Neno maombi limetiokana na neon la kiebrania tephillah, limaanishalo ombi au zaburi za kusifu, vile vile kwa kigiriki huitwa deeµsis, ikimaanisha “kusihi,” “ombi,” na proseuche, “ombi,” “ungano.” Muungano na Mungu huhusisha kisifu, shukrani na kusihi. Maombi hujengwa na Imani kwamba Mungu husikia, hujali, na ni “mtoaji kwa wale wamtafutao kwa bidii. (Waebrania 11:6). Hudumisha na kurejesha mahusiano na Mungu
AFICHAYE dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” Mithali 28:13.
Masharti yanayompasa mtu kufanya ili apate rehema ya Mungu si magumu, ni ya haki na ya maana.
Bwana Mungu hataki tufanye mambo mazito ili tusamehewe dhambi; hadai tuende safari ndefu na taabu ya kuzuru patakatifu; wala kujipigapiga kwa kuonyesha kutubu kwetu, ili Mungu apendezwe nasi, ama kwa kulipia makosa yetu. Asema tu kwamba anayeungama dhambi zake na kuziacha, ndiye atakayerehemiwa.
Mtume Yakobo asema, “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa.” Yak. 5:16. Ungama dhambi zako hasa kwa Mungu, ambaye yeye tu ndiye awezaye kuzisamehe; lakini makosa ambayo umewafanyia wanadamu, basi uyaungame mbele ya wanadamu.
Hivi ikiwa umefanyia fulani yaliyomchukiza kwa njia yo yote, nenda kwake na kuungama kosa lile ulilomfanyia, naye amepaswa kulisamehe kabisa. Nyuma Yake imekupasa kuomba msamaha kwa Mungu kwa sababu huyo mwenzako kiumbe cha Mungu, na kumfanyia mwanadamu makosa ni kumfanyia makosa Muumba na Mwokozi wake. Hivyo kwa njia ya kuomba mbele ya, ‘Mwombezi wetu, Kuhani Mkuu wetu ambaye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi naye awezaye “kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu” huweza kutusafi sha uchafu wote wa dhambi. Ebr. 4: 15. ,
YESU akiwakumbusha juu ya kushinda majaribu aliwaambia
20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga
SOMA KWA UFUPI HISTORIA YA ZIWA GALILAYA .LINGANISHA NA IMANI YA WANAFUNZI LO
Ziwa la Galilaya lilikuwa na ukubwa wa 20x12km.Mara nyingine dhoruba hutokea katika ziwa hili.Zamu ya nne ilikuwa karibu saa tisa asubuhi(25).Wanafunzi walikuwa tayari ziwani kwa muda huo.1. Kwa nini Yesu aliwatuma wanafunzi wake ziwani ingawa yeye shaka alijua ni nini kitakachotokea huko (22)?
Mungu anapokusudia hitimisho (hasa katika maswala ya Uponyaji), pia hukusudia namna ya kutimiza kusudi hilo (kuonyesha hitaji la kuponywa jambo ambalo lahitaji imani.)Maombi hayabadili mpango wa Mungu bali hufanya kusudi la Mungu litimie. Maombi hutengeneza mazingira mazuri ya jinsi na namna tunavyofikiria mipango ya Mungu kwetu, kwa njia hiyo mhumuunganisha Mwanadamu na Mbingu wakati wote.
Maombi ni ufunguo wa mibaraka mingi ambayo Mungu amenuia kumpatia kila mwanaadamu, ni njia ya pekee ambayo mwanadamu hupata nafasi ya kufunua moyo wake kwa Mungu.
Ikumbukwe kwamba tunaposali tunavyotwa karibu zaidi na Mungu, Viumbe ambao hawajaanguka dhambini yaani malaika hujisikia kuwa karibu na Mungu mda wote wakimsujudu jambo ambalo ni msingi wa furaha yao, ni wazi kabisa kuwa malaika hushangaa sana waonapo wanadam wanakaa bila Roho matakatifu kwa njia ya maombi ya kudumu.
Giza na wimbi la dhambi huwa karibu sana na watu wote wapuuziaao maombi, bila maombi ya kudumu na mara kwa mara tunajiweka katika hatari ya kuiacha nuru na kutembea gizani.
MAMBO YATUTHIBITISHIAYO KUWA MUNGU ATAJIBU MAOMBI YETU
a.Isaya 44:3 . Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu;nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu ya utakao wazaa.
b.Hitaji letu ni kithibitisho tosha cha kumfanya Mungu atufungulie mibaraka tele.Mathayo 7:7.Ombeni, nanyi mtapewa;tafuteni, nanyi mtaona;bisheni; nanyi mtafunguliwa. Warumi 8.32,Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwaajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirfimia mambo yote pamoja naye?
2)Acha maisha ya dhambi ukishikilia dhambi yoyote uijuayo maishani mwako Mungu kamwe hatosikia maombi yeko lakini ukiungama na kuiacha kwa kumuendea Mungu kwa moyo uliopondeka maombi yeko yatasikiwa. Ni haki na damu ya Yesu pekee itupatiayo ukubali mbele za Mungu.
3) Kuwa na Imani, ni kipengele kingine muhimu sana kwa maombi yenye mafanikio.
a. Waebrania 11:6. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
b. Marko 11;24. Kwasababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, amini ya kwamba mtayapokea, nayo yatakuwa Yenu. Ni udhihirisho kwetu kwamba Mungu hana mipaka kwa yeyote amjiae kwa imani, lakini kuna nyakati ambapo waweza kuomba halafu usipate majibu papo hapo jambo la kuzingatia ni kuendelea kudai ahadi za Mungu na kuwa mvumilivu. Wakati mwingine waweza kuomba jambo ambalo Mungu anaona si mbaraka kwako hivyo waweza usijibiwe na badala yake Mungu akakupatia linalokufaa zaidi. Mungu huzingatia muda kwa kila alifanyalo hivyo waweza kuomba jambo ambalo Mungu anaona si wakati wake kukupatia wewe endelea kudumu katika maombi saa na wakati utakapofika utajibiwa.
4)Kuwa mwepesi wa kuwasamehe waliokukosea, ukiwa na moyo mgumu kuwasamehe wale wakukoseao kumbuka kwamba unaweka kikwazo cha maombi yako kutokujibiwa. Kama upendavyo kusamehewa na Mungu vivyohivyo wapaswa kuwasamehe wote wakukoseao.
a.Mathayo 6:12. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
5)Uvumilivu, katika maombi hii ni kanuni ya pekee sana ya maombi yanayo jibiwa. Wapaswa kuwa mvumilivu kwa kuzingatia yafuatayo. Uvumilivu katika maombi hudhihirisha kwamba ombi lako ni la muhimu kwako kama lilivyo la muhimu kwa Mungu. Lakini pia si kila ombi lijibiwalo kama utarajiavyo katika 2 Cor 12:9-10 Paulo alimuomba Mungu amuondolee muiba uliomsumbua maishani mwake lakini Mungu hakujibu ombi hilo kwa faida ya Paulo.
a. Wapaswa kuwa mtu wa maombi na kudumu katika maombi huku ukitoa shukrani. Warumi 12:12. kwa Tumaini, mkifurahi; katika dhiki , mkisubiri; katika kusali mkidumu. Wakolosai 4:2. Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; 1 Petro 4:7 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia ; basi iweni na akili, mkeshe katika sala. Wafilipi 4:6, Msijisumbue kwa neno lolote; Bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane kwa Mungu. Yuda 1: 20,21. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
b.Maombi yasiyokoma ni muungaano usiovunjika kati ya roho na Mungu, ili kwamba uzima kutoka kwa Mungu ububujike katika maisha yetu, na kutoka katika maisha yetu usafi na utakatifu umrudie Mungu.
6) Weka mahitaji yako, huzuni , furaha, dukuduku kwa Mungu na kamwe huwezi kumpa mzigo wala kumchosha.
a. Yakobo 5:11, Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri.Mmesikia subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya Kwamba Bwana ni mwingi wa rehema mwenye huruma .Hakuna ukurasa wa maisha wetu ambao ni mgumu kusomwa na Mungu na wala hakuna tatizo kubwa kwa yeye kushindwa kulitatua
7) Omba kwa jina la Yesu, hii ni kwasababu Yesu ndiye njia na kweli na uzima na hakuna mtu awezaye kwenda kwa Baba bila kupitia kwa Yesu. Yeye alimwakilisha Mungu hapa duniani na pia anamwakilisha kila mwanadamu mbinguni mbele ya Mungu Baba.
a.Yohana 16:26,27. Na siku ile matomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi ntawaombea kwa Baba. Nalitoka kwa Baba nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba. Yohana 15:16. Si ninyi mlionichagua mimi ,bali ni mimi niliyewacahgua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda , na matunda yenu yapate kukaa, ili kwamba lolote mmwombalo baba kwa jina langu awapeni. Tuangaze macho yetu Mbinguni na kumtazama Yesu amabaye “Naye ,kwasababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee.(Waebrania 7:25.)
8)Mtukuze Mungu kwa wema aliokutendea na uwe mtu wa kutoa shukrani
a.Zaburi 107:8. Na wamshukuru BWANA , kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
Kumbuka, maombi mengi huambatana na mafanikio mengi, maombi kidogo mafanukio kidogo , vilevile pasipo maombinb hakuna mafanikio. Mungu anahitaji kwamba kupitia somo hili awe amekufungua akili kutambua njia na ufunguo pekee wa mafaniko ambao yawezekana haukuujua hapo mwanzo, dumu katika maombi
ITAENDELEA .........