MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

JE! WAJUA MUNGU ALIVYOIPENDELEA TANZANIA.

Bonde la Ziwa Victoria na maelezo yake kwa ufupi


Bonde la Ziwa Victoria ndani yake kuna Ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa kuliko yote Barani Afrika na chanzo cha mto  White Nile. Ziwa Victoria lipo katika Latitudi 031 Kaskazini na 354 Kusini, na Longitudi 3118 Mashariki na 3454 Magharibi.

Image result for ziwa victoria
Lina wastani wa kina cha mita 80. Ziwa hili linajumuisha nchi 3 ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda. Mito ambayo inamwaga maji Ziwa Victoria ni pamoja na Mto Kagera, Simiyu, Mbarageti, Gurumeti, Mara na Mori. Upande wa Mashariki wa bonde hasa katika miinuko ya Tarime, misimu ya mvua ni miwili, wakati upande wa Kusini wa bonde ambao ni mkoa wa Mwanza kuna msimu wa mvua na kiangazi, na upande wa Magharibi unapata mvua kipindi chote cha mwaka na mvua chache katika mwezi wa saba.
Image result for ziwa victoria
Kiasi cha wastani wa mvua kwa mwaka kinatofautiana katika maeneo mbalimbali ya ziwa na maeneo yanayolizunguka. Upande wa Mashariki wastani wa mvua kwa mwaka ni kati ya 500 na 700mm. Upande wa Magharibi mvua huongezeka hadi kufikia wastani 2000mm katika maeneo ya Bukoba na visiwa vya Ssese. Upande wa kusini mwa ziwa katika maeneo ya Mwanza wastani wa mvua ni kati ya 750-1100mm na upande wa Mashariki katika maeneo ya Mara wastani wa mvua kwa mwaka ni kati ya 750-1000mm na huongezeka hadi 1600mm katika miinuko ya Tarime.
Image result for ziwa victoria


ZITAMBUE MBUGA KUU TANZANIA NA UZURI WAKE.

Tanzania imebarikiwa kwa wanyama wa kila aina. Kuna mbuga kubwa tatu ambazo Tanzania imehifadhi wanyama mwitu. Mbuga hizi ni Mikumi, Manyara na Serengeti. Mbuga hizi zinatunzwa na wafanya kazi wa wizara ya Utalii na Mali Asili,Tanzania. Wageni wengi wanapendelea kuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama na hivyo kujionea fahari yetu katika mbuga hizo. Pia kupitia mbuga hizo husaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato la taifa na hivyo kuendeleza nchi yetu kujisaidia katika huduma zake mbalimbali.

Hifadhi ya Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi mwa Dar ea Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini ya mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar ea Salaam na Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.
Image result for mikumi national park safari



Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.
Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.

Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.

Image result for mikumi national park safari


Hifadhi ya Manyara ni maarufu sana nchini Tanzania kwa simba wanaopanda miti. aina hii ya simba hupatikanandani ya hifadhi hii pekee barani Afrika.
Umaarufu wa hifadhi ya Ziwa manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utalii wa ndani ambapo wananchi wengi kutoka katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania hupenda kutembelea hifadhi hii. Hifadhi hii ipo ndani ya Bonde la Ufa ambalo kingo zake zinaongeza mandhari zaidi.

Image result for mikumi national park safari


Ukweli kuhusu  Hifadhi ya Taifa  ya Serengeti 
Hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti  Kijiografia  inapatikana  katika  Mkoa wa Mara.  Kihistoria  toka  hapo zamani  katika  hifadhi hii ya Serengeti jamii ya Kabila la Wamaasai ambao  ni jamii ya nilotiki  ambayo  kihistoria  asilia  yake  ni  Kusini  mwa  Sudani  iliishi  kwa miaka  mingi  pamoja na Wanyamapori  katika  hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti.
        Ikumbukwe  na ieleweke  ya kwamba  kipindi  cha wakati  huo eneo  hili la Serengeti  ilikuwa  ikihusisha eneo  linalofahamika leo  hii  kama Mamlaka  ya hifadhi ya Ngorongoro ikijulikana  kwa pamoja  kama “Great  Serengeti” kabla ya  eneo  la mamlaka ya hifadhi  ya Ngorongoro  kutenganishwa  mnamo  mwaka  wa 1959 na  kupelekea  jamii  yote ya  kabila la Wamaasai waliokuwa  wakiishi  eneo la Serengeti  kuhamishiwa  katika  Mamlaka ya hifadhi  ya Ngorongoro.
        Asili ya jina Serengeti limetokana na lugha ya Kabila la Wamaasai lenye  kumaanisha  uwanda  mpana.
- See more at: http://www.tazamaramanitanzania.com/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Serengeti.html#sthash.n6mChmIX.dpuf






LIFAHAMU ZIWA RUKWA AMBALO NDILO ZIWA KUBWA LA MAGADI NCHINI TANZANIA


Ziwa Rukwa ni ziwa kubwa la magadi nchini Tanzania. Liko upande wa kusini magharibi ya nchi karibu na Zambia kati ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.
Uenezaji wa ziwa hubadilika mara kwa mara kufuatana na idadi ya mvua inayonyesha katika beseni yake.

Ziwa liko kwa kimo cha mita 800 juu ya UB katika bonde ambalo ni mkono wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Bonde hili ni sehemu ya kusini ya mkono wa magharibi wa bonde hili na mikono yote miwili inaungana huko Mbeya kabla ya kuendelea kwa pamoja katika Ziwa Nyasa.

Beseni ya ziwa line eneo la takriban 80,000 km². Urefu na upana wake hubadilikabadilika kulingana na kiasi cha mvua inayonyesha. Kati ya mito inayoingia ni mto wa Songwe pekee ulio na maji muda wote. Kuna taarifa ya kwamba ziwa lilipotea wakati mwingine isipokuwa beseni ndogo upande wa kusini Songwe inapoingia hubaki na maji. Kama maji ni mengi ziwa lina urefu wa kilomita 180.

Eneo la ziwa ni kavu sana na maji yake ni ya magadi. Kwa hiyo hakuna vijiji mbali na mito hasa upande wa kusini. Majirani ni hasa Wafipa na Wasafwa.
Pamoja na maanzari mazuri Ziwa Rukwa upande wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya linatarajiwa kila mwaka kufungwa kwa miezi sita kwa lengo la kutoa fursa kwa samaki kuzaliana na kukua.

Kwa mujibu wa uongozi wa Wilaya ya Chunya Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kufuatia kasi ya kutoweka kwa samaki katika ziwa hilo  ambapo hivi sasa wavuvi wanavua samaki wachanga mfano wa dagaa ambao hawafai kwa kitoweo.

Ziwa Rukwa tangu uhuru limetoa ajira katika sekta ya uvuvi ambapo wavuvi wameweza kusomesha watoto wao,kujipatia kipato kwa kuuza samaki na kupata kitoweo ambacho kinajenga afya kutokana na samaki wanaopatikana kwenye ziwa hilo.

Kutokana na uharibifu wa mazingira katika ziwa Rukwa upande wa wilaya ya Chunya umesababisha mazalia muhimu ya samaki ndani ya ziwa hilo kuharibika kutokana na shughuli za kibinadamu zinazotokana na uingizaji wa mifugo mingi pamoja na uvuvi wa kutumia kokoro ambao umesababisha samaki wengi kutoweka na kubakia samaki wachanga pekee.

Ng'ombe wakiingizwa ndani ya ziwa Rukwa kwa ajili ya malisho na kunywa maji pia wanaharibu mazalia ya samaki ambayo yapo kwenye magugu yanayoota ndani ya ziwa hilo 
KWA UTHIBITISHIO WA MAANDIKO SOMA MWANZO 1 YOTE
    KIPINDI HIKI    KITAENDELEA, MUNGU AWABARIKI SANA
      





Subscribe to receive free email updates: