HOFU, UGONJWA MBAYA SANA SEHEMU YA KWANZA.
TAFASIRI YA NENO HOFU HUFASILIWA KWA MANTIKI YA WOGA,MASHAKA UTISHO KUTOKURIDHIKA AU KUWA NA WASIWASI FULANI MAISHANI LAKINI KI BIBLIA NAI ZAIDI YA HAPO:
NAKUMBUKA MWAKA 2019 BAADA YA TANGAZO LA UGONJWA WA KORONA MAARUFU KAMA COVD 19 KUGUNDLIWA HUKO CHINA NA BAADAYE KUENEA MAENEO MENGI DUNIANI, UGONJWA HUU ULISABABISHA HOFU KUU DUNIANI KOTE IKIWEMO NA TANZANIA NA KAMA ASINGE KUWA RAISI WETU KWA KTUMIWA NA MUNGU WA MBINGUNI, SIPATI PICHA TANZANIA TUNGEKUWA WAPI KWA HOFU ILIYOKUWA IMETANDA KILA KONA YA INCHI YETU,
Imeandikwa Wafilipi 4:6- 7 " Msisumbukie kwa neno lo lote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu na amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."
KWA KAWAIDA HOFU IMEGAWANYIKA SEHEMU KUU TATU YAANI, HOFU JUU YA MUNGU,HOFU JUU YA MWANADAM NA HOFU JUU YA VIUMBE HAI NA VISIVYO HAI TUANZE NA HOFU JUU YA MUNGU IKOJE IKOJE:
HOFU JUU YA MUNGU
Unapoongozwa na roho ya dhambi na mauti unapata matokeo ya hofu,mashaka,wizi,tamaa,uasherati,ibada ya sanamu,uchoyo,wivu,hasira na mengine mengi yafananayo na hayo
Mfano, mzuri hapa ni YUDA mwanafunzi wa YESU, YUDA alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa YESU alikuwa msomi sana wa mambo ya uchumi, na kwa elimu hiyo alikuwa pewa cheo cha kuwa mtunza hazina wa Kanisa la kwanza liliLokuwa likiongozwa na YESU pamoja na wanafunzi kumi na mbili yaani mitume wa YESU, Mtu huyu baada ya kumsaliti BWANA wake aliingiwa na HOFU KUU, iliyompelekea kufanya maamzi magumu, ya kujinyoga
Kuwa na hofu ni kupoteza muda. Imeandikwa katika Luka 12:25-26 "Na yupi kwenu ambaye ajisumbua ambaye aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja basi ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo kwa nini kujisumbua na hayo mengine?."
Mpe Mungu hofu zako. Imeandikwa katika 1Petro 5:7 "huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishuguliza sana kwa mambo yenu
Kwa kila jambo linalokupa haijarishi ni zuri au baya mshukuru MUNGU wa mbinguni, maana hata AYUBU wakati wote wa ugonjwa wake kauli yake ya mwisho ilikuwa ni hii
Ayubu 22:21
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako". habari hii itaendeleea.