Yesu aliporudi upande wa Magharibi wa ziwa kutoka Gergesa,
aliwakuta makutano yamekusanyika wakimngojea. Alikaa pwani muda kitambo,
akiwafundisha watu na kuponya maradhi yao. Kisha akaenda nyumbani kwa Lawi
Mathayo ili kuhudhuria katika karamu. Hapo Yairo mkuu wa sinagogi alikutana na
Yesu. Akiwa na masikitiko makubwa, alimwambia, “Binti yangu yumo katika hali ya
kufa. Nakuomba uje uweke mkono wako juu yake ili apone; naye aishi.”
Yesu akaondoka mara moja kwenda kwa Yairo. Wanafunzi wake
walistaajabu kwa ukubali wake wa kwenda kwa Rabi huyu, walakini walifuatana na
Mwalimu wao, na kundi la watu pia. Yesu na wanafunzi wake waliendelea pole pole
sana, maana makutano walikuwa wakimsonga pande zote. Baba wa mgonjwa alikuwa na
wasiwasi kwa kusimama mara kwa mara kwa Yesu ili kuwasaidia wenye dhiki, au
kuwafariji wenye mashaka.
Wakati walipokuwa wangali njiani, mjumbe alifika na kutoa
habari kuwa binti wa Yairo amekwisha kufariki. Yesu alisikia hivyo, akasema:
“Usiogope, amini tu, binti yako atapona.”
Basi wakaenda kwa haraka mpaka nyumbani kwa mkuu huyo.
Waombolezaji walikuwako tayari wamgjaza mji na makelel. Yesu alijaribu
kuwayama-zisha, akisema: “Mbona mnafanya ghasia hiVi? Msichana hakufa, ila
amelala.” Walichukizwa kwa maneno ya mgeni huyu. Wamemwona kijana akifa wazi.
Yesu alipotaka waondoke wote, aliwachukua babaye na mamaye, pamoja na Petro,
Yakobo na Yohana, wakaingia pamoja katika chumba alimolala marehemu.
Yesu alikaribia kitanda cha maiti, akaukumbatia mkono wake
kama deaturi yao, akasema: “Msichana, nakauagiza ondoka.”
Akaondoka mara moja kwa kutetemeka, akapita katika watu
wenye kushangaa, macho yake yamekodolewa sawa na mtu atokaye usingizini,
akiangaliwa kwa mshangao mkubwa na watu wote waliokuwa hapo. Wazazi wake
wakamkumbatia kwa furaha isiyosemeka.
Walipokuwa njiani wakienda kwa mkuu huyu, Yesu alikutana na
mwanamke maskini, ambaye alikuwa amesumbuliwa na ugonjwa kwa muda wa miaka kumi
na miwili. Alikuwa ametumia mali yake yote kwa waganga bila kupona. Lakini
aliposikia kuwa kristo yuko, akawa na matumaini. Kama angemfikia tu angepona.
Kwa shida akajikokota pole polae mpaka pwana. Yesu alipokuwa akifundisha watu,
akajaribu kumsogelea, asiweze. Akamfuata katika nyumba ya Lawi Mathayo, lakini
hata huko hakuweza kumfikia kwa asababu ya makutano. Alikuwa katika kukata
tamaa, wakati Yesu aliposogea karibu naye.
Alikuwa karibu na Mganga Mkuu! Lakini kwa ajili ya ghasia
nyingi na fujo kubwa, hakuweza kusema naye, wala kutazamana naye. Akiwa na hofu
na wasiwasi wa kutokubaliana naye na kumweleza hali ya matatizo yake,
alijisogeza kuelekea kwake, huku akijisemea mwenyewa: “Nikimgusa pindo la vazi
lake, nitapona.” Yesu alipokuwa akipita, mwanamke huyu alinyosha mkono wake,
akaweza kugusa upindo wa vazi lake. Katika mguso huo, ndipo alipoweka tumaini
lake lote. Wakati huo huo udhaifu wake na ugonjwa wake ukapona kabisa.
Akajaribu kuondoka katika mkutano huo kwa furaha ya moyo
wake, lakini wakati huo huo Yesu alisimama. Akiangalia huku na huku, aliuliza
kwa sauti ya kusikika: “Nani amenigusa?” Swali hilo lilionekana kuwa ni swali
la kigeni, maana alikuwa akisongwa-songwa na makutano pande zote.
Petro aliyekuwa tayari kusema, alisema: “Bwana makutano
yanakusonga-songa, nawe wauliza: “Nani amenigusa?” Yesu alisema, “Maana naona
nguvu zimenitoka”. Mwokozi aliweza kutambua mguso wa imani, na miguso-guso tu
ya kawaida. Mguso wa imani hauwezi kupita ovyo tu. Angesema mwanamke huyu
maneno ya faraja yataka yodumu mpaka mwisho wa dunia.
Akiwaangalia watu, Yesu aliweza kutambua yule aliyemgusa.
Alipoona kuwa amefahamiwa, mwanamke alijitokeza wazi, akaja akitetemeka,
akaeleza habari za ugonjwa wake, na jinsi alivyopata waokovu kwa Yesu. Ndipo
Yesu akasema. “Binti.... Imani yako imekupnya, nenda zako kwa amani.” Hakumpa
nafasi ya kueleza kwamba kuponywa kwake kumetokana na mambo ya ushirikina ya
kugusa nguo na kupata uwezo wa kupona kimwujiza. Imani kamili ya kutegemea
uwezo wa Mungu ndiyo imemponya.