Yohana Mbatizaji alikuwa mtu wa kwanza kutangaza habari za
ufalme wa Kristo, pia alikuwa mtu wa kwanza kupata mateso. Kutoka mahali peupe
huko jangwani aliletwa gerezani, katika ngome ya Herode, kama mfungwa. Herode
Antipa mwenyewe alisikia mahubiri ya Yohana yakamtetemesha sana. Herode
alimwogopa Yohana, akifahamu kuwa ni mtu mtakatifu, mtu wa haki. Yohana
alikemea kule kuchukuliana na Herodias, mke wa ndugu yake, ambaye ni shemeji
yake. Kwa muda kitambo Herode alitaka kuvunja mawazo hayo ya uasherati, lakini
Herodias alimng’angania kwa nguvu, hata akamshawishi Herode amtupe Yohana
gerezani.
Hali ya gereza ilikuwa mbaya sana, nayo ilimtaabisha sana
Yohana. Muda ulipopita mwingi hali, ya mashaka ikamjia. Wanafunzi wake
walimletea habari za kazi ya Yesu, na jinsi makundi ya watu yanavyomfuata.
Lakini kwa nini mwalimu huyu, akiwa ndiye Masihi, anisaidie katika kufungwa
huku? Mashaka ambayo yasiligalimjia, yakaanza, kumjia. Shetani alifurahi kwa
maneno ya wanafunzi hao ambayo yamemjeruhi roho ya mjumbe wa Mungu. Mara ngapi
rafiki mkuu wa mtu hugeuka kuwa adui yake?
Yohana Mbatizaji alimtazamia Yesu kukitwaa kiti cha utawala
cha Daudi. Wakati ulipopita, wala Yesu hakuonyesha dalili yoyote ya kuwa mfalme
wa dunia hii, Yohana aliingiwa na wasiwasi. Alikuwa ametazamia cheo kikubwa cha
kibinadamu, na uwezo. Masihi angesafisha sakafu kabisa, na kukusanya ngano ghalani.,
na kuyachoma makapi katika moto usiozimika. Soma Isaya 40; Mathayo 3. Sawa kama
Eliya, alitazamia kuja kwa Masihi kutokee kama Mungu atajibu kwa moto.
Yohana Mbatizaji alisimama bila hofu akikemea maovu mahali
pote. Alithubutu hata kumkabili mfalme Herode akimkemea kwa dhambi zake. Na
alingojea Simba wa Yuda aingilie kati na kumwokoa. Lakini Yesu alionekana
akitulia tu, akifanya kazi ya kuponya watu na kufundisha. Alikuwa akila na watu
huku mzigo wa Warumi ulizidi kuwakandamiza watu, ambavyo mfalme Herode na
wenzake waliendelea kufanya wapendavyo, na kilio cha maskini na wenye dhiki
kikipanda mbinguni.