MAISHA BAADA YA KIFO IMEKUWA NI SWALI LA KILA MTU ULIMWENGUNI, NA LIMEKUWA NI SWALA MTAMBUKA KWA SABABU SWALA LA KIFO HALINA UBAGUZI KILA KIUMBE HAI NI HALALI KWA KIFO
JE? BAADA YA KIFO NINI KINACHOTOKEA WENGINE HUSEMA MTU AKIFA HUENDA MBINGUNI NA WENGINE HUSEMA MTU AKIFA HAENDI POPOTE PALE BALI HUBAKIA HAPAHAPA DUNIA
HABARI NJEMA NI HII MAJIBU YAPO NA YANAPATIKANA HAPO CHINI.
Shetani ambaye alianzisha uasi huko mbinguni, anatamani
kuwaunga weneyji wa dunia hii katika vuta yake na Mungu. Adamu na hawa kwa
furaha walikuwa watiifu wa sheria ya Mungu, utii wao ulikuwa hakikisho la daima
kwa madai ya Shetani kwu sheria ya Mungu ni ya kukandamiza. Shetani aliazimia
kuwaangusha, ili apate kutawala duni hii, na kuusimamisha utawala wenye
kupingana na Mungu.
Adamu na hawa walikuwa wametahadharishwa kuhusu hatari ya
adui huyu. Lakini Shetani alijificha kabisa akitenda mambo yake kisirisiri.
Akimtumia nyoka kama chombo chake, nyoka ambaye alikuwa kiumbe kizuri
alimzungumzia Hawa, akisema, “Eti hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda
ya miti yote ya bustanini?” hawa hakuthubutu kushauriana na adui akaanguka kwa ulaghai
wake adui; “Mwanamke akamwambia nyoka; Matunda ya miti ya bustanini twaweza
kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya busatani Mungu amesema Msiyale
wala msiyaguse msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, hakika hamtakufa; kwa
maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo mtafumbuliwa
macho, nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya”. Mwanzo 3:1-5.
Hawa akakubali kushindwa, na kwa mvuto wake Adamu naye
akaingia dhambini. Wote wakayakubali maneno ya nyoka, wakaonea mashaka maneno
ya Mwumbaji wakaona nafsini mwao kuwa aliingilia uhuru wao.
Lakini Adamu aligundua nini maana ya maneno ya Mungu, Siku
mtakayokula matunda ya mti huo, mtakufa hakika? Je, yalikuwa na maana ya
kumzuia asiingie katika hali bora zaidi? Adamu hakuona kuwa maana ya maneno ya
Mungu ilikuwa hivyo alivyosema nyoka. Mungu akasema kuwa adhabu ya kutotii
maneno yake ni kurudi mavumbini, yaani kufa. “Maana wewe ni mavumbi, na
mavumbini utarudi”. Mwanzo 3:19. Maneno ya shetani kuwa, macho yenu
yatafumbuliwa, yalikuwa na ukweli tu katika sehemu hii, maana macho yao
yalifumbuliwa wakaona upumbavu wao. Wakajua mabaya na kuonja uchungu wa matunda
ya uasi wao.
Mti wa uzima ulikuwa na uwezo wa kuendeleza uzima. Adamu
alikuwa na hiari ya kuuendea mti wa uzima bila kikomo na kuyafurahia matunda
yake, naye angeishi milele. Lakini alifanya dhambi akazuiliwa asiyale tena
matunda ya mti wa uzima, hivyo akawa mtu wa kufa. Hali ya kutokufa ilikuja kwa
ajilia ya uasi, na mwanadamu asingekuwa na tumaini lolote la kuishi milele,
kama Mungu kwa rehema zake asingemtoa Mwanawe kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi
za mwanadamu. “Mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wametenda dhambi”
“Kristo Yesu aliyebatilisha mauti na kufunua uzima na kutokuharibika kwa ile
Injili” Ni kwa njia ya Yesu tu ndipo hali ya kutokufa hupatikana. “Amwaminiye
Mwana yu na uzima wa milele, asiyemwamini Mwana hataona uzima” Rumi 5:12; Tim
1:10; Yohana 3:36
UJUMBE HUU UNALETWA KWENU NA CHARLES SHIBITA PUNDA WA YESU KWA MASWALI NA MAJIBU ULIZA AU PIGA 0763371047 au email adress pshibita@gmai.com