Hekalu la Mungu lilifunguliwa huko mbinguni, ndipo sanduku la
agano lake likaonekana katika hekalu lake”. Ufunuo 11:19. Sanduku la agano la
Mungu jipya liko mbinguni katika patakatifu mno, chumba cha pili cha
patakatifu. Katika huduma ya hema takatifu duniani, ambayo ilikuwa mfano wa
kivuli cha ile ya mbinguni, chumba hiki kilifunguliwa tu wakati wa siku kuu ile
ya upatanisho kwa ajili ya kutakasa patakatifu. Kwa hiyo upatanisho kwa ajili
ya kutakasa patakatifu. Kwa hiyo tamko lile lisemalo kuwa hekalu la Mungu
lilifunguliwa, na kwamba sanduku la ushuhuda likaonekana, lilikuwa utangulizi
wa kuonyesha kuwa patakatifu mno mbinguni palikuwa tayari kufunguliwa katika
chumba cha pili ili Kristo, Kuhani wetu Mkuu yuko tayari kuingia na kuanza kazi
hiyo mwaka 1844. Watu ambao wangefuatana naye katika huduma hiyo, waliona sanduku
la agano lake. Kadiri walivyojifunza juu ya hekalu waligundua kuwa Kristo
anabadili huduma na sasa anahudumu mbele ya agano la Mungu.
Sanduku lililokuwa katika hema takatifu hapa duniani
lilikuwa na mbao mbili za mawe ambazo zilikuwa zimeandikwa juu yake sheria ya
Mungu. Hekalu la Mungu lilipofunguliwa huko mbinguni, sanduku la agano lake
lililonekana humo. Sheria hii ilionekana katika patakatifu pa patakatifu
iliyonenwa na Mungu na kuandikwa na kidole cha chanda chake juu ya mbao mbili
za mawe.
Wale walioelewa fundisho hili walifahamu vyema maneno ya
Mwokozi yasemayo: “Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka; yodi moja wala nukta
moja ya torati haitaondoka” Mathayo 5:18. Sheria ya Mungu ambayo ndiyo mafunuo
ya mapenzi yake, na maelezo ya tabia yake, itadumu milele na milele.
Katikati ya mpangilio wa sheria ya Mungu, husimama amri ya
Sabato, ambayo ni amri ya nne. Roho wa Mungu aliwaagizia wanafunzi hao Neno la
Mungu, wakaona kuwa wameipuuzia siku takatifu ya Mungu kwa ujinga wao. Wakaanza
kuchunguza sababu za kushika Jumapili, ambayo ni siku ya kwanza ya juma.
Hawakuona mahali popote panapoeleza kwamba Sabato ya siku ya saba imefutwa,
wala kubadilishwa. Walikuwa wakitafuta kwa bidii kufanya mapenzi ya Mungu; na
sasa wamegundua kuwa kushika sabato ni mojawapo ya mapenzi yake, kwa hiyo
wakaishika kwa furaha.
Juhudi nyingi zilifanyika ili kutafuta imani ya watu wa
Marejeo. Hakuna mtu aliyekosa kuona kuwa fundisho la patakatifu huko mbinguni
linahusiana na madai ya Mungu ya kushika sheria yake pamoja na Sabato. Hii
ndiyo ilikuwa siri ya upinzani wa maandiko yaliyokuwa yakionyesha huduma ya
Kristo mbinguni, katika patakatifu pa huko. Watu walijitahidi kufunga mlango
uliofunguliwa na Mungu, na kufungua mlango uliofungwa na Mungu. Lakini Kristo
amefungua mlango wa huduma yake katika patakatifu pa patakatifu. Amri ya nne
yaani ya Sabato ilikuwako kati ya sheria za Mungu ikitunzwa huko. Wale
waliouamini ukweli huo unaohusu uombezi wa Kristo wa sheria ya Mungu,
waligundua kuwa huo ndio ukweli wa ufunuo 14, ambao ni ukweli wa maonyo ya
namna tatu utakaowatayarisha wenyeji wa dunia juu ya kurudi kwake Yesu. Lile
tamko kwamba, “Sasa hukumu yake imekuja ni tangazo la ujumbe wa kweli ambao
hauna budi kuhubiriwa mpaka Kristo atakapokoma kuombea watu, naye atakuja kuchukua
watu wake kwake. Hukumu iliyoanza katika mwaka 1844 lazima iendelee mpaka mambo
ya watu wote yaamuliwe, wale waliokufa na walio hai pia. Itaendelea mpaka
mlango wa rehema utakapofungwa kwa binadamu wote.”
Makusudi watu wawe tayari kusimama hukumuni, ujumbe
unawaamuru kwamba, “Mcheni Mungu na kumtukuza” na “Msujudieni yeye aliyefanya
mbingu na nchi na bahari, na chemichemi za maji” Matokeo ya kuukubali ujumbe
huu yamesemwa: “Hapa ndipo penye subira ya watu washikao amri za Mungu na imani
ya Yesu” Ufunuo 14:7-12.
Ili kujitayarisha kwa hukumu, watu ni lazima wazishike amri
za Mungu, ambazo ndiyo kipimo cha tabia katika hukumu. Paulo asema, “Wote
waliokosa wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria … katika siku ile Mungu
atakapozihukumu siri za wanadamu, kwa Kristo Yesu”. “Watendao sheria
watahesabiwa haki” Imani ni muhimu kwa kushika sheria ya Mungu. “Maana pasipo
imani haiwezekani kumpendeza Mungu”. Warumi 2:12-16; Waebrania 11:6; Warumi
14:23.
Ujumbe wa malaika wa kwanza uliwaita watu wamche Mungu na kumtukuza,
na kumsujudia yeye aliye Mwumbaji; wa mbingu na nchi. Kufanya hivyo ni lazima
waitii sheria yake. Bila utii hakuna ibada inayompendeza Mungu. “Huku andiko
kumpendeza Mungu, kwamba tuzishike amri zake” 1 Yoh. 5:3 Mithali 28:9.