Milele hata milele Yesu Kristo yuko katika umoja na Baba.
Alikuwa sura ya Mungu, nuru ya upendo wa Mungu, ing’aayo mng’aro wa utukufu
wake. Ili kuufunua upendo na utukufu wa Mungu, alikuja katika ulimwengu wetu wa
giza. Kwa hiyo Ulitabiriwa kwamba, “Nao watamwita jina lake Immanuel, . . .
yaani Mungu pamoja nasi.” Mat. 1:23; Isaya 7:14
.
Yesu alikuwa “Neno la Mungu” Mawazo ya Mungu yalisikika
ndani yake. Ufunuo huu haukutolewa kwa wanadamu waliozaliwa katika dunia tu.
Dunia yetu ndogo ndicho kitabu kidogo cha kusomwa na walimwengu. Waliokombolewa
na wale wa dunia ambazo hazikuanguka watauona msalaba wa Kristo ambao ndio
elimu yao na wimbo wao. Wataona kuwa utukufu ung’aao katika uso wa Yesu ni
utukufu wa kujitoa kwake binafsi kwa upendo. Wataona kuwa kanuni ya mbinguni na
ya duniani ni upendo wa kujitoa nafsi. Upendo huo “usiojitafutia mambo yake”
hutokana na Mungu nao umedhihirishwa kwa njia ya Yesu, ambaye ni mpole na
mnyenyekevu.
Mwanzo Kristo aliuweka msingi wa dunia. Mkono wake uliiweka
dunia katika anga na kuyaweka maua katika nchi. Aliijaza nchi na uzuri, na anga
na wingi wa nyimbo. Zaburi 65:6; 95:5. Juu ya vitu vyote aliandika upendo wa
Baba.
Sasa dhambi imechafua kazi safi ya Mungu, hata hivyo
maandiko hayo ya upendo wa Mungu yanadumu kuwako. Hakuna kitu cha ubinafsi
kilichoko isipokuwa moyo wa binadamu ndiyo umejazwa na ubinafsi. Kila mti na
kichaka na jani hutoa, vitu vya asili vya uhai ambavyo bila hivyo mwanadamu au
mnyama hawezi kuishi, na mwanadamu na mnyama huhudumia miti na vichaka na
majani.
Bahari hupokea maji katika vijito toka nchi, lakini hupata
maji hayo ili kutoa. Mvuke unaopanda kutoka baharini huinyoshea nchi na
kuiburudisha, ili iweze kutoa machipukizi. Malaika walioko kwenye utukufu
furaha yao ni kutoa. Huleta nuru kutoka juu na kuwasaidia wanadamu wapate
kumfuata Kristo.
Lakini tukiacha hayo yote, tunamwona Mungu ndani ya Yesu.
Tunaona kuwa utukufu wa Mungu kutoa. “Siutafuti utukufu wangu wenyewe, ila
utukufu wake aliyenituma” Maneno hayo aliyasema Yesu. Yohana 8:50; 7:18. Kristo
alipokea kutoka kwa Mungu ili apate kutoa. Kwa njia ya Mwana, maisha ya Baba
huwafurikia wote. Kwa njia ya Mwana huduma ya upendo hufurika kwa wote, hivyo
kwa njia ya Kristo mzunguko wa manufaa ya Kristo hukamilika.