MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

SAFARI NA MSAFIRI . . . ..sehemu ya kwanza........

Neno safari, Safari maana yake ni matembezi ya ardhini, mara nyingi ni hutumika kwa watalii wanaotembea kuja Afrika, lakini neno hili limetokana na lugha ya kiarabu likiwa na maana hiyo hiyo. Hata hivyo kumekuwa na safri nyingi sana ambazo zinatumia aina mbalimbali ya usafiri kama vile usafiri wa moto na ambao siyo wa moto,wengine pia wamekuwa wakitumia usafiri usio onekana kwa macho ya nyama huo wote ni aina ya usafiri ambao mwanadamu hutumia ili kufanikisha mambo yake au mahitaji yake ya kila siku. Leo ninakuletea aina mpya ya SAFARI NA MSAFIRI katika misha ya mwanadam, safari hii nisafari ya KIROHO, Tangu ADAMU na HAWA kuumbwa hadi sasa yaani tangu mwanzo wa wazazi wetu wa kwanza kuumbwa hadi leo ni takribani miaka 6000 iliyopita mwanadamu amekuwa mkimbizi katika inchi yake aliyo pewa na MUNGU yaani Bustani ya Edeni, Lakini hakuishia hapo tu bali ndani ya hiyo Edeni upande wa mashariki alitengeneza bustani nzuri sana, ambayo inajulikana na wengi kama bustani ya Edeni. Bustani hii ndiyo Mungu aliyomweka mwanadamu wa kwanza hapo aishi (yaani Adamu na uzao wake.) Lakini kama tunavyosoma biblia, wazazi wetu wa kwanza walipoasi, walifukuzwa kutoka katika bustani ile, na kuanzia hapo,mwanadamu akwa mkimbizi kwa kufukuzwa na MUNGU baada ya uasi walioufanya Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
Hivyo MUNGU AKAWEKA MPANGO WA UKOMBOZI ilikumrejesha huyu mwanadamu ambaye tayari alikuwa amekuwa mkimbizi, {Yohana 3:16-17 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.} SWALI MPANGO WA UKOMBOZI AU WOKOVU NINI? Mpango wa wokovu * ni mpango wa furaha wa Mungu kwa Watoto Wake. Kiini chake ni Upatanisho wa Yesu Kristo. Ikiwa utafuata mafundisho ya Yesu Kristo, utapata amani ya kudumu ya nafsi katika maisha haya na shangwe ya milele baada ya kifo. Kadri unavyojifunza kuhusu mpango wa wokovu, utapata majibu kwa maswali haya: “Nilitoka wapi?” “Madhumuni yangu ni nini katika maisha?” “Nitaenda wapi baada ya maisha haya?” Ukweli ni kwamba Mpango wa [wokovu] ulitayarishwa tangu uumbaji wa ulimwengu, kupitia Kristo, kwa wote ambao wataamini katika jina lake,

Subscribe to receive free email updates: