Wakati walipomngojea Bwana katika mwaka 1844, na Bwana
hakuja wale waliomtazamia walikuwa katika wasiwasi na mashaka sana. Wengi
waliendelea kuchunguza Maandiko, ili kuhakikisha msimamo wa imani yao. Unabii
ulikuwa wazi ukionyesha kuwa kurudi kwake Bwana ku karibu. Mibaraka watu waliyopokea
na uongofu wao vilionyesha kuwa ujumbe ulikuwa wa mbingu. Utatanisho wa unabii
ambao walidhani kuwa unawaonyesha kurudi kwa Kristo katika mwaka 1844, lilikuwa
fundisho la kuwafunza kuwa wavumilivu ili kungojea ufunuo zaidi katika mambo
ambayo hawayajui.
Kati ya unabii huu uko wa Habakuki 2:1-4. Hakuna hata mtu
aliyeona kuwa kule kukawia kumo katika unabii. Baada ya uchungu wao na kukata
tamaa kwao fungu hili la Habakuki lilikuwa la muhimu. “Maana njozi hii bado ni
kwa wakati ulioamuriwa. Inafanya haraka kufikilia mwisho wake, wala haitasema
uongo ijapokawia ingojee, kwa kuwa haina budi kuja haitakawia. Mwenye haki
ataishi kwa imani”.
Unabii wa Ezekiel pia uliwafariji waumini. “Bwana Mungu
asema hivi …. Siku hizo ni karibu, na utimizo wa maono yote …. Mimi nitanena na
neno lile nitakalolinena litatimizwa wala halitakawilishwa tena….. nitanena
neno hilo na kulitimiza, asema Bwana Mungu”. Ezekiel 12:23-25, 28.
Wenye kungojea walifurahi. Mungu ajuaye tangu mwanzo mpaka
mwisho ameatumainisha. Kama mafungu ya sehemu kama hizo yasingelikuwako, imani
yao ingetoweka kabisa.
Mfano wa wanawali kumi uliomo katika Mathayo 25 unatoa
kielelezo cha watu wa marejeo pia. Hapa kanisa la mwisho linaelekezwa jinsi
mambo yalivyo. Hali yake inafananishwa na arusi za huko mashariki.
“Ndipo ufalme wa mbinguni unafanana na wanawali kumi,
waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki Bwana arusi. Watano wao walikuwa
wapumbavu, na watano wenye busara. Wale walikuwa wapumbavu walizitwaa taa zao,
wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika
vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia
wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane pakawa na kelele, haya, Bwana arusi,
tokeni mwende kumlaki” Mathayo 25:1-6.
Wote walichukua taa zao ambazo ni mfano wa Biblia. Basi
wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Lakini wakati wale wapumbavu hawakuchukua
mafuta, wenye busara walichukua mafuta pamoja na taa zao. Wenye busara hawa
walijifunza Maandiko Matakatifu ili kujua ukweli ulivyo, kwa hiyo wakawa na
imani ambayo haikuweza kuyumbishwa na hali yo yote. Wengine walikuwa
wakichangamka tu kwa ajili ya ujumbe bila kuwa na imani ya kweli, ila msisimko
tu, wanapokutana na wengine katika mikutano. Hawa walikuwa wakikutazamia kuja
kwa bwana arusi ili wapokee zawadi. Hawakuwa na imani ambayo inasimama imara
katika matatizo na kukawia kwa wakati. Walimtazamia Bwana aje mara moja. Imani
yao haikufaulu.
Kuja kwa Kristo kama kulivyotangazwa na ujumbe wa malaika wa
kwanza, kulifananishwa na kuja kwa bwana arusi. Tangazo la kuja kwake lilienea
pote lilijibika kwa mfano wa wanawali kumi. Katika mfano huu “wote walichukua
taa zao, ambazo ni mfano wa Biblia. Basi wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.
Lakini wakati wale wapumbavu hawakuchukua mafuta, wenye busara walichukua
mafuta pamoja na taa zao.” Wenye busara hawa walijifunza maandiko matakatifu
ili kujua ukweli ulivyo, kwa hiyo wakawa na imani ambavyo haikuweza kuyumbishwa
na hali yoyote, Wengine walikuwa wakichangamka tu kwa ajili ya ujumbe bila kuwa
na imani ya kweli, ila msisimko tu, wanapokutana na wengine katika mikutano.
Hawa walikuwa wakikutazamia kuja kwa bwana arusi ili wapokee zawadi. Hawakuwa
na imani ambayo inasimama imara katika matatizo na kukawia kwa wakati.
Walimtazamia Bwana aje mara moja. Imani yao haikufaulu.
“Hata bwana arusi alipokawia, wote walisinzia na kulala
usingizi.” Kule kukawia kwa bwana arusi kunafananishwa na kukawia kwa wakati,
uchungu wa kutojua, yaani kukawia. Wale waliokuwa na imani ya kweli walikuwa
wamesimamishwa mwambani, ambako hakuna kung'olewa na fujo yoyote. “Wote
walisinzia na kulala” Kundi moja lenye kuacha imani yao, kundi jingine lenye
kungoja kwa uvumilivu nuru ilipowamulikia wazi. Imani ya juu juu haiwezi
kufaidia lolote, wala kutegemea msaada wa ndugu.