Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis ameahidi kuendelea na mageuzi ya Kanisa hilo, licha ya kuvuja kwa nyaraka muhimu za kanisa hilo, zinazoelezea hasira zake kuhusu matumizi
mabaya ya fedha ya makao makuu ya Kanisa Katoliki-Vatican. Akizungumza leo mbele ya maelfu ya watu katika uwanja wa Mtakatifu Petro, amewataka kutoyumbishwa na kuvuja kwa nyaraka hizo za siri. Papa amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwa wajumbe wawili wa tume iliyoundwa na Papa Francis, ya kufanya mageuzi katika mfumo wa kifedha wa Kanisa hilo. Watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuvujisha nyaraka hizo kwa waandishi wa habari wanaofanya uchunguzi wa masuala ya rushwa ndani ya Vatican. Papa amesema kuchapishwa kwa nyaraka hizo ni kosa na kwamba ni kitendo cha kusikitisha ambacho hakina tija.