Nyumani hatimaye, nihamu ya kila mtu kufika nyumbani, tangu wazazi wetu wa kwanza wameumbwa ule mwaka wa 2004 BC waliishi katika furaha na raha maisha yao , hapakuwa na alama ya yoyote ya dhambi iliyoonekana katka maisha yao ya EDENI,
LAKINI baada tu mama yetu wa awali yaani HAWA kuingia kwenye shida hii ya kushawishiwa na nyoka hapo ndipo mambo yalipoharibika na kujikuta wanadamu wote tumekuwa wakimbizi katka nchi ya ya ugeni ambamo ndimo tulimo sasa.
Lakini MUNGU wetu wa mbinguni hakutuacha hivi hivi, kwa sababu ya upendo wake usio na mwisho MUNGU aliandaa mpango wa ukombozi, na mpango huo kwa mala ya kwanza ulitangazwa pale Edeni,kwa kumchuinja mwana kondoo kwa ajiri ya kuwavisha wazazi wetu wa kwanza, vazi la haki ambalo tayari walikuwa wamelipoteza, na hivyo KONDOO aliwakilisha vitu vikuu vitatu, 1. kifo cha KRISTO 2. VAZI la haki lilopotea ambalo awali walipatiwa kama sehemu ya kujistiri aibu yao 3. madhara ya dhambi na mwisho wake.
SWALI, nyumbani hatimaye maaana yake nini, ukweli ni kwamba, baada ya dhambi kuingia tu, Makao yetu ya awali ambamo ndimo tulimo takiwa kuishi milele, tuliondolewa na kwenda kuwa wakimbizi katika nchi iliyo laniniwa, ambomo kifo, magonjwa, na shida mbalimbali vinaendelea kutusumbua, jama vile wana waisrael kuridi katika nchi ya ahadi ilikuwa shauku kubwa kwao hata sisi leo ni shauku kubwa kwetu kurudi nyumbani(nyumbani hatimaye) yohana akishuhudia numbani kwetu jinsi palivyo aliandika akasema...
ufunuo21:1-7
kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake.
Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya.
Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho.
Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
OMBI LANGU, TUWEPO WOTE KATIKA HAFURA YA NYUMBANI HATIMAYE., mada hii itaendelea..usikose sehemu ya pili.