Viumbe vya ulimwengu na jinsi Mungu alivyowafunulia wanadamu
mambo ya jayo, vyote huonyesha upendo wake Mungu. Baba yetu aliye mbinguni
ndiye asili ya uhai, hekima, na furaha. Vitazame viumbe vyote jinsi vilivyo
vizuri na vya a jabu. Fikiri jinsi vifaavyo kwa mahitaji na furaha siyo ya wanadamu
tu, bali ya viumbe vyote vilivyo hai. Jua na mvua, vinavyofurenisna na
kuburudisha nchi, pamo ja na vilima, bahari na mabonoo, yote hutuonyesha upendo
wa Muumba wetu. Mungu ndiye anayeviruzuku viumbe vyake vyote mahitaji yao ya
kila siku. Katika naneno nazuri ya Mtunga Zaburi twasoma haya,-
“Macho yao wote yakutazamia wewe;
Nawe huwapa chakula chao majira yake.
Hufunua mkono wako,
Humshibisha kila hai uradhi.”
Zaburi 145:15,16.
Mungu alimwumba mwanadamu katika hali ya furaha na utakatifu
kamili; na wakati ilipotoka mkononi mwa Muumba, nchi ilikuwa nzuri kabisa;
haikuwa na dalili ya uharibifu wala ya laana la Mungu. Taabu na mauti viliingia
kwa ajili ya kuharibu amri za Mungu. Walakini upendo wake Mungu huonyeshwa hata
kwa maumivu yaliyokuja kwa ajili ya dhambi. Imeandikwa kwamba Mungu aliilaani
ardhi kwa ajili ya mwanadamu. Mwanzo 3:17. Miti yenye miiba na magugu - yaani
shida na majaribu yanayompata mwanadamu katika uzima wake - yaliwekwa kuwa
msaada wake, kuwa ni namna mo jawapo ya mafundisho yake yanayotakiwa katika
mpango wa Mungu juu ya mwanadamu, apate kumtoa katika hali mbaya ya dhambi na
kumrudisha katika hali njema jinsi alivyokuwa mara ya kwanza.
Ingawa dunia imeanguka katika hali mbaya kwa ajili ya
dhambi, lakini yote yaliyomo si huzuni na mashaka tupu. Viumbe vimekuwa kama
mitume wa Mungu kutuletea maneno ya kututia faraja na kututuliza roho zetu.
Kila mti wa miiba una maua yake; yaani, katika kila shida twaweza kupata baraka
za Mungu.
“Mungu ni upendo” imeandikwa kila mahali. Ndege waimbao
vizuri, kila aina ya maua na miti,yote hutushuhudia upendo na uangalifu wa
Mungu, jinsi atakavyo kuwafurahisha watoto wake.
Neno la Mungu huonyesha tabia zake. Yeye mwenyewe ametangaza
upendo na huruma vyake visivyo na kiasi. Musa alipoomba, “Nionyeshe basi
utukufu wako,” Bwana alimjibu akanena, “Nitapitisha mimi wema wangu wote mbele
yako.” Huu ndio utukufu wake. Bwana alipita mbele ya Musa, akatamka, “Bwana,
Bwana Mungu, mwenye rehema na neema, si mpesi kwa hasira, na mwingi wa huruma
na kweli; awawekeaye elfu huruma, mvenye kusamehe uovu, na kosa, na dhambi.”
Kutoka 33:18,19; 34:6,7. Naye “mvumilivu, na mwenye wema mwingi,” “kwa sababu
apendezwa na huruma huyu.” Yona 4:2; Mika 7:18.
Mungu amejifungia mioyo yetu kwake kwa namna nyingi zinazotuonyesha
upendo wake; katika viumbe vya ulimwengu, na kwa upendano ulio wema wa
wanadamu, Mungu ame jaribu kutuonyesha wema wake. Lakini hayo yote hayawezi
kutudhihirishia barabara upendo wake jinsi ulivyo, kwa kuwa adui, yaani
Shetani, amepofusha macho ya kiroho ya wanadamu ili wawe na hofu ya Mungu; nao
humwona Mungu kama ni mkali asiye na huruma. Shetani aliwapoteza wanadamu ili
wamdhanie Mungu kuwa ni mkali kabisa - kama jaji aliye na roho ngumu asiyeweza
kumwachia mtu. Aliwatilia wanadamu fikara kama Muumba wetu huwachunguachungua
watu ili apate kujua makosa yao na kuwalipa kisasi. Bwana Yesu alikuja hapa
duniani na kuishi kati ya wanadamu kwa kusudi kuziondolea mbali fikara mbaya
hizo, na kutuoryesLa upendo wa Mungu jinsi ulivyo.
Mwana wa Mungu alitoka mbinguni ili awaonyeshe wanadamu Baba
aliye mbinguni. “Hakuna mtu allyemwona Mungu wakati wo wote; Mwana wa pekee
aliye katika kifua aha Baba, huyu ndiye aliyefasiri habari yake.” “Wala hakuna
mtu amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.”
Yoh.l:18; Matt.11:27. Mmo ja wa wanafunzi wake alipomwambia,“Tuonyeshe Baba,”
Yesu alimjibu,“Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukuni jua, Filipo ?
Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba ?” Yoh.l4:8,9.
Yesu alipoeleza namna ya kazi yake aliyokuja kuifanya hapa
duniani, alisema hivi,-
“Roho ya Bwana ni juu yangu,
Kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.
Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo,
Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa,
na vipofu kupata kuona tena,
Kuwaacha wa huru waliosetwa.”
Luka 4:18.
Hiyo ndiyo kazi yake. “Naye akatembea huko na huko, akitenda
kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani.” Mat.10:38. Katika matendo
yake yote alionyesha upendo, rehema na huruma. Alikuwa katika hali ya
kibinadamu ili apate kujua mahitaji ya wanadamu. Hakuna hata maskini kabisa
aliyeogopa kumfikilia karibu. Watoto pia wakavutwa kwake.
Yesu hakuficha hata neno lo lote la kweli, lakini aliyasema
yote katika moyo wa upendo. Alitumia busara sana na uangalifu na huruma katika
maongezi yake na watu. Hakuwafanyia watu jeuri kamwe, hakusema maneno yo yote
makali yasipohusu, hakuwahuzunisha watu kupita kiasi. Hakuulaumu udhaifu wa
kibinadamu. Alisema kweli tupu, lakini alisema yote katika moyo wa upendo.
Alichukia sana na hali ya unafiki, na kutokuamini, na uovu; lakini kila
aliposema maneno ya lawama na mashtaka, aliyasema kwa masikitiko makubwa.
Aliulilia Yerusalemi, mji alioupenda, ambao ulikataa kumpokea yeye aliye Njia
Kweli, na Uzima. Walimkana yeye aliye Mwokozi, lakini hata hivyo ‘ akazidi
kuwahurumia. Maisha yake yalikuwa ya kujinyima mwenywe na kuwafikiria wengine.
Kila mtu alikuwa na thamani kubwa machoni pake. Ingawa alikuwa Mwana wa Mungu,
hakumdharau mwanadamu ye yote; bali aliwaona wote kuwa ni wenye dhambi ambao
alikuja kuwaokoa.
Hizo ndizo tabia zake Kristo kama zilivyofunuliwa katika
maisha yake. Tena hizi ndizo tabia za Mungu mwenyewe pia. Yesu, Mwokozi aliye
mwema, mwenye huruma, ndiye Mungu hasa aliyedhihirishwa katika mwili wa
kibinadamu. 1 Tim.3:16.
Yesu aliishi, akateswa, akafa ili atukomboe. Akawa “mtu wa
huzuni,” ili tuwe washirikia pamoja naye katika furaha ya milele. Naye Mwana
Mpendwa wa Mungu, aliye jaa noema na kweli, Mungu alimwacha atoke katika mahali
pa utukufu na kutika hapa duniani palipoharibika kwa ajili ya dhambi, penye
giza la mauti na laana. Alimkubali atoke mahali anapopendwa na Babaye na
kusifiwa na malaika, a je kuaibika, kudhiliwa, kuchukizwa, na kuuawe., “Adhabu
ya amani yetu juu yako.” Isa.53:5. Mwangalie jinsi alivyo jangwani, katika
bustani ya Gethsemane, tena juu ya msalaba, Mwona Mtakatifu wa Mungu akachukua
mwenyewe uzito wa dhambi ya wanadamu. Yeye aliyekuwa na uno ja kwa Mungu,
akaona mwenyewe moyoni mwake ubaya wa hali ya kutengane na Mungu, ndiyo hali ya
wanadamu kwa ajili ya dhambi, kwa ajill ya matengano hayo akaona uchungu moyoni
naye akalia, “Mungu Wungu, Mungu wangu, mbona umeniacha ?” Matt.27:46. Uzito wa
dhambi, jinsi ulivyo mbaya kupita kiasi, na jinsi unavyoleta kutengana na Mungu
- huu ndio uliouvunja moyo wa Mwana wa Mungu.
Lakini Yesu hakujitoa kuwa dhabihu kubwa hivi maksudi
kumtilia Baba yake moyo wa kuwapenda wanadamu na kuwaokoa. Sivyo! “Kwa maana
jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hate akampeleka Mwana wake wa pekee, ili
mtu aliye yote amwaminiye asepotee, bali apate uzima wa milele.” Yoh.3:16.
Tangu zamani Baba yetu aliye mbinguni ametupenda, si kwa ajili ya mapatanisho
aliyoyafanya Yesu, ila kwa kuwa Mungu mwenyewe alitupenda naye akamkubali Yesu
afanye mapatanisho hayo. Kristo ndiye njia ambayo kwayo Mungu hutuonyesha
upendo wake kwetu. “Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha
ulimwengu na nafsi yake.” 2 Wakor.5:19. Mungu alipata maumivu pamoja na
Mwanawe. Huko Gethsemane, na kwa kufa kwake Kalwari, Mungu alijitoa kwa ajili
ya wokovu wetu.
Yesu alisema, “Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka
uzima wangu ili niutwae tena,” Yeh-10 17. Yaani, ni kama Yesu angesema hivi;
“Baba yangu amewapendeni sana hata anazidi kunipenda mimi kwa sababu ya kujitoa
maisha yangu kwa ajili yenu. Mimi. nikawa ninajitoa badala yenu tena kuwa kama
dhamana yenu. na kwa jinsi nilivyoehukua makosa yenu na adhabu ambayo
miliwapasiwa ninyi, kwa hayo Baba yangu huzidi kunipenda mimi; kwa sababu yu
Dhabihu yangu, Mungu aweza kuwa mwenye haki tena kumhesabia haki yule
amsadikiye Yesu.”
Hapana awezaye kutuokoa, ila Mwana wa Mungu tu; kwa kuwa
yeye pekee aliyekuwa pamoja na Baba ndiye awezaye kumsifu na kueleza tabia
zake. Yeye tu aliyeujua upendo wa Mungu ndiye awezaye kuudhihirisha upendo ule
barabara. Hakuna njia nyingine ya kutuonyesha jinsi Mungu anavyowapenda
wanadamu waliopotea, ila kwa njia hii mo ja tu, yaani ya Kristo alivyojitoa na
kufa badala yao.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akampeleka Mwana wake wa pekee.” Yoh.3:15. Mungu alimtoa Mwanawe aishi kati ya
wanadamu ili azichukue dhambi zao, apate kuadhibiwa badala yao, na kuwatolea
maisha yake kama dhabihu; pia Mungu akamtoa awe katika hali moja na wanadamu
ambao wamepotoa, na kushirikiana nao katika mambo ya maisha yao na ha ja zao
zote. Yeye aliyekuwa mmo ja na Mungu ame jiunga na wanadamu kwa namna isiyoweza
kuvunjwa. Yesu “haoni haya kuwaita ndugu zake;” (Waeb.2:ll); yeye ndiye Dhabihu
yetu, Mwombeaji wetu mbele ya Mungu, Ndugu yetu aliye katika mfano wa
kibinadamu na kushirikiana nao hao ambao ameku ja kuwaokoa - Yeye ndiye Mwana
wa mwanadamu. Alifanya hayo yote ili awakomboe wanadamu katika dhambi na hali
yake mbaya, naye mwanadamu apate kujua upendo wake Mungu na kushirikiana naye
katika hali ya furaha na usafi.
Tukifahamu kima cha wokovu wetu, jinsi Mwana wa Mungu
alivyokufa kwa ajili yetu, imetulazimu kutambua jinsi tunavyoweza kuwa watu
walio bora katika Kristo. Mtume Yohana alipofahamu upendo wa Mungu jinsi ulivyo
mkubwa mno, aliona hana budi kumcha Mungu na kumsujudu moyoni mwake. Upendo
huo, jinsi ulivyo wa huruma na rehema, ni upendo mkubwa usioweza kusemeka; naye
Yohana alisema, “Fahamuni, ni pendo la namna gani alilotupa Bwana, kuitwa wana
wa Mungu.” 1 Yoh.3:l. Mungu amewaona wanadamu kuwa ni wenye themani kubwa wa
namna gani; Kwa kuanguka katika kufanya dhambi, wanadamu wakawa chini ya
mamlaka ya Shetani. Lakini kwa kumwamini Kristo na kutolewa kwake, wawoza kuwa
wana wa Mungu. Kristo alikuwa katika hali ya kibinadamu ili apate kuwasaidia
wanadamu. Nao wenye dhambi wakiwa wanashirikiana naye Kristo, watageuzwa hali
yao, na kustahili kuitwa “wana wa Mungu.
”
Upendo wa ajabu huo, hauwezi kulinganishwa na kitu cho
chote! Wana wa Mfalme aliye mbinguni! Ahadi ya kupendwa sana! Jambo la maana
sana lifaalo kufikiriwa! Upendo usio na kifani, jinsi Mungu alivyoupenda
ulimwengu usiompenda! Fikara hiyo huutiisha moyo na kuutuliza ili ufungwe kwake
Mungu na kufanye mapenzi yake. Na jinsi tunavyozidi kuzichungua tabia za Mungu,
na kufahamu jinsi alivyotufanyia kwa kufa kwake Kristo msalabani, ndivyo
tunavyozidi kuona kama Mungu ndiye mwenye rehema na huruma, na ndiye awezaye
kuwasamaha wenye makosa, naye ni mwenye haki, naye huwapenda wanadamu kwa
upendo mkubwa upitao kiasi cha upendo wa mama kwa watoto wake.