WATU wengi, hasa walio Wakristo wapya, siku zingine huwa na mashaka moyoni juu ya mambo mengine katika Biblia ambayo hawawezi kuyaeleza ama kuyafahamu. Naye Shetani huyatumia mambo yale kwa kuwapunguzia imani yao katika kukubali kwamba Biblia ni ufunuo wa Mungu. Wanasema, “Nawezaje kujua njia iliyo ya haki? Kama kweli Biblia ni Neno la Mungu, nawezaje kuondolewa mashaka haya moyoni, nisije nikashikwa na fadhaa?”
Kila jambo atakalo Mungu tulisadiki, hakosi kutubainishia
sababu ya kuwa na imani juu ya jambo lile. Jinsi Mungu mwenyewe alivyo hai,
namna ya tabia zake, na ukweli wa Neno lake, mambo haya yote yamehakikishwa
kwetu kwa namna nyingi. Hata hivyo Mungu haoni ni afadhali kutuondolea nafasi
ya kuwa na shaka. Imetupasa kumwamini Mungu kwa vile tunavyobainishiwa mioyoni
mwetu juu ya mambo yasiyoonekana, siyo kwa ajili ya mambo yaliyo dhahiri katika
macho yetu ya kibinadamu.
Haiyamkiniki kwa nia ya kibinadamu kufahamu kabisa namna ya
tabia za Mungu wala kazi yake. “Kwa kutafuta utampata Mungu? Utampata Mwenyiezi
Mungu alivyo bora? Juu kama mbingu; utafanyaje? Chini kupita ahera; utajuaje?”
Ayub 11:7, 8.
Mtume Paulo alisema, “Ee ajabu ya utajiri na hekima na
maarifa ya Mungu; hazina hata kiasi! hukumu zake hazichunguziki, na njia zake
hazitafutikani!” Warumi 11:33. Na hata “mawingu na giza yamemzunguka,” “haki na
hukumu maweko ya kiti chake.” Zab. 97:2. Katika matendo yake juu yetu twaweza
kufahamu makusudi yake kwa kutosha kuona upendo wake na huruma yake isiyo na
kiasi, na jinsi uwezo wake ulivyo mkuu kupita cheo. Twaweza kutambua makusudi
yake kwa kadiri inavyotufaa; zaidi ya hayo imetulazimu kumtawakali Mwenyiezi
Mungu, ambaye moyo wake umejaa upendo.
Katika Neno la Mungu, vile vile katika sifa yake, kuna mambo
ya siri wasiyoweza wanadamu kuyafahamu. Jinsi dhambi ilivyoingia ulimwenguni,
jinsi Kristo alivyojifanya kuwa na umbo halisi la binadamu, uzazi wa pili jinsi
ulivyo, ufufuo, na mengineyo katika Biblia, ni mafumbo makubwa sana kushinda
akili za kibinadamu kuyaeleza, wala kufahamu maana yake vizuri. Lakini hatuna
sababu ya kuwa na shaka juu ya Neno la Mungu kwa ajili ya kutofahamu mafumbo ya
uongozi wake na majaliwa yake. Hata katika mambo ya ulimwengu na viumbe vyake
twaona mafumbo mengi tusiyoweza kuyafahamu. Wenye akili sana wameshindwa
kueleza habari za uhai jinsi ulivyo, hata uhai wa vidudu vidogo. M.ahali pote
pana maajabu tusiyoweza kuyafahamu. Kwa hivyo mbona tunastaajabu tukiambia kuwa
kuna mambo ya kiroho yasiyowaza kufahamiwa na kuelezwa na binadamu? Shinda
imekuwa kwa ajili ya udhaifu na akili chache za binadamu. Katika Maandiko
yenyewe Mungu ametuhakikishia jinsi Maandiko haya yalivyo yake, tusione shaka
moyoni juu ya Neno lake kwa sababu ya kutofahamu mafumbo yake yote.
Mtume Petro amesema kwamba katika Maandiko “yamo mambo
ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara,
huyapotoa . . . kwa upotevu wao wenyewe.” 2 Pet. 3:16. Wengine husema ya kwamba
mafumbo ya Biblia ni sababu ya kutosadiki maneno yake: lakini kwa kweli mafumbo
haya ni ushahidi mkuu kuwa yametoka kwa Mungu. Kama ingekuwa Biblia haina
habari za Mungu ila tu mambo yawezavo kuelezwa kwa urahisi na kufahamiwa na
binadamu, Biblia isingekuwa na hakika kwamba ni ya Mungu kweli.
Mafundisho ya Biblia juu ya wokovu, yametolewa kwa namna
ifaayo kwa mahitaji na matakwa ya moyo wa binadamu; watu wastaarabu na wenye
elimu nyingi wamevutwa na uzuri wa maneno yake; na hata watu duni waweza
kuelewa na kufahamu njia ya wokovu. Hata hivyo twaweza kuyasadiki hivi tu, kwa
kuwa Mungu ndiye anayetujulisha mambo hayo. Mpango wa Mungu juu ya ukombozi wa
wanadamu umebainishwa vizuri kwetu, ili mtu ye yote ajue la kufanya katika
kutubu kwa Mungu, na kuwa na imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ili apate
kuokoka kwa njia aliyoiweka Mungu. Walakini ndani ya mambo haya kuna mafumbo ya
Mungu yasiyofunuliwa ila kwa yule anayeyachunguza kwa moyo na bidii. Na kwa
jinsi anavyozidi kuyachunguza maneno ya Biblia, ndivyo anavyozidi kusadikishwa
kwamba ni Neno la Mungu aliye hai.
Wenye kumkana Mungu hutupilia mbali Neno lake kwa sababu
hawawezi kufahamu mafumbo yake yote. Hata na wengine wanaojidai kuwa wanasadiki
Biblia, huona mashaka moyoni juu ya jambo hilo. Mtume amesema, “Angalieni,
ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga
na Mungu aliye hai. Waeb. 3:12. Ni vizuri kujifunza mafundisho ya Biblia, na
kuchunguza “hata mafumbo ya Mungu,” (1 Wakor. 2:10 ), kwa kadiri yana-
vyofunuliwa katika Maandiko. Ingawa ni “kwa Bwana Mungu wetu yaliyo ya siri,”
ni kwetu sisi “yaliyofunuliwa,” Kumbu. 29:29. Lakini ni kusudi la Shetani
kuipotoa njia ya binadamu kama anataka kuyachunguza mambo. Kwa ajili ya ufundi
wanaojiona kuwa nao katika kuchunguza mafundisho ya Biblia, watu wengine huwa
wepesi wa kuchukizwa wasipoweza kueleza maana ya kila sehemu ya Maandiko kwa
namna ya kutosheleza nafsi zao wenyewe. Ni aibu kwao kukiri ya kwamba
hawayafahamu vizuri. Hawataki kumngojea Mungu hata atakapowafunulia maana ya
hakika. Huona kwamba akili za kibinadamu zimetosha kuwafahamisha Maneno ya
Mungu; nao wakishindwa kufanya hivi, basi huyakana kuwa si ya Mungu. Kuna
maelezo na mafundisho mengi ya dini yanayodhaniwa tu ya kuwa asili yake ni
maneno ya Biblia, lakini maana yake ni kinyume cha ukweli wa Biblia. Kwa ajili
ya mambo hayo watu wengi hushikwa na fadhaa na kuona shaka mioyoni mwao. Lakin
imekuwa hivyo si kwa ajili ya Neno la Mungu hasa, ila kwa kuwa wanadamu
wamepotoa maneno yake.
Kama wanadamu wangeweza kupata kufahamu jinsi Mungu alivyo hasa,
pamoja na matendo yake, basi, wasingekuwa na jambo jipya la kuvumbua,
wasingezidi kuelimishwa tena, wasingepata kuzidisha maendeleo yao ya kiroho.
Hapo Mungu asingekuwa Mwenye enzi; tena kwa vile ambavyo binadamu angekuwa
amefika mwisho wa elimu na maarifa yote, asingepata maendeleo yo yote tena.
Tumshukuru Mungu kwa kuwa si hivyo. Mungu ni mewnye uwezo wote, mwenye kujua
yote; “ndani yake zimo hazina zote za hekima na maarifa.” Wakol. 2:3. Maisha ya
milele wanadamu watakuwa wanachunguza na kuendelea kufahamu akili za Mungu,
wema wake, na enzi yake, bila mwisho.
Kuna njia moja tu kwa kupata kuelimishwa na kuendelea
kufahamu Neno la Mungu,— kama Roho ya Mungu inang’aa mioyoni mwetu na
kutumuliki. “Mambo ya Mungu hakuna ayajuaye ila Roho ya Mungu;” “maana Roho
huyachunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” 1 Wakor. 2:11,10. Tena Mwokozi
aliwaahidia wafuasi wake hivi: “Ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika
yote iliyo kweli; . . . atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni habari.” Yoh.
16:13, 14.
Mungu ataka binadamu atumie akili zake. Kuchunguza na
kujifunza Biblia kunaimarisha roho zetu kwa jinsi isivyowezekana katika
kujifunza mambo yo yote mengine. Ili tupate Kufahamu Maandiko, na mioyo yetu
isifadhaisnwe, imetupasa kuwa na imani na moyo mmoja kama watoto, tuwe tayari
kufundishwa ua kumwomba Roho Mtakatifu msaada wake. Tukiona uwezo wa Mungu na
akili zake jinsi vilivyo kuu zaidi pasipo kiasi, na kuelewa hali yetu ya
kutoweza kufahamu namna ya utukufu wake, hapo basi imetupasa kunyenyekea; na tunapofunua
katabu cha Neno lake, imetupasa kuwa na heshima na unyenyekevu moyoni kama tupo
mbele yake hasa.
Kuna mambo mengi ya fumbo, ambayo Mungu atawadhihirishia
wale watakao kweli kuyafahamu. Lakini bila uongozi wa Roho Mtakatifu binadamu
huelekea kupotoa maneno ya Biblia na kueleza maana isiyo ya kweli. Masomo mengi
ya wanadamu katika Biblia yamekuwa bure bila faida. Kama kitabu cha Neno la
Mungu kinafunuliwa bila heshima na maombi: mtu asipomkazia Mungu fikara zake na
upendo wake na kufanya mapenzi ya Mungu, bila shaka atashikwa na fadhaa. Ndipo
Shetani atayatawala mawazo yake, na kumtilia moyoni mwake maelezo ya Biblia ya
yasiyo ya kweli. Kila mara wanadamu wasipopatana na Mungu katika maneno na
matendo yao, ingawa ni wenye maarifa ya namna gani, bila shaka watakosa
kufahamu Maandiko, tena haifai kuyaamini maelezo yao. Wengi wao walio na
mashaka moyoni, asili ya kushuku kwao ni kupenda dhambi. Masharti na vizuizi
vya Neno la Mungu havipendezi wenye moyo wa kujisifu; na wale wasiokubali
kufanya matakwa ya Biblia yake huwa wepesi kutosadiki kuwa ni Neno la Mungu
halisi. Bali, wote watakao kwa moyo kujua matakwa ya Mungu na huyafanya, hao
nao watabainishiwa kuwa Biblia na Maneno ya Mungu yawezayo kuwapa hekima hata
wapate wokovu.
Kristo asema, “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua
habari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu.” Yoh. 7:17. Badala ya kubishana
bure juu ya mambo msiyoweza kuyafahamu, ni heri mfanye kila wajibu wenu kwa
vile mnavyofahamu na kuelewa nao, ndipo mtasaidiwa kuyafahamu na kuyafanya yale
ambayo sasa mnayaonea mashaka.
Mungu ataka tujihakikishie ukweli wa Neno lake na ahadi
zake. Asema, “Onjeni mwone BWANA ndiye mwema.” Zab. 34:8. Tusitegemee neno la
wengine, ila tuonje sisi wenyewe na kuona wema wake. Asema tena, “Ombeni, na
mtapata,” Yoh. 16:24. Ahadi zake zitatimia. Haziwezi kuwa na upungufu. Na kwa
vile tunavyomkaribia Yesu, na kufurahishwa na upendo wake, ndivyo nuru yake
itakavyong’aa mioyoni mwetu, tena mashaka na giza vitaondolewa. Mtume Paulo asema
ya kwamba Mungu alituokoa “na nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika
ufalme wa Mwana wa pendo lake.” Wakol. 1:13. Kila ambaye “amepita toka mauti
hata uzima” anaweza kutia “muhuri wake kwamba Mungu ni wa kweli.” Yoh. 5:24; 3:
33. Awe- za kushuhudia, “Nimepata msaada kwake Yesu; naye ameniruzuku mahitaji
yangu yote, nimeshibishwa njaa ya moyo wangu; tena sasa Biblia inakuwa kwangu
ufuno wa Yesu Kristo. Waniuliza mbona namwamini Yesu?—Kwa kuwa ni Mwokozi
wangu. Kwa nini nasadiki Biblia? Kwa sababu nimeona kuwa ni sauti ya Mungu
moyoni mwangu.” Twaweza kuwa na ushuhuda ndani yetu kuwa neno la Biblia ni
kweli, tena Kristo ni Mwana wa Mnngu. Twajua kwamba hatufuati hadithi
zilizotungwa kwa werevu. 2 Petro 1:16.
Petro awaamuru Wakristo walio ndugu zake, “Kaeni katika
neema, na katika kumjua Bwaua wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.” 2 Pet. 3:18.
Watu wa Mungu wakikaa katika neema yake, watazidi kudhihirishiwa Neno lake.
“Matembezi yao wenye haki kama nuru nyeupe, iangazayo ikizidi hata mchana
utimiapo.” Methali 4:18.
Kwa imani twaweza kutazama mbele hata mpaka ufalme wa Mungu,
na kutumaini ahadi ya Mungu juu ya kutuzidisha akili, na jinsi uwezo wetu wote
utakavyoungamana na uwezo wa Mungu. Twaweza kufurahi kwa kuwa yote ambayo sasa
tumeshikwa na fadhaa nayo, hapo ndipo yatadhihirishwa kwetu; mambo yanayokuwa
magumu kufahamiwa, wakati huo yataelezwa dhahiri. “Wakati wa sasa tunaona kwa
kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa
sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.” 1 Wakor
13:12.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kukubali Neno lake
Nina raha moyoni.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kwake daima napata
Uzima na amani.
Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu, Mpendwa na Rafiki
UJUMBE HUU UNALETWA KWENU NA CHARLES SHIBITA PUNDA WA YESU KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NUMBER
UJUMBE HUU UNALETWA KWENU NA CHARLES SHIBITA PUNDA WA YESU KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NUMBER