MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

UTAMBUE UKWELI JUU YA MGOGORO ULIYOPO KATI YA ISRAEL NA PALESTINA.


1.   . Je, ni kweli kwamba taifa la Israel ni taifa mkakati lililoanzishwa ili kukabiliana na nguvu ya Urusi huko mashariki ya kati ?

-Jibu ni Hapana, kwasababu Taifa la Israel liliundwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948, ambapo kura zilipigwa tarehe 29 November 1947. Urusi ya Kisovyeti , Marekani na Uingereza ndiyo waliyopiga sana debe Taifa hilo liundwe.

- Kipindi hicho Wayahudi walikuwa wanaonewa huruma na mataifa karibia yote duniani kwasababu ya Mauji yao ya Halaiki yaliyofanywa na Wanazai huko Auschwitz nchini Polandi. Kulikuwa na uvumi kwamba ili jambo kama hilo lisiwakute tena Wayahudi ni lazima watafutiwe nchi yao ya kuishi.

- Upande wa pili ni lazima Ukumbuke kwamba Wayahudi ndiyo waliongoza Mapinduzi ya Kikomunisti nchini Urusi mwaka 1917 na walikuwa mstari wa mbele kwenye kupigana Vita ya pili ya dunia dhidi ya genge la Mafashisti hivyo ushawishi wao huo ulifanya Warusi na Wamarekani wakubali kirahisi kutengeneza hilo taifa.

-Mwisho kabisa, dhana ya kurudi nchini Israeli ilizaliwa tangu zamani hata kabla ya kuwepo Marekani na Urusi. Kubwa zaidi Wazayuni kama wakina Theodore Hertz ndiyo waliyoipigia sana chapuo mnamo miaka ya 1800's.

NB: Japo siku zilivyoenda mbele Mataifa makubwa yalitumia hili suala kama njia ya kueneza ushawishi wao katika eneo la Mashariki ya Kati. Kila taifa kubwa lilitegemea Israeli atakuwa upande wake, hivyo vita baridi ilivyoanza Marekani alitumia Israeli kama mlango wake wa kuzuia maslahi ya Urusi pale Mashariki ya kati. Huu mkakati uliitwa CONTAINMENT POLICY na ulisukwa na Raisi Harry S Truman. Mfano Mzuri tu hata Ujerumani iligawanywa kuwa mataifa mawili adui kwasababu tu hawa wakubwa walivutana. Hili lilienda kuanzia:

o    India (Upande wa Urusi) Vs Pakistani (Upande wa Marekani)
o    Korea Kaskazini (Upande wa Urusi) Vs Korea Kusini (Upande wa Marekani)
o    Vietnam Kaskazini (Upande wa Urusi) Vs Vietnman Kusini (Upande wa Marekani)
o    China (Upande wa Urusi) Vs Taiwan (Upande wa Marekani)
Hivyo hata pale Mashariki ya Kati ilikuwa vivyo hivyo: Ukweli ni kwamba mpango huu ulikuwepo tangu muda lakini mataifa makubwa yalikuwa na Maslahi yake binafsi (wote walitaka kutawala vyanzo vya mafuta) hivyo kila mtu alitegemea Israeli atakuwa swahiba wake.

2. Je, ni kweli kuwa kabla ya kulianziasha taifa hilo huko mashariki ya kati, kuna wakati walifikiria kulianzisha katika nchi ya Uganda? Je ilikuwaje?


-
Ndiyo, Wayahudi baada ya kuona kuwa wanateswa sana huko Ulaya walimuomba swahiba wao Uingereza awatafutie nchi ya kukaa. Wazayuni walitaka Kurudi Palestina lakini ikashindikana kwasababu Mashariki ya Kati ilikuwa chini ya Dola la Kiislamu la Uturuki tokea Karne ya 15 hadi Karne ya 20 baada ya kuisha Vita ya Kwanza ya dunia mwaka 1919. Muingereza aliona ni vyema Wayahudi wapelekwe kwenye baadhi ya maeneo ya makoloni ya Uingereza kama Uganda. Wajerumani walifikiria kuwapeleka Madagascar. Hebu pitia hapa:Naomba kujua historia ya Urusi

3. Nini tofauti kati ya Wazayuni (Zionists) na Wayahudi (Jews)?

- Tofauti ni kubwa sana, Uzayuni ni mfumo wa Kisiasa na Uyahudi ni mfumo wa Kidini na Kitamaduni.
Uzayuni ni Mfumo ulioanzishwa na Myahudi anayeitwa Theodore Hertz mnamo miaka ya 1800's ambao unasema ni lazima Wayahudi warudi Sayuni (Mji wa baba yao Daudi). Huku Uyahudi ni dini yenye mizizi ya Kiebrania inayotaka mtu amuabudu MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo tu. (Hata wewe unaweza kuwa Myahudi ukitaka, Mfano. Watoto wa Trump wote wanaabudu dini ya Kiyahudi)


-
Professor John Mearshimer kwenye Essay yake inayoitwa "The Israel Lobby" anasema siku hizi mtu yoyote anaweza kuwa Mzayuni (Zionist). Akasema mtu yeyote anayekubaliana na Siasa na sera za nchi ya Israeli ni Mzayuni. Mfano Mzuri ni wale Walokole wa Marekani pamoja na Neo-Cons wote ni Wazayuni. Unaweza kupitia hapa kuipata:http://mearsheimer.uchicago.edu/pdfs/IsraelLobby.pdf

4. Nini kilitokea hata kupelekea mauaji ya wayahudi/waisrael kule German? Kuna habari kuwa Rothschild family ambao originally ni jews ndo walikuwa nyuma ya yale mauaji na pamoja na kwamba wao ni jews wenyewe pamoja na miradi yao hawakuathirika na udikteta wa Hitler, na kuna tetesi kuwa hata Hitler a.k.a Alois alitoka katika familia hiyo. Je ni kweli?

-Mauaji ya Wayahudi yana Historia ndefu kidogo, lakini kwa sababu hasa iliyopelekea Wayahudi kuuwawa kwa kiasi kikubwa ni Vita ya Kwanza ya dunia na Ukomunisti wa Urusi. Ikumbukwe Wayahudi wengi walikuwa wakiishi Ujerumani, Ufaransa, Poland, Yukreini na Urusi. Wakati vita ya kwanza ya dunia inaendelea vugu-vugu la Uzayuni lilikuwa limepamba moto. Wazayuni walimshauri Waziri mkuu wa Uingereza kwamba atoe tamko linalosema endapo Wayahudi watajiunga na Triple Entente (Uingereza, Ufaransa,Urusi na Marekani ) dhidi ya Triple Alliance (Ujerumani, Italia , Austria, Ottoman Empire, Bulgaria) basi Uingereza wangewapa Wazayuni nchi yao kule Mashariki ya kati. Tamko hilo lilitwa The Balfour Declaration. Pitia hapa kulisoma:Text of the Balfour Declaration


-
Bahati mbaya Wayahudi wengi walikuwa jeshini Ujerumani na hivyo walisaidia kuvujisha siri nyingi za kijeshi za Ujerumani. Kwa upande wa pili Wazayuni Walisaidia Uingereza na Ufaransa kusaini mkataba wa siri uitwao Sykes-Picot Agreement wa mwaka 1916 ambao ulisema kwamba baada ya vita ni lazima watagawana Ufalme wa Uturuki (The Ottoman Empire) hivyo maeneo mengi ya Mashariki ya kati yangekuwa huru hivyo Waarabu na Wayahudi wangepata nchi yao. Huu mkataba ulipewa Baraka zote na Wazayuni matajiri mfano Familia ya Rothschild. Huu mkataba ulivujishwa na Wakomunisti na ukaonyesha na ukadhihirishia dunia kwamba Wayahudi wanafadhili mbinu chafu ili kuhujumu mataifa makubwa. Pitia hapa uusome huo mkataba: Sykes-Picot Agreement | 1916

- Upande mwengine Vita ya Kwanza imeisha Wajerumani na mataifa mengine wakawalaumu sana Wayahudi kwamba wao ni Wasaliti. Kibaya zaidi Ukomunisti uliingia hadi Ujerumani na Ujerumani ikawa masikini sana. Ikumbukwe waliokuwa wanaeneza Ukomunisti wa Urusi walikuwa ni Wayahudi kama Vladmir Illych Ulyanov Lenin, Leon Trotsky, Felix Dzerzhinsky n.k. Baada ya wakina Lenin kumuua Mfalme Alexander Ramanov wa Pili wa Urusi pamoja na familia yake yote dunia ikazidi kuwachukia Wayahudi. Hii ni moja ya sababu Hitler alivamia Urusi kwa nguvu sana.

-Hilo la Adolf Hitler kuwa mjukuu wa Rothschild halina ushahidi wowote wa kitaaluma hivyo naomba tusilizungumzie kabisa.


5. Hawa wayahudi/israel walitokea wapi mpaka wakatapakaa katika nchi za ulaya na Marekani?

-Hii hoja ya Wayahudi kuwepo Ulaya inapingwa sana na wengi lakini nadhani kuna sehemu kubwa sana ya Historia tunaisahau kabisa. Wengine wanasema kule kuna umbali sana, hivyo Wayahudi wasingeweza kukimbilia Ulaya. Lakini ni lazima tukumbuke kwamba Israeli ilikuwa ni koloni la dola la Mrumi kwa zaidi ya Miaka 500. Hivyo wazungu walikuwepo sana pale,hata Pilato aliyemuhuku Bwana Yesu alikuwa ni Mzungu. Mtume Paulo alishawahi kwenda kuhukumiwa mbele ya Kaisari huko Rumi, sehemu yenye umbali mkubwa kabisa na Yerusalemu.

-Hivyo kama Ulaya,Afrika na Asia ilikuwa ni nchi moja chini ya Rumi kwanini Wayahudi wasiweze kusafiri kwenda Ulaya? Ukisoma hata kwenye Biblia utaona jinsi mitume Wayahudi wengi walivyoenda kuishi Uyunani(Ugiriki), Misri (Bwana Yesu na familia yake walifika hadi Misri) na Rumi. Hivyo walianza kwenda Ulaya wakati wa nyuma kidogo.

-Upande wa Pili baada ya dola la Rumi kuanguka Waislamu walitawala Mashariki ya kati yote ile: Lakini kuanzia karne ya kumi na moja hadi kumi na mbili kulikuwa na Vita za kidini Al-Maaruf kama Crusades ambazo Kanisa la Katoliki chini ya Baba Mtakatifu Urban wa Pili walizianzisha. Walisema wanataka kuwaondoa Waislamu kwenye eneo lao Mji Mtakatifu (The Holy Land). Hivyo wazungu wengi walitoka Ulaya akiwemo Mfalme wa Uingereza Richard The Lion Heart. Kipindi hiki Sultani wa Mashariki ya Kati na Afrika aliitwa Salahadeen ambaye aliwashinda Wayahudi na kuitwaa Yerusalemu hivyo Wayahudi wengi waliondoka na wale wapiganaji wa mataifa ya Ulaya.

- Kuhusu Wayahudi kuwepo Marekani ni swali lisilokuwa na mashiko sana kwasababu Marekani ni nchi ya Wageni. Imejengwa na watu wenye Asili ya Ufaransa, Italia, Irishi, Uingereza, Uhispania n.k. Kwanza kabisa ni lazima Ujue Wayahudi wengi waliishi Uingereza na Marekani lilikuwa koloni la Muingereza, hivyo kama walivyofanya Wazungu Wayahudi nao walienda kutafuta maisha nchini Marekani wakati bado ni koloni. Ikumbukwe Uingereza ilishawahi kuwa na Waziri mkuu Muisraeli aliyeitwa Benjamin Disraeli hivyo walikuwepo sana Uingereza hata kabla ya Marekani kupata Uhuru. Pili Wayahudi wengi walikimbilia Marekani baada ya Uhuru kwasababu The New World was the Land of Opportunity tofauti na Ulaya kwenye manyanyaso. Walienda kwa Awamu tatu,hebu soma hapa:
Jewish Immigration to America: Three Waves | My Jewish Learning

NB: Sababu ni nyingi sana lakini naomba niishie hapa na nikuachie maswali ya kufikiria:
o    Wangoni kwao ni Afrika Kusini lakini walifikaje hapa Tanzania?
o    Watutsi kwao ni Ethiopia lakini walifikaje pale Rwanda?
o    Kabila la Wairaki wanatokea huko Mashariki ya kati lakini walifikaje pale Manyara?
o    Marekani yote ni Bara la Wahindi Wekundu lakini Mbona inakaliwa na Wazungu?
o    Misri ya zamani ilikaliwa na Weusi lakini mbona leo Waarabu wamejaa?

6. Kuna uhusiano gani wa siri kati ya israel na marekani? Je kuna/iliwahi kutokea influence yoyote ya Israel ndani ya Russia?

- Hilo la Marekani nimeshakujibu tayari: Ila hili la Urusi nasema NDIYO KUBWA kabisa.
Ushawishi wa Wayahudi ni mkubwa sana huko Urusi na Ushahidi wa hili uko wazi kabisa. Kumbuka sera ya Ukomunisti ni sera ya Myahudi Karl Marx na ilipigiwa chapeo na Wabolsheviki wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 1917.

- Niseme tu haya yafuatayo:
1. Baba wa taifa la Urusi ya Kisovyeti alikuwa ni Myahudi Vladmir Illych Ulyanov Lenin.
2. Muasisi wa jeshi la Urusi na mifumo yake mle ndani alikuwa ni Myahudi Leon Trotsky.
3. Muasisi wa K.G.B (Shirika la kipelelezi) kipindi hicho ni The Cheka alikuwa Myahudi Felix Dzerzhinsky.
4. Mzee Yevgeny Primakov alikuwa Waziri Mkuu kipindi cha Boris Yeltsin.
5. Waziri wa Ulinzi wa Israeli Bwana Avigdor Lieberman alizaliwa Urusi baba yake akiwa mwanajeshi kule.

Orodha ni ndefu sana lakini hata Waziri Mkuu wa Uingereza Bwana Winston Churchill alishawahi kusema yafuatayo kuhusu Wayahudi, Ukomunisti na Urusi. Pitia hapa umsome:
Some people like them, some don't

Subscribe to receive free email updates: