AKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU.
💦Kuna mambo kwa akili za
kinadamu yanashindikana, akili ya kibinadamu inafika mwisho.
Pale akili yako
inapofika mwisho hapo ndio mwanzo wa akili za Mungu. "Maana mawazo yangu
si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile
mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko
njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu."ISAYA 55:8_9.
💎Yamkini kuna
hali,majaribu na mapito mbalimbali unapitia sasa,watu wako wa karibu
wamekukatisha tamaa kuwa hilo jaribu/pito/shida yako haiwezekani tena.Labda ni
dokta kutokana na vipimo akakuvunja moyo kuwa hutapona tena,hautazaa tena na
n.k.
Leo nakumbia habari za Mungu mwenye uweza wa mambo yote hakuna
jambo lolote la kumshinda yeye.Ukimwamini sasa atafanya yasiyowezekana katika
macho ya wanadamu kuwezekana na kuwashangaza waliokubeza.
Haikuwa rahisi kwa ajuza Sara kuamini katika umri wa miaka
tisini matiti yake yangenyonyesha mtoto wa kumza.
Lakini tunaona Mungu akimtokea Sara na kumpa mtoto katika umri
mkubwa ambapo wanasayansi akili zao zinagoma katika umri mkubwa vile mwanamke
kuzaa mtoto.
"Ndipo Ibrahim akaanguka kifudifudi akacheka,akasema
moyoni,
Je!Mtu wa umri wa miaka mia,kwake atazaliwa mtoto?Naye Sara
mwenye umri wa miaka tisini atazaa?"MWANZO 17:17,"BWANA akamwambia
Ibrahimu,Mbona Sara amecheka akisema,Mimi kweli nitazaa mwana,nami ni mzee?Kuna
neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?..."MWANZO 18:13_14.
Hakika hakuna la kumshinda Bwana.Hata kama Ibrahimu na Sara
walishajikatia tamaa tunaona kwa majira yaliyokubarika Isaka anazaliwa.
💎Unaona mambo magumu
hayawezekani kwa sababu haujampa Mungu nafasi ya kudhihirisha uweza wake katika
maisha yako.
"Tazama mimibni BWANA,Mungu wa wote wenye mwili;je !Kuna
neno gumu lolote nisiloliweza?YEREMIA 32:27.Mungu anatushanga kuwa hatumtegemei
na kumwamimi kwa 💯🐥%kuwa yeye anaweza.Anza leo kuwamwani Mungu yeye anaweza na
hakuna la kumshinda.
💎Katika mapango na malengo
yako uliyonayo nakusihi usiwaze na hofu kuwa itakuwaje?Ni kweli siku zimeenda
na miezi imesogea labda haujapata kazi,mke,mume n.k. Namutia moyo hata hayo
usipoyaona kwako haina maana kuwa Mungu hawezi tena kukutendea kwa sababu yeye
ni Mungu wa wote wenye mwili hivyo na la kwako analiweza pia."Kwa kuwa
hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu"LUKA 1:37
KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.
SHARE