MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

Ibada yafanywa Urusi kuwakumbuka wahanga wa ajali ya ndege

bada ya kuwakumbuka watu waliokufa katika ajali ya ndege ya Urusi iliyotokea kwenye Rasi ya Sinai, Misri, imefanyika leo kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Isaac huko Saint Petersburg, Urusi
. Nje ya Kanisa hilo, kengele iligonga kwa mara 224, kwa heshima ya watu waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, wengi wao wakiwa raia wa Urusi. Ibada hiyo imeonyeshwa moja kwa moja katika televisheni ya taifa, huku picha za wahanga zikionyeshwa sambamba na kila mlio wa kengele. Wakati huo huo, wataalamu wa masuala ya anga wanaochunguza chanzo cha ajali hiyo ya ndege wamesema leo kuwa wana uhakika wa asilimia 90 kwamba mlio uliosikika katika kisanduku cha kurekodi sauti ndani ya chumba cha rubani, sekunde ya mwisho kabla ya kuanguka, ni mlipuko uliosababishwa na bomu. Wamesema uchunguzi uliofanywa hadi sasa katika kisanduku cheusi cha kurekodia mawasiliano ya ndege, unaonyesha kuwa ni bomu.

Subscribe to receive free email updates: