"Lakini pasipo
imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima
aamini kwamba yeye
yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao" (Waebrania 11:6).
Wako wengi katika
ulimwengu wa Kikristo wanaodai kwamba yale yote yanayotakiwa ili
kuokolewa ni kuwa na
imani; kwamba matendo si kitu, ila imani peke yake ndiyo ya lazima.
Lakini Neno la Mungu
linatuambia sisi kwamba imani pasipo matendo imekufa.
Wengi wanakataa kuzitii amri [kumi] za Mungu, ila wanaikuza sana imani. Lakini basi, imani lazima iwe na msingi
wake.
Ahadi zote za Mungu zimetolewa kwa masharti.
Iwapo tunafanya mapenzi yake, iwapo
tunakwenda katika
nuru yake, basi, hapo ndipo tunaweza kuomba lo lote tutakalo, nalo
tutatendewa. Wakati
sisi tunajitahidi kwa bidii kuwa watiifu, Mungu atazisikia dua zetu; lakini
hataweza kutubariki
sisi katika uasi wetu. Ikiwa tutachagua kutozitii amri zake [kumi], basi,
tunaweza kupiga
kelele, tukisema, "Imani, imani, uwe na imani peke yake," na jibu
hili litatujia
kutoka katika Neno
imara la Mungu, likisema, "Imani pasipo matendo imekufa" (Yakobo
2:20,26). Imani kama
hiyo itakuwa tu kama shaba iliayo na upatu uvumao. Ili kuweza kupata
mafao ya neema ya
Mungu ni lazima tufanye sehemu yetu; tunapaswa kufanya kazi kwa uaminifu
na kuzaa matunda
yapasayo toba.
Sisi ni watenda kazi pamoja na Mungu. Usikae
kivivu, ukiwa unangojea tukio moja kubwa, ili
kumfanyia Bwana kazi
kubwa. Usiache kufanya kazi inayokukabili moja kwa moja njiani mwako,
lakini unatakiwa
kuzitumia vizuri zaidi nafasi ndogo ndogo zinazojitokeza kukuzunguka....
Kupigana Mieleka,
Kufanya Kazi, na Kujitahidi
Yatupasa kufanya yote yale yanayowezekana kwa
upande wetu kupiga vita vile vizuri vya
imani. Yatupasa
kupigana mieleka, kufanya kazi, kujitahidi, kusumbuka kuingia katika mlango ule
ulio mwembamba.
Yatupasa kumweka Bwana mbele yetu daima. Tukiwa na mikono safi, tukiwa
na mioyo safi,
yatupasa kujaribu kumheshimu Mungu katika njia zetu zote.
Msaada umetolewa
kwetu ndani yake yeye
aliye na uweza wa kuokoa. Roho yule wa kweli na nuru atatuhuisha na
kutufanya upya kwa
utendaji wake wa siri [usioweza kuelezeka]; kwa kuwa maendeleo yetu yote ya kiroho yanatoka kwa Mungu, si ndani yetu wenyewe.
Mtenda kazi wa kweli atakuwa na nguvu
ya Mungu ya
kumsaidia, lakini yule aliye mzembe hataweza kusaidiwa na Roho wa Mungu.
Kwa njia moja tu sisi tunaachwa kutegemea
nguvu zetu wenyewe; yatupasa kujitahidi kwa
nguvu zetu zote kuwa
na bidii na kutubu, kuitakasa mikono yetu na kuisafisha mioyo yetu kutokana na uchafu wa kila namna; yatupasa kukifikia kiwango kile cha juu kabisa, tukiamini kwamba Mungu atatusaidia katika juhudi zetu hizo.
Yatupasa kutafuta kama tunataka kuona, na kutafuta
kwa imani; yatupasa
kubisha [kugonga mlango], ili mlango huo upate kufunguliwa kwetu.
Biblia
inatufundisha kwamba
kila kitu kinachohusu wokovu wetu hutegemea njia yetu ya utendaji. Iwapo
sisi tutapotea
[tutaangamia], basi, uwajibikaji huo utakuwa ni wetu kabisa. Iwapo msaada
umetolewa kwetu, na
iwapo sisi tunayakubali masharti ya Mungu, basi, tunaweza kuupata uzima
ule wa milele.
Yatupasa kuja kwake Kristo kwa imani, yatupasa kujitahidi kufanya imara kuitwa
kwetu na uteule wetu.
Msamaha wa dhambi umeahidiwa kwake yeye
atubuye na kuamini; taji ile ya uzima
itazawadiwa kwake
yeye atakayekuwa mwaminifu mpaka mwisho.
Tunaweza kukua katika neema
hiyo kwa kuendelea
kukua katika neema ambayo tayari tunayo.
Yatupasa kujitunza wenyewe
tusitiwe mawaa na
ulimwengu huu kama tutataka kuonekana kuwa hatuna lawama katika siku ile
ya Mungu.
Imani na
matendo huenda bega kwa bega; hufanya kazi yao kwa ulinganifu katika kazi
ile ya kutupatia
ushindi. Matendo pasipo imani yamekufa, na imani pasipo matendo imekufa.
Matendo kamwe
hayataweza kutuokoa; ni wema wake Kristo utakaofaa kwa ajili yetu.
Kwa njia
ya imani katika yeye,
Kristo atazifanya juhudi zetu zote zisizokuwa na ukamilifu wo wote
kukubalika kwa Mungu.
Imani tunayotakiwa kuwa nayo si imani ile ya kutofanya kitu cho chote;
imani iokoayo ni ile
itendayo kazi kwa upendo na kuitakasa nafsi. Yule atakayeinua juu kwa
Mungu mikono yake
iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano [mashaka] atakwenda kwa akili
katika mapito [njia]
ya amri [kumi] za Mungu.
Iwapo sisi tunataka kupewa msamaha wa dhambi
zetu, basi, yatupasa kwanza kutambua dhambi
ni nini, ili tupate
kutubu na kuzaa matunda yapasayo toba.
Ni lazima tuwe na msingi imara kwa
imani yetu; lazima
ijengwe juu ya msingi wa Neno la Mungu, na matokeo yake yataonekana katika
utii kwa mapenzi ya
Mungu yale yaliyodhihirishwa [yaliyofunuliwa]. Asema hivi yule mtume, "...
[na huo utakatifu]
ambao hapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao" (Waebrania 12:14).
Imani na matendo vitatufanya sisi tuwe na
uwiano sawa na kutufanya tuwe na mafanikio katika
kazi ile ya
kuikamilisha tabia yetu ya Kikristo. Yesu asema hivi, "Si kila mtu
aniambiaye, Bwana,
Bwana, atakayeingia
katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu
aliye mbinguni"
(Mathayo 7:21). Akiwa anazungumza juu ya chakula cha kimwili, mtume huyo
alisema, "Kwa
kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa
mtu hataki kufanya
kazi, basi, asile chakula" (2 Wathesalonike 3:10). Sheria [kanuni] iyo
hiyo
hutumika kuhusiana na
lishe yetu ya kiroho; iwapo mtu ye yote atataka kula mkate ule wa uzima, basi, na ajitahidi [afanye juhudi] kuupata.
Tunaishi katika kipindi cha maana na cha
kutamanisha [kusisimua] sana cha historia ya
ulimwengu huu.
Tunahitaji imani nyingi kuliko tulivyopata kuwa nayo [huko nyuma]; tunahitaji
kushikwa kwa nguvu
zaidi kutoka juu. Shetani anafanya kazi yake kwa nguvu zake zote ili apate
kutushinda, kwa maana
yeye anajua ya kuwa ana wakati mchache tu wa kufanya kazi yake
Paulo
alikuwa anaogopa na
kutetemeka katika kutimiza wokovu wake; na sisi, je! tusingeogopa
kwamba ahadi ile
tuliyoachiwa tusije tukaonekana kuwa tumeshindwa kuitimiza, na sisi wenyewe
kuonekana kuwa
hatustahili kupewa uzima ule wa milele? Yatupasa kukesha na kuomba,
kujitahidi kwa juhudi
ile inayotuletea maumivu makali ili tupate kuingia katika mlango ule ulio
mwembamba.
Yesu Anaufidia
Upungufu Wetu
Hakuna udhuru wo wote kwa kutenda dhambi au
kwa kuwa wazembe. Yesu ametangulia katika
njia ile, naye
anataka sisi kufuata katika nyayo zake. Yeye ameteswa, amejitoa mhanga kuliko
mtu
ye yote miongoni
mwetu anavyoweza kufanya ili apate kutuletea wokovu ule karibu sana nasi.
Hatuna haja ya kukata
tamaa. Yesu alikuja katika dunia yetu kumletea mwanadamu uweza wa
Mungu ili kwa neema yake,
tupate kubadilishwa [tabia zetu] na kufanana naye.
Kama moyoni mwake imo nia ya kumtii Mungu, na
juhudi zinafanywa naye kuelekea kwenye
mwisho huo, basi,
Yesu ataikubali nia yake na juhudi hiyo kuwa ndiyo huduma bora kabisa
iliyotolewa na
mwanadamu huyo, naye ataufidia upungufu wake [mwanadamu huyo] kwa wema
wake mwenyewe wa
uungu. Walakini hatawakubali wale wanaojidai kuwa wanamwamini, ila
hawataki kuzitii amri
[kumi] za Baba yake. Tunasikia maneno mengi kuhusu imani, lakini
tunahitaji kusikia
maneno mengi zaidi juu ya matendo.
Wengi wanajidanganya nafsi zao wenyewe
kwa kuendelea kuishi
kwa kufuata dini rahisi, inayoruhusu mambo yote, yaani, isiyokuwa na
msalaba.
Lakini Yesu asema hivi, "Mtu ye yote
akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike
msalaba wake,
anifuate" (Mathayo 16:24).
UJUMBE HUU UMELETWA KWENU NA CHARLES SHIBITA PUNDA WA YESU. KWA MAWAILIANOZAIDI PIGA SIMU NUMBER 0763371047