Fundisho
la patakatifu lilifungua siri ya uchungu ule uliowapata. Fundisho hilo
liliwafungulia ukweli wote jinsi ulivyo. Huonyesha jnsi mkono wa Mungu
ulivyowaongoza watu wa marejeo. Wale waliokuwa wakitazamia kuja kwake Yesu mara
ya pili kwa utukufu mwingi, walitiwa uchungu kwa kutokurudia kwake, walipoteza
matumaini yao kwa Yesu. Sasa katika patakatifu mno walimwona kwa upya Kuhani
wao mkuu, ambaye atakuja kama mfalme na Mwokozi wao. Nuru ya fundisho la
patakatifu iliangaza giza la wakati uliopita. Wakaona patakatifu iliangaza giza
la wakati uliopita. Wakaona wazi wakati uliopita, wakati uliopo, na wakati
ujao. Ingawa hawakuelewa ujumbe waliohubiri, walakini walikuwa sawa.
Makosa
hayakutokana na kuhesabu miaka ya unabii, lakini yalikuwa katika mambo
yatakayotokea mwisho wa siku 2300. Lakini yote yaliyotabiriwa na unabii
yalikuwa yametendeka.
Kristo
hakuja duniani, ila aliingia katika patakatifu mno huko mbinguni. “Nikaona
katika njozi za usiku na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na
mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye” Daniel
7:13.
Kuja
huko kulitabiriwa na Malaki pia. “Naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu
lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja,
asema Bwana wa majeshi”, Malaki 3:1. Kuja kwa Bwana katika hekalu lake kulikuwa
kwa ghafla, bila kutazamiwa, kwa watu wake. Hawakumtazamia.
Watu
hawakuwa tayari kumlaki Bwana wao. Kulikuwa bado kazi na maandalio yaliyokuwa
yakitakiwa.
Kwa
jinsi walivyomfuata kuhani wao mkuu kwa imani, katika huduma yake wajibu mpya
ungefunuliwa kwao. Ujumbe mwingine ulipasa utolewe kanisani.