MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

JE! YESU NINANI? NA ALITOKA WAPI?.


ILI KUJUA YESU ALITOKA WAPI NA  NINANI? LAZIMZ KWANZA TUANZE  NA UTABILI WAKE
Image result for historia ya nabii isaya

HAPA  UNABII UNATHIBITISHA KUWA  YESU  NI MUNGU KUPITIA NABII ISAYA.
Isaya Alikuwa Nani?
MAANA YA JINA: “Wokovu wa Yehova”
FAMILIA: Mtu aliyeoa, mwenye angalau wana wawili
MAKAO: Yerusalemu
MIAKA YA UTUMISHI: Angalau miaka 46, kuanzia karibu mwaka wa 778 K.W.K. hadi wakati fulani baada ya mwaka wa 732 K.W.K.
WAFALME WA YUDA WALIOKUWAPO SIKU ZAKE: Uzia, Yothamu, Ahazi, Hezekia
MANABII WALIOKUWAPO SIKU ZAKE: Mika, Hosea, Odedi
6  Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
7  Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

Isaya 6: 8, "Kisha nikasikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, mimi hapa, nitume mimi! '" Isaya 7:14, "Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanaume, naye atamwita jina lake Imanueli"
 1
1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. 2Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA; ISAYA 11:1-2
DANIEL ANAMSEMA KAMA HAKIMU ATAKAYE HUKUMU ULIMWENGU
13  Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
14  Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa
Image result for jesus from heaven pictures

Image result for jesus from heaven pictures


 YOHANA PIA ALISHU HUDIA KATIKA MAONO KUWA YESU NI MUNGU


Hapo Mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu. Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu.Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye. Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu. Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane, ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini.Yeye hakuwa huo mwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Huu ndio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni, na kuwaangazia watu wote. 10 Basi, Neno alikuwako ulimwenguni; na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. 12 Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu. 13 Hawa wamekuwa watoto wa Mungu si kwa uwezo wa kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali Mungu mwenyewe ndiye baba yao. 14 Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na kweli. Yohana 1:1-14

MTUME PAUL ALISHUHUDIA PIA KRISTO NI MUNGU, TWENDE PAMOJA KATIKA MAFUNGU YAFUATAYO
 
Image result for GOD

Image result for GOD

 Iweni na mtazamo huu wa akili ndani yenu ambao ulikuwa pia ndani ya Kristo Yesu,+  ambaye, ingawa alikuwa katika umbo la Mungu,+ hakufikiria kufanya unyakuzi, yaani, kwamba yeye awe sawa na Mungu.+  Hapana, bali alijiondolea mwenyewe hali yake na kuchukua umbo la mtumwa+ na kuwa kama wanadamu.+  Zaidi ya hayo, alipojikuta katika umbo la mwanadamu,+ alijinyenyekeza naye akawa mtiifu mpaka kifo,+ ndiyo, kifo juu ya mti wa mateso.+  Kwa sababu hii pia Mungu alimpandisha kwenye cheo cha juu zaidi+ na kumpa kwa fadhili jina lililo juu ya kila jina lingine,+ 10  ili katika jina la Yesu kila goti lipigwe la wale walio mbinguni na wale walio duniani na wale walio chini ya nchi,+ 11  na kila ulimi ukiri+waziwazi kwamba Yesu Kristo ni Bwana+ kwa utukufu wa Mungu Baba.+
 WAFILIPI 2:5-11

  1. SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU.
1.YESU NI MUUMBAJI.
Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake ( YOHANA 1:3,14 )  “vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili;nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli”.Yesu aitwa Neno la Mungu (UFUNUO 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu“(YOHANA 1:1)..  na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (WAKOLOSAI 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani.Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.
2.YESU ALIKUWEPO KABLA YA VITU VYOTE KUWEPO DUNIANI.
( WAKOLOSAI 1:17 ) “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote;na vitu vyote hushikamana katika yeye”.(MIKA 5:2 ) Basi,wewe Bethlehemu,Efrata,uliyemdogo kuwa miongoni mwa maelfu za Yuda;kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale;tangu milele“.
Yesu Kristo alikuwako kabla ya Nabii Ibrahimu kuwako(YOHANA 8:52-58)Watu walioambiwa maneno hayo n a Yesu mwenyewe wliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwa anakufuru.Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho,( YOHANA 4:24)..YOHANA 17:5,24.WAEBRANIA 7:3 ).Imasema  “hana baba,hana nana,hana wazazi,hana mwanzo wa siku zake,wala mwisho wa uhai wake,bali amefananishwa na Mwana wa Mungu;huyo adumu kuhani milele”.YESU ni alfa na omega,wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (UFUNUO 22:13).Bali kwa damu ya thamani,kama ya mwana-kondoo asiye na ila,asiye na waa,yaani ya Kristo.Naye amejulikana kweli tangu zamani,kabla haijawekwa misingi ya  dunia,lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yetu ( 1PETRO 1:19-20 ).
3.YESU NI MTAWALA JUU YA YOTE.  HII NI SIFA YA MUNGU PEKEE.
  (YOHANA 330 ) “Yeye ajaye kutoka juu,huyo yu juu ya vyote.Yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia,naye anena mambo ya duniani,yeye ajaye kutoka mbinguni yuu juu  ya yote” . ( YOHANA 13:13 ) “Ninyi mwaniita ,Mwalimu, na Bwana;nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo“. ( WARUMI 14:9 ) “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii,awamiliki waliokufa na walio hai pia”. Nenokumiliki ni kutawala sifa ya kutawala ni sifa ya Mungu pekee.
4,YESU KRISTO NI ZAIDI YA MTU YEYOTE AU NABI AU MTUME YEYOTE YULE..
( WAEBRANIA 3:1-7 ) Mustari 3 unasema,Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahiliutukufu zaidi kuliko Musa,kama vile yeye atengenezayenyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”..Anayezungumziwa hapa ni Yesu Kristo Mungu muumbaji. YESU ,ameketi mkono wa kuume wa ukuu huko mbinguni (WAEBRANIA 1;3-4).
5,YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WALIMWENGU (WATU) WOTE.

Image result for jesus from heaven pictures
( ZABURI 58:11 ), ‘Hakika yuko Mungu anayetawala katika dunia“. (UFUNUO 18;8 ) “Kwasababu hiyo,mapigo yake yatakuja katika siku moja,mauti na huzuni na njaanaye atateketeza kabisa kwa moto.Kwamaana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“.Tene ndiye atakaye ihukumu Dunia yote “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote,bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.(MATHAYO 25:31-32 ) “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake,namalaika watakatifu wote pamoja naye,ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufuwake.Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake,naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi” .(MATENDO 10:42 ) “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( WARUMI 2:16 )  “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na injili yangu,kwa Kristo Yesu.( 2TIMOTHEO 4:1 ) “Nakuagiza mmbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu,atakayewahukumu waliohai na waliokufa;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.
6.YESU HABADILIKI TENE HANA KIGEUGEU.                                     {WAEBRANIA 13:8} “Yesu Kristo ni yeye yule jana na leohata milele“. ( WAEBRANIA 1:10-12 ) “Wewe ,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi.Na mbingu ni kazi ya mikono yako;Hizo zitaharibika,lakini wewe unadumu;Nazo zote zinachakaa kama nguo,Na kama mavazi,utazizinga,nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,na miaka yako haitakoma“. ( MALAKI 3:6 ) Kwa kuwa mimi,Bwana,sina kigeugeu” ( ZABURI 102:26-27 ) “Hizi zitaharibika,bali wewe utadumu;Naam,hizi zitachakaa kama nguo;na kama mavazi utazibadirisha,nazo zitabadilika.Lakini wewe U yeye yule;na miaka yako haitakoma“. ( YAKOBO 1:17 ) “Kwake hakuna kubadilika,wala kivulu cha kugeukageuka”.
  1. YESU YUPO KILA MAHALI ,KOTEKOTE DUNIANI.
Image result for jesus from heaven pictures
( MATHAYO 18:20 ) “Kwa kuwa walipo wawili watatu,wamekusanyika kwa jina langu,mimi nipo papo hapo katikati yao”. Mwenye uwezo wa kukaa mahali pote ni Mungu
Yesu aliabudiwa na kusujudiwa akiwa hapa duniani,Sifa ya kuabudiwa na kusujudiwa ni ya Mungu pekee hivyo Yesu ni Mungu.(MATHAYO 4:10).
  • Hata malaika wote wanamsujudia Yesu (UFUNUO 22:8-9,WAEBRANIA 1;6).
  • Ndiyo maana Yesu alisujudiwa akiwa mtoto mchanga alipozaliwa (MATHAYO 2:11,MATHAYO 14:33<LUKA 24;52).
  • Hata pepo wachafu walimsujudia yesu.

ujumbe wa MUNGU  ni huu

Image result for kitabu cha ufunuo 14
Kisha nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu wote waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote, watu wa lugha zote na rangi zote. Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari na chemchemi za maji.


Tazama! Anakuja katika mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina. “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Uwezo, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.


Image result for jesus from heaven pictures



 Ayubu 22:21 'Mjue sana Mungu ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia'. 

MUNGU AWABARIKI SANA NA KUKUONGOZA KUMJUA KRISTO YESU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI
 KWA MASWALI ZAIDI PIGA SIMU NUMBER 
+255763371047 AU Email pshibita@gmail.com\pshibita@yahoo.com














Subscribe to receive free email updates: