kuinuka kwa Madhehebu kuwa mengi ilisababishwa na Kanisa la Awali kuruhusu wapagani wa Kirumi kujiunga na kanisa, kisha kanisa likamilikiwa na wapagani na ndio matokeo ya kutokea kwa Kanisa Katoliki. Ukweli ni kwamba Katoliki kwa Asili halikuwa kanisa la Kikristo, bali ni Upagani uliovaa vazi la Kikristo. Wakatoliki wengi hudai kwamba Makanisa Yote yametoka Katoliki ni KWELI, lakini hawasemi sababu iliyopelekea watu kujitoa Kanisani na kuanzisha madhehebu mengine. Chanzo Kikubwa ni kwamba watu walikuwa wanakimbia #UPAGANI uliomo ndani ya Kanisa Katoliki.
Sasa kilichosababisha zaidi Madhehebu kuongezeka ni kwamba wale Waasisi waliotoka Katoliki hawakutoka na Ukweli wote, bali walitoka na ukweli Robo, na Robo tatu nyingine ni Upagani uleule wa Katoliki. Na hivyo ikawa inapelekea tena baada ya mtu kujua Ukweli zaidi ya ule wa kwanza naye anajitoa kwenda kuanzisha Kanisa lake.
Wengine wakigombana ndani ya kanisa, basi mmoja wapo anajitenga na kuanzisha kanisa, Wengine wameanzisha Makanisa kwa sababu ya kugombania vyeo. Hivyo Madhehebu mengi ya Kikristo bado yanaendelea kufuata baadhi ya mafundisho potofu ya Katoliki, ijapokuwa hudai kwamba walijitenga, lakini kwa kuendelea kufuata mafundisho potofu ya Katoliki inakuwa haina maana tena ya kujitenga. Na ndio maana Biblia inaliita Kanisa Katoliki ni mama wa Makahaba: #Ufunuo wa Yohana 17:5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri,
BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
Kanisa hili linaitwa mama wa makahaba kwa sababu ya kukosa uaminifu wa mafundisho ya Kristo na Kushikamana na mapokeo ya Kipagani, Na hivyo madhehebu yote ambayo yanafuata mapokeo yake ni Mabinti zake na Katoliki ni mama. #Ezekieli 16:44 Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake. Kwa hiyo asilimia kubwa ya mafundisho katika madhehebu ya Kikristo ni yale ya Kutoka Katoliki. Baadhi watahoji vipi juu ya SDA mbona halijatajwa? Ukweli ni kwamba Kanisa la Kweli la mitume lilikuwa ni la Watunza sabato, Lakini baada ya upagani kuingia kanisani Ibada ya siku ya Sabato iliondolewa na Kostantino, na jumapili ikaingizwa kama siku ya kupumzika na kufanya ibada baadala ya Sabato: Katika kitabu cha Romani Catholic kinachoitwa HISTORIA YA KANISA KATIKA VIPINDI VYAKE SABA. UK. 24
, wanasema: “Mwaka 313 Kaisaria Kostantino hakukawia kutangaza uhuru wa kanisa kwa “Tangazo la Milano”. Basi Wakristu walipata uhuru uleule wa dini kama wapagani. Walirudishiwa makanisa na mali waliyokuwa wamenyimwa wakati wa udhalimu. Kaisaria alitangaza pia Jumapili iadhimishwe kama “Siku ya Bwana”, na watu waukumbuke ufufuo wa Yesu.
Kwa hiyo baada ya Jumapili kusimikwa, ikabidi wale wote waliokuwa wanapinga mapumziko na kufanya ibada siku ya Jumapili ikabidi waanze kuuawa na wengine wakakimbilia Maporini na wakawa wakiendelea kumuabudu Mungu kwa kificho, na ndio kipindi hiki Yohana analiona kanisa likiwa nyikani.
#Ufunuo wa #Yohana 12:14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Hivyo watunza sabato walikuwepo nyakati zote lakini kwa kificho, maana walikuwa wanasakwa sana, Lakini baada ya Marekani kutangaza Uhuru wa kuabudu, watu hawa ilibidi waanze tena kujitokeza, na ilipofika mwaka 1845 ikabidi waanze kuchapa vijarida vinavyohusu Umuhimu wa Ibada ya siku ya sabato, Vijarida hivyo vilisambazwa kila mahali katika Nchi ya Marekani, Na asilimia kubwa waliokutana na vile vijarida walikiri ni kweli Sabato ni moja ya Amri kumi na kuna wajibu wa kuitunza, Hivyo wachungaji wengi wa jumapili waliupokea ujumbe huo na wakaachana na ibada ya jumapili, Vijarida hivi viliwafikia pia Ellen G White na Mume wake James White, nao ikabidi wajiunge na kundi hilo.
Na hivyo mwaka 1860 kundi hili likaitwa “Seventh Day Adventist” (SDA), Ikiwa na maana kwamba ni Watu wanaosubiri Marejeo ya Yesu Kristo mara ya Pili, na kukumbuka Ibada ya siku ya saba, ambayo madhehebu mengine yameitelekeza, Na ndio Dhehebu pekee ambalo kwa Aslimia kubwa bado linaendelea kupinga mafundisho Potofu ya Katoliki, Na shetani analiandama sana Kanisa la SDA kwa sababu ya Utii wa Amri kumi zote na imani ya Yesu; #Ufunuowa #Yohana 12:17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari. #Ufunuo wa Yohana 14:12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Ukweli ni kwamba watu wengi wanafanya kazi ya kulichafua dhehebu hili la SDA kila siku, wakati ndio dhehebu lenye ukweli kimafundisho, Hiyo yote ni kazi ya Shetani, ili watu wasijue ukweli kupitia SDA. Na mikakati ya Katoliki ni kuyarejesha madhehebu yote ya Kikristo yaliyotoka kwake, na mikakati hiyo inaendelea kupitia
#UMOJA WA #MAKANISA. #WITO WA #MUNGU NI
#KWAMBA: #Yohana 10:16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. #Yeremia 6:16 Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu.
Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo. Je, ni kweli hapo ulipo ni katika zizi la Kristo au ni zizi la Ibirisi na inabidi uitike wito wa kutoka huko? Je, ni kweli umesimama katika njia kuu(Dhehebu) sahihi? Au upo kwenye njia panda zilizotengenezwa na wanadamu? Huu sio muda wa kuendelea kushikilia mapokeo ya wanadamu, Huu ni muda wa kuitafuta kweli. #Mathayo 7:13-14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Itafute njia nyembamba na mlango mwembamba. Watu wengi wanadai kwamba SDA kuna sheria ngumu, usiogope hivyo ni vitisho vya shetani maana Biblia inasema: #Wafilipi 4:13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Huu sio wakati wa kupenda injili laini za kufurahisha moyo wako, injili za Miujiza, Utajiri, Uponyaji, Amani NK. Huu ni wakati wa kutafuta injili itakayofanya moyoni ujione unamuhitaji Yesu akusaidie kutii kweli.
#Isaya 30:9-10 Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana; wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
MUNGU AKUBARIKI: BY:PUNDA WA YESU, TUPIGIE
. 0763371047 0675355220
KUMBUKA, WOKOVU NI KWAKO NA MAAMUZI NI YAKO, ACHANA NA MISIMAMO YA DINI KUBALI KUJIFUNZA, MAARIFA NA UELEWA HUJA KWA NJIA YA KUJINZA. MIMI NILICHAGUA KUJINZA WEWE JE? CHAGUA HIVI LEO ILI UPATE KUELEWA MENGI ZAIDI. MUNGU AKUBARIKI SANA .