MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

UKWELI KUHUSU MAMBO YAJAYO.

Image result for ujumbe wa malaika watatu
MAMBO YAJAYO KWA UWAZI Kwa miaka michache iliyopita, dunia imenshuhudia tukio moja baada ya lingine. Ukame, mafuriko, vimbunga vya kuharibu, mitetemeko ya ardhi, yote yamefanyika yakifuatana kwa karibu sana. Maelfu walipoteza maisha yao katika ajali mbali kwenye nchi kavu, majini na hewani; ilhali wengine mamilioni wakifa njaa, mataifa mengi yamefilisika, wasiweze kulipa madeni yao. Vita, migomo, mpasuko wa idadi ya watu duniani, kuharibiwa kwa mazingira, yanamfanya mwanadamu kuutazama wakati ujao kwa uoga mno. Mengi ya matukio haya yametabiriwa katika Biblia (Math. 24:4-31, Lk. 21:25-28, Ufunuo 6:12-17, 16, 17, 18). Kila wakati, Mungu ameionya dunia kuhusu hukumu ijao kwa sababu ya uasi wetu (Isaya 24:5-20, 46:9-10, Am. 3:7, Ufunuo 1:1

FUNZO KUTOKA MATUKIO YA ZAMANI Kwa mfano, Mungu alimuonya Nuhu kuhusu mafuriko, Abraham na Lutu kuhusu uharibifu wa Sodoma na Gomora na Musa kuhusu mapigo ya Misri. Matukio haya yameandikwa kutuonya sisi ili tupate kuelewa ya kwamba unabii wa Biblia umetimia au utatimia (1 Wakor. 10:6-12, 2 Petro 2:5-9, Waebrania 4:11). Kwa hivyo, tunapata onyo la Mungu kwa kizazi cha mwisho jinsi unayowakilishwa katika

Image result for ujumbe wa malaika watatu
ambao tunaupata katika Ufunuo 14 jinsi alivyoandika Yohana.
Huu ni mwito wa mwisho kwa watu wote ambao unatolewa na Mungu kabla ya kurudi kwa Kristo kama Mfalme na Hakimu. Ujumbe huu unalo onyo la muhimu sana kuhusu hukumu katika Biblia: (1) “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na chemchemi za maji.” (2) “Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.” (3) “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo wa ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele za malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana na usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake” Ufunuo 14:6-11. Onyo hili ni la muhimu sana kwa kila mtu! Lakini tutaepukaje kumsujudu mnyama na sanamu yake au kuipokea chapa yake ikiwa hatujui ni nini maana ya mnyama na sanamu yake? Kukosa ufahamu katika jambo hili kuna matokeo ya kifo. ,,Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” Hos. 4:5 (Isaya 29:13-14). Hata hivyo, Mungu ameahidi hekima kwa wenye haki (Meth. 2:1-7, Dan. 12:4,10, Math. 7:7-8).

Kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, sikufurahii kufa kwake mtu muovu; aghairi mtu muovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?” Ez. 33:11 (Linganisha 2 Petro 3:10- 11, Mal. 3:18, 4:1-2). Ni nini maana ya mnyama na alama yake? Kabla ya kumjadili mnyama, lazima tuelewe historia iliyomtangulia huyu mnyama. Pahali pazuri pa kuanzia ni katika kitabu cha Daniel, ambacho kinashughulikia unabii, kuanzia karne ya sita kabla hajazaliwa Yesu hadi wakati wa leo. Kutafsiri mfano katika Biblia hautegemei ujuzi wa mtu. Unabii ni historia iliyoandikwa kabla yake kutendeka. Biblia yenyewe inatupatia mwelekeo na ufahamu (2 Pet. 1:20). Mnyama katika unabii anawakilisha mfalme au ufalme. Jambo hili ni dhahiri katika Dan. 7:17,23: “Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani... Huyo mnyama atakuwa wa nne juu ya dunia.” Katika Dan. 7:3 imeandikwa: “Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini...“ “Bahari” au “maji” huwakilisha ,,jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Ufunuo 17:15 (Isaya 8:7). Katika Dan. 7 nabii anaziona falme za dunia zikiwakilishwa na “Wanyama” Maelezo sawa na hayo tunayapata katika Dan. 2:27-45 ambapo kila kiungo kinaeleza mwelekeo wa mwanadamu katika siku za usoni.

Image result for SANAMU YA NEBUKADNEZA

PICHA KUONESHA WANYAMA WANNE KATIKA DANIEL 7
Image result for daniel 7 explained

Image result for daniel 7 explained
“Wa Kwanza alikuwa kama simba...“ Dan. 7:4 (Dan. 2:37-38). Simba anawakilisha ufalme wa Babeli uliotawala dunia miaka ya 608- 538 kabla Yesu kuzaliwa, utawala wa pekee siku za Danieli. Sanamu ya Simba mwenye mabawa imehifadhiwa katika jumba la hifadhi la Pergamon mjini Berlin, Ujerumani.

 DUBU

 “Na tazama, mnyama mwingine, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyu hivi; inuka ule nyama tele.” Dan. 7:5. Mnyama huyu ni sawa na maelezo ya mikono na kifua cha shaba cha Dan. 2:32,39. Mnyama huyu anawakilisha falme mbili za waamedi na waajemi waliotawala baada ya Babeli miaka ya 538-331 kabla ya kuzaliwa Yesu. Waamedi ndio waliotangulia kutawala kisha badaaye Waajemi. Mikono miwili katika Dan. 2 na kuinuliwa upande mmoja katika Dan. 7, ni maelezo yanayotilia mkazo unabii huu. Upande mmoja ulikuwa na nguvu kuliko mwingine. Mbavu tatu zinawakilisha mataifa matatu ya Babeli, Lydia na Misri yaliyopigwa na
Waamedi na Waajemi
.
 CHUI “

Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama Chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.” Dan. 7:6. Mnyama huyu ni sawa na yule wa Dan. 2:32,39. Ulikuwa ufalme wa Wayunani ukiongozwa na Alexander uliowaangusha Waajemi na kutawala
miaka ya 331-168 kabla ya Yesu kuzaliwa. Alexander alipokufa, ufalme wake uligawanyika katika sehemu nne (Falme za Diadoki) zinazowakilishwa na vichwa vinne. Sehemu hizi zilikuwa Macedonia, Thrace, Syria na Misri
.
 MNYAMA WA NNE “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi” Dan. 7:7. Mnyama huyu ni sawa na yule wa Dan. 2:33,40,41. Ufalme huu wa nne uliokuja baada wa ule wa waunani ni ufalme wa Rumi uliotawala kuanzia mwaka wa 168 kabla ya kuzaliwa Yesu, hadi 476 baada ya kuzaliwa. Mnyama huyu alikuwa tofauti sana na wale waliomtangulia hivi kwamba Danieli alishindwa kueleza mfano wake. Katika ufalme huo wataondoka “wafalme kumi” ni katika Dan. 7:24 inawakilisha “wafalme kumi watakaotokea katika ufalme huu”. Historia inaweka wazi kwamba ufalme wa Rumi uliangushwa mwaka wa 476 baada ya kuzaliwa Yesu, na uligawanyika katika falme kumi ambazo ni mataifa kumi ya Uropa ya leo. Falme hizi kumi za Dan. 7:7 ni sawa na vidole kumi vya Dan. 2:42-44. Mataifa haya ni: (1) Ujerumani, (2) Ufaransa, (3) Uingereza, (4) Uswizi, (5) Uispania, (6) Ureno, (7) Utaliano; (8) Heruli, (9) Vandals, (10) Ostrogoths. PEMBE NDOGO “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.” Dan. 7:8 Alama tofauti za kutambua pembe ndogo: 1. Alizuka kati ya zile pembe (falme) kumi, na wakati alipoinuka kutawala, pembe tatu zilingolewa na akachukua nafasi yao. 2. Katika Dan. 7:24 tunaambiwa pembe ndogo inazuka baada ya zile kumi. Katika historia yote ni ufalme mmoja tu unaotimiza masharti haya katika Rumi yenyewe mwaka wa 476 baada ya kuzaliwa Yesu, Upapa, serikali ilioongozwa na mtu mmoja chini ya kanisa katoliki; ulisimamishwa. Katika kuinuliwa kwake, falme tatu za Haruli, Vandals na Ostrogoths “ziliangushwa”. Kwa amri ya Justinian (Codex Justinianus), mfalme wa Rumi ya mashariki, katika mwaka wa 533 baada ya kuzaliwa kwake Yesu. Askofu wa Roma alifanywa kuwa kiongozi wa makanisa yote ya ukristo (Ostrogoths) ndiyo waliokuwa wapingamizi wa mwisho kung’olewa kabisa mwaka wa 538 na kufukuzwa kutoka Rumi na Jemerali Balisarius. Mwaka huo ndipo Rumi ya upapa ilidhibitishwa kuwa serikali kwa wakati uliotabiriwa (angalia maelezo baadaye). 3. Katika Dan. 7:25 tunasoma “naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu”, maana yake ni mateso makubwa ya wakristo. Yeyote aliye na ufahamu katika historia, atafahamu ya kwamba maelezo haya yanaulenga Upapa. Mateso makali dhidi ya wakristo wakati wa zama za giza (Kuwahoji watu kuhusu imani yao, kuwachoma wazushi, vita vya kidini) haya yote yanajulikana na yamo katika kurasa za historia.
  PICHA  KUONESHA PEMBE NDOGO.
Image result for daniel 7 explained


4. Tunazidi kusoma: “ataazimu kubadili majira na sheria...“ Ni dhahiri ya kwamba Upapa umebadilisha amri kumi za Mungu. Katika Katakisimu ya Katoliki, utawala wa Upapa umebadilisha sheria ya pili inayopiga marufuku uabudu sanamu. Pia, Upapa umebadilisha sheria ya nne, ya utunzaji wa Sabato, iliyo sheria ya pekee kuhusu “Wakati”, kwa kuifanya Jumapili siku ya kwanza ya juma, kuwa siku ya kupumzika badala ya siku ya saba ya juma (2 Wathes. 2:3-4, Zab. 94:20). Walibadilisha “wakati” wa kuabudu. Wakaanzisha siku ya kuabudu isiyo ya kweli; badala ya siku ya Saba ya juma, Sabato isiyobadilika tangu mwanzo (Kut. 20:8-11; 31:13,16-17, Eze. 20:12, Isaya 56:2-3,6-7; Zab. 89:35, Waeb. 4:1-11, Yak. 2:10), ilyotunzwa na Kristo pamoja na Mitume (Lk. 4:16, Math. 24:20, Matendo 13:42, Waeb. 4:10-11). Siku ya kwanza ya juma (siku ya Jua), siku ya kuabudu jua, ikaanzishwa, kinyume kabisa na amri ya Mungu. Mungu tayari alikuwa amewaonya watu wake wasije wakaikubali hii siku bandia ya ibaada (Ufunuo 14:9-11, 16:2, 19:20, angalia Eze. 8:16-18). 5. “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu ya makufuru. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana Jina Lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.” Ufunuo 13:5-6, Dan. 7:8,25, Dan. 8:25, 2 Wathes. 2:3-4. Je, makufuru yanatafsiriwa vipi katika Biblia? Wakati mmoja Kristo akitafutiwa makosa, wayahudi walisema ya kwamba amekufuru, “kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya u Mungu” Yoh. 10:33. Aina nyingine ya makufuru Lk. 5:21: “Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu pekee yake?” Aina haya ya makufuru mawili yanalenga upapa (“Hapa duniani tunashikilia nafasi ya Mungu Mwenyezi”, Encyc. Papa Leo wa kumi na tatu tarehe, 20-6-1894). Mara kwa mara papa huitwa “Baba Mtakatifu” hata ingawa Yesu alisema mtu yeyote asiitwe jina hili (Math. 23:9). Kwa sababu jina hili ni la Baba yetu aliye juu mbinguni pekee yake. Yoh. 17:11. 6. Katika Dan. 7:25, 12:7 na Ufunuo 12:14, kutawala kwa upapa kunatafsiriwa kuwa nyakati tatu na nusu wakati, Ufunuo 11:2, 13:5 kama miezi arobaini na miwili Ufunuo 11:3, 12:6 kama siku elfu na mia mbili na sitini.


Tafsiri ya Biblia inayoeleza siku moja = mwaka mmoja (Eze. 4:6, Hes. 14:34) ni dhahiri ya kwamba mafungu haya yote yanamaanisha miaka 1260. Wakati mmoja ni sawa na mwaka mmoja. Nyakati za zamani walihesabu mwaka mmoja kuwa siku 360. Mwezi mmoja unazo siku thelathini (Mwanzo 7:11,24, Mwanzo 8:4), kuna siku 150 ambazo ni sawa na miezi 3 ½ x miezi 12 = miezi 42, na miezi 42 x siku 30 = siku 1260, au miaka halisi 1260 katika historia. Tunafahamu kwamba muda uliyotabiriwa ulitimizwa kwa usahihi katika historia ya upapa. Kuharibiwa kabisa kwa Ostrogoths mashariki mwa ufalme wa kirumi mwaka wa 538 baada ya kuzaliwa kwa Yesu (ambao waliokuwa wa mwisho kupinga utawala wa Kirumi), unaeleweka kuwa ndio mwanzo wa utawala wa Upapa. Tukianza kuhesabu miaka 1260 kwanzia 538, tunafika mwaka wa 1798. Katika mwaka huu, Pope Pius wa sita alichukuliwa mateka na mfaranza Jenerali Berthier baada ya vita vikuu vya Ufaransa. Ukatimia unabii wa: “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka” Ufunuo 13:10. Tangu mwaka huo, upapa haujawahi kupata nguvu sawa na zile za awali. Katiba ya kidemokrasia iliwekwa, na Rumi ikawa nchi huru, nguvu za kisiasa za Rumi zikafika mwisho, ikatimia miaka 1260 sawa na ilivyotabiriwa katika Biblia. Katika Ufunuo 13:1-10 historia inaeleza jinsi nguvu za Upapa zilipoanza kutoka katika ufalme wa Rumi ya kishenzi, jinzi ulivyotawala miaka 1260, na jinzi ulivyopata jeraha la mauti.

jabia mnyama yule.” Hii ni dhahiri kwamba utawala huu utakuwepo hadi Kristo atakaporudi (Tazama Dan. 7:21-22). 8. Wakati wa jeraha la mauti na kurejeshewa nguvu zake, mnyama mwingine anatokea: “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.” Ufunuo 13:11-12. Je, ni utawala upi unaoelezwa? Ni taifa moja duniani linalotimiza masharti haya – Marekani – mataifa mbali mbali yalishikana na kuwa taifa moja miaka ya 1763-1800. Katika Ufunuo 13:11-18, anaanza akiwa mpole lakini anamalizia kutawala dunia yote. Imetabiriwa kwamba Marekani itamfanyia mnyama sanamu ambayo itawafanya wanadamu wote Kumsujudia yule mnyama ambaye jeraha lake lilipona. Sanamu hii ni sawa na utawala wa upapa kwa miaka 1260. Maelezo ya ibaada hii yanaonyesha utawala wa kidini na kisiasa unaoshirikiana. Katika Dan. 3:5,10,14,18,28 tunajifunza kuwa ibaada ya sanamu za watu na aina zingine sawa na hizo, ni kuabudu sanamu kinyume na amri ya Pili (Kut. 20:4-6). Ibaada ya Jumapili ni ishara ya nguvu, alama ya mamlaka ya upapa, kujiwekea sheria zao wenyewe (wao wenyewe wanakiri ya kuwa sheria hizi ni zao wala si za Mungu!). Unabii unaeleza kwamba Marikani itaweka sheria ya kuabudu Jumapili, (“alama ya mnyama”) kwa kusimamisha “sanamu”. Sanamu hii ni Uprotestanti ulioasi, mkusanyiko wa makanisa, utakaoshirikiana na serikali kuweka sheria za kidini. Dunia yote tayari inatambua kuwa Jumapili ndio siku ya kupumzika (soma kitabu kiitwacho Vita Kuu - “The Great Controversy”). Ni ujeuri wa Upapa kudhani ya kuwa wanaweza kubadilisha sheria kumi, amri za Mungu. Hili ndilo litakalo kuwa swala la muhimu hivi karibuni, uamuzi wa kufa na kupona (Ufunuo 13:14-15): Kumtii Mungu au amri za watu (Mal. 3:18, 4:1, Ufunuo 16:2). Ufahamu ya kuwa wakati huu, Marekani itafanya “ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu” (Wazia bomu ya mwaka wa 1945 ya Hiroshima, makombora ya hewani ya Iraq, au mwamusho wa kiroho ulio na mwanzo wake kule Marekani.) “...Naye awakoshesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kufanya mbele ya huyo mnyama.” (soma pia Math. 24:24) “...akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, (Upapa) aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi” Ufunuo 13:13-14. Upapa unadai kwamba tendo la kuibadilisha Sabato hadi siku ya kwanza ya juma ni lao na ni “alama” ya mamlaka yake katika mambo ya kidini (Linganisha Dan. 7:25): “Jumapili ilianzishwa na wakatoliki na unaweza kutetea utakatifu wake kwa misingi ya kikatoliki pekee... Katika Biblia kwanzia Mwanzo hadi Ufunuo, hakuna fungu hata moja linaloidhinisha kubadilishwa kwa Sabato kutoka siku ya saba ya juma hadi siku ya kwanza.” (Catholic Press, Sidney, mnamo tarehe 25-8-1900). “Tunaidhinisha Jumapili  badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa la katoliki lilitoa utakatifu kutoka Jumamosi hadi Jumapili katika mkutano wa Laodekia mnamo mwaka wa 364 AD.” (“The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine” kutoka kwa P. Geiermann, kazi ya Papa Pius wa kumi, tarehe 25-1- 1910 aliyepokea Baraka ya mitume). “Kanisa la Mungu lilifurahia kubadilisha sherehe kutoka siku ya Sabato hadi siku ya Jumapili.” (Chapisho la katekisimu ya Roma Kurasa wa 247 baada ya uamuzi wa kusanyiko la Trent kwa amri ya Papa Pius wa Tano). “Sabato, ambayo ni siku ya saba ya juma ilitunzwa na Kristo na mitume na ilisherehekewa na wakristo wa zama hizo na ilisalia vivyo hivyo hadi ilipobadilishwa katika Mkutano wa Laodekia. Kwanza kabisa, mkutano huu ulijadili swala la siku ya Bwana kisha baadaye wakawazuia watu wasipumzike katika siku ya saba ya Juma, na kwamba atakayefanya hivyo atalaaniwa.” (William Prynne, Mkufunzi maarufu Mwingreza wa mambo ya kidini kutoka kwa kazi yake ya “Dissertation on Lord’s Day”, ukurasa wa 32). “Sabato, siku inayojulikana katika amri, ilibadilishwa na kuitwa siku ya Bwana. Neno hili halijabadilika kwa mujibu wa maneno ya Yesu (Kwa sababu anasema mwenyewe kuwa hakuja kubadilisha sheria, bali kuitimiza) bali kwa ajili ya mamlaka ya kanisa, sheria hii imebadilika.” (Askofu Mkuu wa Rheggio, mahubiri ya tarehe 18-1-1562, Mansi XXIII, ukurasa wa 526). “Ni kanisa katoliki lililobadilisha siku ya kupumzika kutoka Jumamosi hadi Jumapili siku ya kwanza ya Juma... Je, dunia yote inatii mamlaka ya kanisa lipi? Waprotestanti wanadai ya kwamba wanatii Biblia ilhali kwa kuitunza siku ya Jumapili, wanatii sheria ya kanisa Katoliki. Biblia inasema, “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase”, lakini kanisa katoliki linasema, “La, uitunze na kuitakasa siku ya kwanza ya Juma” na dunia yote inatii mamlaka ya kikatoliki!” (Papa Enright tarehe 15-12-1889). “Ni dhahiri kuwa kanisa katoliki linadai kuwa ni wao waliofanya [kutoka Jumamosi hadi Jumapili] mabadiliko... na kwamba kitendo hicho ni alama ya mamlaka yao ya kidini.” (H.F. Thomas, Katibu Mkuu wa Kadinali Gibbons, mnamo tarehe 2-10-1895). 9. Katika Ufunuo 13:18, tunapata ishara nyingine, hesabu ya mnyama. “Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.” Moja wapo wa majina rasmi ya papa ni “Vicarius Filii Dei”. Tafsiri yake ni, “Mwakilishi wa Mwana wa Mungu”. Katika kuwajibu maswali wasomaji wa jarida la kikatoliki liitwalo “Our Sunday Visitor”, la tarehe 18- 4-1915, tunasoma: “Majina yaliopo katika kofia ya Papa ni haya, ‘Vicarius Filli Dei’.” Jina hili (ambalo ni makufuru) tiazama hapo chini hayo makufuru

Image result for pope's title in latinImage result for pope's title in latinImage result for pope's title in latin

furu, kwa sababu linajiinua juu ya Roho Mtakatifu (Yoh. 16:12-15, 14:26, Warumi 8:26) ilhali tunafahamu kuwa mwakilishi wa Yesu hapa duniani ni “Roho Mtakatifu”) ndilo jina la Mnyama (aya ya 17). Kwa mujibu wa aya ya 17 na 18, tunapata nambari ya jina lake, 666. Katika kilatini baadhi ya herufi zinaweza kuhesabika. Huu ndiyo unabii unaotuonyesha ni nani “Mpinga Kristo” (linganisha 2 Wathes. 2:3-12, 1 Yoh. 4:3, 2 Yoh. 7, Warumi 8:3). Katika lugha ya Kigiriki, neno “Mpinga Kristo” linamaanisha “mtu ajiwekaye katika nafasi ya Masihi wa Bwana (anti – badala ya, crio - kutiwa mafuta)”. (Tafsiri halisi ya Agano Jipya, Kurasa ya 371). Kwa hivyo “Mpinga Kristo” ndiye anayedai kuwa mwakilishi wa Kristo – hivi ndivyo anavyodai Papa! Ikiwa Papa angelijitambulisha katika lugha ya agano jipya angalisema hivi: “Mimi ndimi Mpinga Kristo!

” KUMBUKA SAA YA WOKOVU NI SASA NA SIYO BAADAE MUNGU AWABARIKI SANA.

MWENDELEZO WAHABARI HII ITAENDELA WAKATI UJAO



Subscribe to receive free email updates: