32/Jinsi ya Kumshinda Shetani
Mashindano makuu baina ya Kristo na Shetani karibu
yatakwisha; kwa hiyo mwovu Shetani anajitahidi sana mara mbili ili kuishinda
kazi ya Kristo anayowafanyia wanadamu., Anakusudia kuwashikilia watu katika giza
la kutoamini mpaka Kristo amalize kazi yake ya kuwapatanisha wanadamu. Hali ya
ubaridi inapotokea kanisani shetani hutulia, maana hayo ndiyo matakwa yake.
Lakini watu wanapoamka na kuuliza swali: “Tufanye nini ili tupate kuokoka?”
Basi huamka na kuingiza hali ya kupotosha, ili kupinga kazi ya Kristo na Roho
Mtakatifu.
Wakati fulani malaika walipohudhuria mbele za Bwana ili
kuabudu, shetani pia alihudhuria, sio kuabudu bali kuendeleza udhalimu wake wa
kupinga haki. Ayubu 1:6. Wakati wakristo wanapokusanyika kwa ibada, naye
huhudhuria ili kuyapotosha mawazo ya wenye kuabudu. Anapoona watumishi wa Mungu
wanaandaa mahubiri, yeye naye huyanakili, ili kuyapotosha kwa ujanja, kabisa
kusudi yasiwafikie watu kama itakwiavyo, hasa kwa wale aliowadanganya. Mtu ambaye
angepaswa kuusikia ujumbe huo, hushughulika na mambo mengine ambayo yatamzuia
asiusikie ujumbe huo.
Shetani huwaona watumishi wa Mungu wakiwa na mzigo kwa ajili
ya giza linalowafunga washiriki. Huwasikia wakiomba Mungu awasaidie katika hali
yao ya ulegevu. Kisha kwa nguvu mpya huwavuta wafuate mambo mengine labda ya
ulafi, au ubinafsi, ili kuwapumbaza wasiweze kupambanua mambo ya lazima
wanayohitaji.
Shetani anajua kuwa wote ambao hawajali maombi na kusoma
Biblia hawawezi kuyashinda mashambulio yake. Kwa hiyo huvumbua kila aina ya
vitu vyenye kuwashughulisha hata wakose nafasi ya kuomba na kusoma. Wasaidizi
wake wako tayari kabisa kuleta upinzani katika mambo ambayo Mungu anawatendea
waadamu. Watawaonyesha watumishi hodari wa Mungu kama watu waliodanganyika na
wadanganyaji. Ni kusudi lao kupotosha kila kusudi jema, na kazi bora, ili kutia
mashaka kwa watu ambao hawana uzoefu na ujuzi mwingi. Hutia kasoro na masuto
kwa kila kazi njema. Lakini watu hao watafahamu baadaye wale wanaomfuata na
kumtumaini. “Mtawatambua kwa matunda yao”. Mathayo 7:16; ufunuo 12:10.