Biblia inasema hapao mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi Mwanzo 1:1
Hii inamaana ya kwamba vitu vyote tunavyoviona duniani na angani na hata tusivyoviona viumbwa na MUNGU kwa uwezo wa ajabu na mkuu mno asioweza kuuelewa mwanadamu MUNGU anauwezo mkubwa sana.
Hakuna hata mtu mmoja hata kama atakuwa na elimu ya juu kiasi gani, anayewez kufahamu sayansi yote ya MUNGU aliyo itmia kuumba vitu, Binadamu anafahamu kidogo sana maana uwezo wa kuhamu una mpaka, yaani yeye ni mwanadamu atabaki kuwa mwnadamu
Biblia inasema: "Mambo ya siri in ya Bwana, MUNGU wetu; lakin yaliyofunuliwa kwetu ni yetu sisi" na watoto wetu milele " Kumbukumbu 29:29 hii ina maana kwamba mambo mengine ya vitu alivoviumba MUNGU hatuwezi kuvifahamu kabisa .
lakini tutakapofika mbinguni tutafunuliwa habari za mambo ambayo tulishindwa kuyaelewa hapa duniani na tutaendelea kujifunza mambo mapya chini ya Mwalimu YESU, na wala hatuyaelewa yote
japo tutajifunza milele zote , maana mambo aliyoyaumba MUNGU ni mengi sana nayaajabu mnokiasi ambacho kuyajifunza ni kazi kubwa, kumbuka kuwa MUNGU ni wa milele na amekuwa akiumba vitu vya milele zote
Tunapojifunza ukuu wa MUNGU kupitia mambo ya anga,zaidi tuanangalia sana habari ya nguvu na uweza uliyotukuka kuliko kawaida, hivyo wanadamu wamekuwa wachunguzi wa mambo ya anga zaidi wamekuwa wakitumia vyombo zaifu ambavyo kwavyo wakati fulani waekuwa wakipoteza maisha pamoja na mabilioni ya fedha.
Kwahiyo ni maombi yangu kuwa yale tutakayojifunza yataongeza uwezo japo kidogo kumfahamu MUNGU zaidi na jinsi alivyo mkuu na baada ya kufahamu alivyo mkuu sifa na utukufu zimendee yeye mile na milele
Watu wengi hawajui nyota ni kitu gani na wengine wanazielewa nyota kwa namna isyo sahihi, Hivyo katika sura inayofuata tutajifunza nyota ni kitu gani, imeumbwa kwa kutumia kitu gani na tutajifunza habari ya familiya za nyota, ni uhakika kwamba utafurahia kujua habari za nyota na familiya yake, naamini pia kwa kuelewa habari za nyota kw ausahihi,kutakufanya na uongeze ufahamu wako juu ya muumbaji wako na wangu yaani "MUNGU "
NYOTA INAYOITWA JUA
Watu engi sana wanaelewa kidogo sana na pengine kwa makosa , kuhusu habari za nyota nini, kwa mjibu wa wataalamu nyota ni nyota ni kitu kikubwa ambacha hakina uhai kinacho elea angani nacho hutoa nuru na joto bila kuteketea hivyo ili kujifunza na kujua vizuri juu ya nyota ,ni vizuri kujifunza jinsi Jua lilivyo kwa maana jua ni nyota
JUA ni nyota kama zilivyo nyota zingine angani, daima jua linaonekana kuwa kubwa kukliko nyota zingine kwa sababu, JUA liko karibu nasi, JUA liko umbali wa kilometer miloni 149.5 ambazo ni sawa na maili 93,000,000 kutoka kwenye sayari yetu dunia.
Nyota zina majina, nyota ilyo karibu nasi, inayotumlika inaitwa JUA, nyota JUA.inakipenyo cha maili 865,000 au kilometer 1,400,000 wakati dunia yetu inakipenyo cha maili 7,918 to hivyo sasa, JUA ni kubwa mara 109 zaidi ya dunia.
JUA limeumbwa kwa hewa zizotoa joto nuru,Hizo hewa ni Hydrogen,ambayo in asilimia 75 ya mwili wa jua na hew hii ya hydrogen iko sehemu ya nje ya mwili huo wa JUA.katikati ya jua .JUA limeumbwa kwa Helium ambayo ina asilimia 25 ya mwili wa jua. zaidi ya hayo kuna asalimia 0.1ya mwili wa jua iliyoumbwa kwa hewa ya oxygen na nitrogen.
JUA hutoa joto kali sana kwani, joto la jua ni ni centgrade 5500 kwa nje, wakati katikati ya JUA ni joto 15,000,000 centgrade, hilo ni joto kubwa sana ambalo MUNGU, kwa uwezo wake ameliweka liweze kumlikia sayari zingine ikiwemo sayari Dunia ambayo pia nayenyewa hupata nuru yake kutoka kwa jua, yote haya yanathibitisha ukuu wa MUNGU na uweza wake hauchunguziki soma kitabu zaburi 19:1
Zaburi 19:1-14 BHN
somo hili litaendele kwa kina zaidi, ombi langu kwako usiishie hapa bali endelea kuujua ukuu wa MUNGU kupitia anga za juu, MUNGU akubariki sana endelea kubarikiwa mtu wa BABA .