Yesu alifunulia wanafunzi wake maarifa ya watu wake tangu
wakati ambao alipaswa kuchukuliwa kutoka kwao, hata kurudi kwake katika uwezo
na utukufu. Kuingia ndani sana ya wakati ujao, jicho lake likaona zoruba kali
zilipaswa kupiga juu ya wafuasi wake kwa miaka iliyokuwa karibu ya mateso.
Tazama Matayo 24:9,21,22. Wafuasi wa Kristo wanapaswa kupitia kwa njia ya namna
moja ya laumu na mateso ambayo Bwana wao alipitia. Uadui juu ya Mkombozi wa
ulimwengu ulipaswa kuonekana juu ya wote wanaopaswa kuamini jina lake.
Upagani ulifahamu kwamba injili ikishinda, hekalu na
mazabahu zake yalipaswa kuondolewa; kwa sababu hii mioto ya mateso ikawashwa.
Wakristo walinyanganywa mali zao na kufukuzwa nyumbani mwao. Hesabu kubwa ya
wenye cheo na watumwa, watajiri na masikini, wenye elimu na wajinga, waliuawa
bila huruma.
Ya kianzia chini ya utawala wa Nero, mateso yakaendelea kwa
karne nyingi. Wakristo walitangazwa kwa uongo kuwa ni wao walioleta njaa,
tauni, na matetemeko ya inchi. Wachongezi wakasimama tayari, kwa ajili ya faida
tu, kwa kusaliti wasio na kosa kama waasi na tauni kwa jamii. Hesabu kubwa
wakatupwa kwa nyama wa pori ama kuchomwa wahai katika viwanja vya michezo
(amphitheatres). Wengine wakasulubiwa; wengine wakafunikwa na ngozi za nyama wa
pori na kusukumwa kwa nguvu katika uwanja (arena) wa kuchezea ili kupasuliwa
kwa waimbwa. Kwa siku kuu za wote makutano mengi sana yalikusanyika kwa
kufurahisha macho na kusalimia walioumizwa kwa kifo na kuwachekeleya na
kushangilia.
Wafuasi wa Kristo walilazimishwa kutafuta maficho katika
mahali pa ukiwa na pekee. Chini ya milima inje ya muji wa Roma, vyumba virefu
vilifunuliwa katika inchi na miamba kwa maelfu ngambo ya pili ya kuta za mji.
Ndani ya makimbilio haya ya chini ya udongo wafuasi wa Kristo wakazika wafu wao,
na hapo pia walipaswa kukimbilia, walipozaniwa maovu na kugombezwa, walipata
makao. Wengi wakakumbuka maneno ya Bwana wao, kwamba kama wakiteseka kwa ajili
ya Kristo, inafaa wafurahi sana. Zawadi yao itakuwa kubwa mbinguni, kwa maana
ndivyo walivyotesa manabii waliokuwa mbele yao. Tazama Matayo 5:11,12.
Nyimbo za ushindi zikapanda katikati ya ndimi za moto zenye
kutatarika. Kwa imani waliona Kristo na malaika wakiwatazama pamoja na usikizi
mwingi sana na kutazama kusimama imara kwao pamoja na kibali. Sauti ikaja
kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu: “Uwe mwaminifu mpaka kufa, nami nitakupa
taji ya uzima”. Ufunuo 2:10.
Nguvu za Shetani kwa kuharibu kanisa la Kristo kwa mauaji
zilikuwa bure. Watumishi wa Mungu waliuawa, lakini injili iliendelea kutawanyika
na wafuasi wake kuongezeka. Mkristo mmoja akasema: “Tunazidi kuongezeka kwa
hesabu namna munavyozidi kutuuwa, damu ya Wakristo ni mbegu”.
Shetani basi, ili aweze kushinda Mungu alikata shauri ya
kusimamisha mwenge wake ndani ya kanisa la Kristo, ili apate ujanja kile
alichoshindwa kupata kwa nguvu. Mateso yakakoma. Kwa mahali pake kukawekwa
mvuto wa mafanyikio ya kidunia heshima za muda. Waabudu sanamu wakaongozwa
kupokea sehemu ya imani ya kikristo, wakikataa mambo ya ukweli yaliyo ya maana
. Wakatangaza kumkubali Yesu kama Mwana wa Mungu na kuamini kufa na kufufuka
kwake, lakini bila kukubali hali yao ya zambi, na hawakusikia lazima ya
kuungama au badiliko la moyo waweze kuungana katika mafikara ya imani katika
Kristo.
Sasa kanisa lilikuwa katika hofu ya maangamizo. Kifungo,
mateso, moto, na upanga vilikuwa ni mibaraka kwa kulinganisha pamoja na jambo
hili. Baadhi ya Wakristo walisimama imara, kutangaza kwamba haikupasa kufanya
mapatano. Wengine walikubali kugeuza imani yao. Chini ya vazi ya kondoo ya
ukristo unaodaiwa, Shetani alikuwa akijificha yeye mwenyewe ndani ya kanisa,
kwa kuchafua au kuharibu imani yao.
Wakristo wengi mwishowe walikubali kushusha kanuni ya imani
yao. Na umoja ukafanyika kati ya ukristo na upagani. Ingawa waabudu sanamu walijifanya
kuwa washiriki wa makanisa walizidi kujiunga kwa ibada ya sanamu zao, ila tu
wakageuza vyombo vya ibada yao kwa sanamu za Yesu, na hata za Maria na
watakatifu. Mafundisho mabaya, kawaida za kuabudu mambo ya uchawi, na sherehe
za ibada ya sanamu zikaunganishwa katika imani ya kanisa na ibada. Dini ya
Kikristo ikaharibika, na kanisa likapoteza utakatifu (usafi) na uwezo wake.
Wengine lakini, hawakudanganyika. Waliendelea kushika uaminifu wao kwa Muumba
wa ukweli
UJUMBE HUU UMELETWA KWENU NA CHARLES SHIBITA PUNDA WA YESU.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU 0763371047 au pshibita@gmail.com