“Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye
upande wa wana wa watu wako: na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake
haukuwapo tangu lilipoanzaa kuwapo taifa hata wakati huo huo, na wakati huo
watu wako wataokolewa: kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu
kile”. Daniel 12:1.
Wakati ujumbe wa malaika wa tatu ufungwapo, watu wa Mungu
watakuwa wamekamilisha kazi yao, Watakuwa wamepokea mvua ya masika, nao sasa
wako tayari kukabiliana na saa ya kujaribiwa inayowajia, Ujumbe wa mwisho wa
kukata shauri umekwisha kutolewa ulimwenguni, na wote waliojithubutisha kuwa
waaminifu kwa Mungu wametiwa “mhuri wa Mungu”. Ndipo Yesu anapokomesha kazi
yake kama mwombezi wa wanadamu huko mbinguni. Hapo atasema kwa sauti kuu,
“imekwisha” “mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; mwenye uchafu na azidi kuwa
mchafu; mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa”.
Ufunuo 22:11. Kristo amekwisha kufanya ukombozi kwa watu wake, na amefuta
dhambi zao. “Na ufalme na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu” (Daniel
7:27) karibu kutolewa kwa warithi wa wokovu, na Yesu atatawala kama mfalme wa
wafalme, na Bwana wa mabwana.
Atakapotoka patakatifu, giza kuu litawafunika watu dunaini.
Wenye haki hawana budi waishi machoni pa Mungu mtakatifu bila kuwa na mwombezi.
Kile kinachowalinda waovu kimeondolewa, na shetani anachukua utawala kamili
bila kizuizi kwa watu ambao hawakutubu. Roho wa Mungu ameondolewa dunaini.
Shetani atawatumbukiza wenyeji wa ulimwengu katika taabu kuu ya mwisho. Malaika
wa Mungu waliokuwa wakizuia pepo kuu, sasa wanaziachia pepo hizo ni fujo ya ajabu
na mauaji yasiyosemwa. Ulimwengu mzima utahusikia katika kuangamizana bila
huruma, zaidi ya maangamizo yaliyouangukia Yerusalemu wa zamani. Mpaka sasa
majeshi yako tayari, yanangoja tu ruhusa ya Mungu ili yaanze kazi ya kuangamizi
kila kona.
Wenye kushika sheria ya Mungu watahesabika kama ndio wenye
kusababisha maafa hayo, yaliyojaa ulimwenguni. Nguvu na uwezo uliofanya kazi ya
kumaliza Injili iliwachukiza waovu, na shetani atachochea roho ya chuki isiyo
na kifani, ili kuwaandama wale waliopokea ujumbe na kujiunga na kundi la Mungu.
Wakati Mungu alipowaacha Wayahudi wao pamoja na makuhani wao
walikuwa bado wakijihesabu kuwa ni wapendwa wa Mungu. Huduma za kanisani
zilikuwa zinaendeshwa kama kawaida, kila siku waliomba baraka kwa Mungu, kama
watu wataua, na hali wamejaa uharibifu, wakiwa na hatia ya damu ya Mwana wa
Mungu. Hali kadhalika, mstari wa ulimwengu utakapokuwa umepigwa, na kesi yake
imeshakatwa milele, wenyeji wa ulimwengu hawatatambua hata kidogo. Aina za
ibada ambazo hazina misingi zitakuwa zinaendeshwa kimitindo, na watu ambao
Mungu hayumo kati yao. Shetani ndiye atakuwa akiwaongoza ili kukamilisha kusudi
lake la udanganyifu.
NDUGU ZANGU KAENI CHONJO ULIMWENGU MDA SI MREFU UTAANGAMIA.