KITABU CHA UFUNUO 13 MAANDIKO YANASEMA KWAMBA 1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi,
na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake
majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama
niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na
kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake
cha enzi na uwezo mwingi.
4 Wakamsujudu yule joka
kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama,
wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita
naye?
5 Naye akapewa kinywa
cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi
arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake
amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya
vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na
lugha na taifa.
8 Na watu wote wakaao
juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha
uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
9
"Mtu akiwa na sikio na asikie"
Kuwa mkristo maisha
yako yote nakisha ukapokea alama ya mnyma katika saa ya mwisho
ya historia ya ulimwengu, huo utakuwa msiba mkubwa,na wakutisha sana .
Alama ya mnyama itakuwa ni hatua ya mwisho katika uasi zidi ya MUNGU, lakini utakuwa ni uasi uliofichwa kwa werevu sana kuliko mwingine ambao shetani amewahi kuwashirikisha wanadamu katika uasi wake, litakuwa ni jaribu lake kubwa kuliko yote ambayo amewahi kuwahusisha wanadamu kwanini?.
kwasababu ya mambo makuu matano anayoyaandaa ambayo ni
1.alama ya mnyama itakuja imeavaa ukristo.
2.itabuniwa wakati wa mdololo mkubwa wa uchumi
3. itatangazwa wakati wa janga kubwa la badiliko la hali ya hewa
4.alama ya mnyama itakuja kama suluhisho la ugaidi duniani
5.alama ya mnyama itakuja kama suluhisho la magonjwa dunia
Wakati huo itaonekana kuwa ni laziama watu wote waungane ili kuepusha janga la ulimwengu mziama na itaonekana kwamba alama ya mnyama ndio ufumbuzi pekee, hivyo neno la MUNGU hutuambia kuwa mtu yeyote atakayepinga atatishwa vikali na mamlaka hiyo tunayasoma yote haya katika kitabu cha ufunuo 13 na 14
LAKINI MASWALI YA KUJIULIZA NI HAYA,
1.ALAMA YA MNYAMA NI KITU GANI HASA.
2 NA KINAKUWAKUWAJE HASA, JE?
3. NI NAMBA HALISI YAANI 666.
4.AMA NI KITU FULANI KILICHOFICHIKA KATIKA MAANA HALISI YA UNABII.
hakika mada hii itaendelea hadi mwisho wa maswali yetu tajwa hapo juu
MUNGU AKUBARIKI, ZAIDI AKUEPUSHE NA HII HOJA YA MPINGA KRISTO YAANI ALAMA YA MNYAMA napatikana kwa namba za simu kama utakuwa na maswali piga simu namba 0763371047