Mafundisho
yahusuyo kutokufa kwa roho kwanza yalitokana na imani ya wapagani, na wakati wa
giza la kiroho mafundisho haya yaliingizwa katika imani ya kikristo na
kuhesabika kuwa ni mojapo ya ukweli, na yakashika mahali pa Maandiko yasemayo
kuwa, “wafu hawajui neno lo lote” Mhubiri 9:5. “Watu wengi huamini kuwa roho za
wafu ndizo zile, zisemwazo kuwahudumu wale watakaourithi wokovu” Waebrania
1:14.
Imani
ya kuwako roho za wafu kuja kuwahudumia watu wanaoishi, imeandaa njia ya
kuingizia mambo ya kisasa ya kuongea na wafu. Kama watu wanaoufahamu unaozidi
ule waliokuwa nao wakati walipoishi, mbona hawaji tu kiwazi na kuwaelimisha
watu? Ikiwa roho za wafu huwazungukia jamaa zao walioko duniani, mbona hawakai
na kuongea nao? Mbona wanaoamini kuwa mtu akifa huwa anajua mambo, hukataa nuru
ya Mungu inayoeleza mambo ya roho? Hapa ndipo Shetani hufanyia kazi yake.
Malaika waovu huonekana kama wajumbe katika ulimwengu wa roho.
Mkuu
wa uovu yaani shetani anao uwezo wa kuleta sura za watu waliokufa ambao ni
jamaa. Maigizo ya watu hao ni kamili kabisa. Huonekana kama wao halisi. Watu
wengi hufarijika kuwa ndugu na rafiki zao wako wanaishi huko mbinguni. Bila
kujihadhari na hatari yo yote, hutega masikio kwa “roho zidanganyazo, na
mafundisho ya mashetani” 1 Tim. 4:1.
Waliokufa
bila kujitayarisha, yaani bila kujitoa kwa Kristo, hudai kuwa wako katika
furaha kuu huko mbinguni. Watu hawa bandia wanaojidai kuwa wanakaa rahani
mbingu, mara nyingine husema maneno ambayo huwa ya kweli. Wakishakuaminiwa,
hutoa mafundisho yaliyo kinyume cha Biblia. Kwa kuwa mara nyingine husema
maneno ya kweli na kutabiri mambo fulani ambayo hutokea kuwa kweli, hivyo
mafundisho yao ya uongo hukubaliwa kama mafundisho ya kweli ya Biblia. Sheria
ya Mungu imewekwa kando, na Roho wa neema amedharauliwa. Hiyo ndiyo mizimu, na
roho za mashetani. Roho hizi hukataa Uungu wa Kristo na kumhesabu Mwumbaji kuwa
na hali sawa na yao.
Wakati
matokeo ya udanganyifu huo hukubaliwa kama ukweli, hutokea ishara ambazo ni
kazi za yule mwovu huwadangaya watu wakaziamini kama ishara za Mungu. Watu
wengi huamini kuwa hali ya kuongea na wafu. Au mizimu ni ujinga wa kibinadamu.
Wanapokabiliwa na maonyesho ya wazi ambayo hawawezi kuyakanusha, hukubali kuwa
hayo kutoka kwa Mungu.
Kwa
msaada wa shetani wachawi wa Farao waliigiza kazi ya Mungu na kufanya miujiza.
Soma Kutoka 7:10-12. Paulo ashuhudia kuwa kuja kwa Bwana kutatanguliwa na
“Kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na maajabu za uongo, na
katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea” 2Tes. 2:9-10. Yohana
naye anasema, “Naye, afanye ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka
mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya
nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya” ufunuo 13:13-14. Hapa sio ujanja wa
kibinadamu unaoelezwa. Watu hudangaywa na shetani kwa ishara ambazo wajumbe
wake huzifanya, sio wanazojifanya kuzifanya.