Wakati wa matatizo na dhiki ulio mbele yetu unataka imani
halisi, imani yenye kudumu, yenye kustahimili taabu, uchelevu, na njaa, imani
iliyo imara, ijapokuwa inajaribiwa vikali sana, haitafifia. Ushindi wa Yakobo
ni uthibitisho wa nguvu ya maombi. Wote watakaozishika ahadi za Mungu kama
Yakobo alivyofanya watafaulu kama yeye. Kushindana na Mungu ni wachache kiasi
gani wanajua maana yake! Wakati mawimbi ya mashaka na kukata tama yanapomvamia
mtu, ni watu wachache kiasi gani wenye kuzishikilai ahadi za Mungu.
Wale wanaoonyesha imani kidogo wakati huu, wamo katika
hatari kuu ya kutumbukia katika udanyanyifu wa shetani. Hata kama watastahimili
jaribu, hata hivyo watakumbwa na mashaka kwa sababu siyo mazoea yao kumtegemea
Mungu. Lazima sasa tuhakikishe ahadi zake na kuzithibitisha. Kila mara matatizo
huwa makubwa wakati wa kutokea kuliko wakati wa matazamio. Lakini sivyo
itakavyokuwa katika dhiki iliyo mbele yetu. Maelezo yanayoelezwa kuhusu dhiki
hiyo, hata yawe na ufundi namna gani hayatalingana na jambo halisi. Katika muda
huo kila mtu lazima asimame peke yake mbele za Mungu.
Sasa wakati Kuhani wetu mkuu, anapofanya upatanisho kwa
ajili yetu, ingetupasa tuwe wakamilifu katika Kristo. Mwokozi wetu hakujitolea
kwa majaribu ya mwovu hata kwa wazo. Shetani hupata vitu katika mioyo ya
wanadamu ambavyo huvishikilia na kumwezesha awaingilie; huwa na aina fulani za
dhambi ambazo hupendelewa na watu, ambazo humpa nafasi washinde. Lakini Kristo
alisema kumhusu yeye: “Yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu” Yohana
14:30. Shetani hakuweza kupata jambo kwa Yesu Mwanawa Mungu, ambalo kwalo
angeweza kumshinda. Hapakuwa na dhambi yo yote ndani yake ambayo angeingilia
kwake. Hii ndiyo hali ambayo wale watakaosimama wakati wa taabu watakuwa nayo.
Ni katika maisha haya ndiyo inatupasa kujitenga na dhambi
kabisa, kwa imani katika damu ya ukombozi wa Kristo. Mwokozi wetu anatualika
tuungane naye, tuunge udhaifu wetu na nguvu zake, kutostahili kwetu na haki
yake. Anatutegemea sisi kuungana na mbingu ili kurekebisha tabia zetu zifanane
na za Mungu.
Mambo ya ajabu kuhusu tabia ya kishetani zitaonekana
mbinguni, kama alama ya pepo wachafu wafanyao miujiza. Roho za mashetani
zitawaendea “wafalme wa dunia” na ulimwengu wote kuwahimiza waungane na shetani
katika pambano lake la mwisho na serikali ya mbinguni. Watu watainuka
wakijifanya kuwa Kristo mwenyewe. Watafanya miujiza ya kuponya na kudai kuwa
wamepata mafunuo kutoka mbinguni kupingana na Maandiko.