Watu wengi,
hasa walio Wakristo wapya, siku nyingine huwa na mashaka moyoni juu ya mambo
mengine katika Biblia ambayo hawawezi kuyaeleza ama kufahamu. Naye Shetani
huyatumia mambo yale kwa kuwapunguzia imani yao katika kukubali kwamba Biblia
ni ufunuo wa Mungu. Wasema,“Nawezaje kujua njia iliyo ya haku ? Kama kweli
Biblia ni Neno la Mungu, nawezaje kuondolewa mashaka haya moyoni, nisi je
kushikwa na fadhaa ?”
Kila jambo
atakalo Mungu tulisadiki, hakosi kutubainishia sababu ya kuwa na imani juu ya
jambo lile. Jinsi Mungu mwenyewe alivyo hai, namna ya tabia zake, na ukweli wa
Neno lake, mambo haya yote yamehakikishwa kwetu kwa namna nyingi. Hata hivyo
Mungu haoni ni afadhali kutuondolea nafasi ya kuwa na shaka. Imetupasa
kumwamini Mungu kwa vile tunavyobainishiwa mioyoni mwetu juu ya mambo
yasiyoonekena, siyo kwa ajili ya mambo yaliyo dhahiri katika macho yetu ya
kibinadamu.
Haiyamkiniki
kwa nia ya kibinadamu kufahamu kabisa namna za tabia za Mungu wala kazi yake.
“Kwa kutafuta utampata Mungu ? Utampata Mwonyiozi Mungu alivyo bora ? Juu kama
mbingu; utafanyaje ? Chini kupita ahera; utajuaje ?” Ayub 11:7,8.
Mtume Paulo
alisema, “Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hata kiasi!
hukumu zake hazichunguziki na njia zake hazitafutikani” Warumi 11:53. Na hata
“mawingu na giza yamemzunguka,” “haki na hukumu maweko ya kiti chake.”
Zab.97:2. Katika matendo yake juu yetu twaweza kufahamu makusudi yake kutosha
kuona upendo Wake na huruma yake isiyo na kiasi, na jinsi uwezo wake usivyo
cheo. Twaweza kutambua makusudi yake kwa kadiri inavyotufaa; zaidi ya hayo
imetulazimu kutawakali Mwenyiezi Mungu, ambayo moyo wake umejaa upendo.
Katika Neno
la Mungu, vilevile katika sifa yake, kuna mambo ya siri wasiyoweza wanadamu
kuyafahamu. Jinsi dhambi ilivyoingia ulimwenguni, jinsi Kristo alivyofanyika
kuwa na umbo halisi la binadamu, uzazi wa pili jinsi ulivyo, ufufuo, na
mengineyo katika Biblia, ni mafumbo makubwa sana kushinda akiii za kibinadamu
kuyaeleza, wala kuyafahamu maana yake vizuri. Lakini hatuna sababu ya kuwa na
shaka juu ya Neno la Mungu kwa ajili ya kutofahamu mafumbo ya maongozi yake na
majaliwa yake Mungu. Hata katika mambo ya ulimwengu na viumbe vyake twaona
mafumbo mengi tusiyowoza kuyafahamu. Wenye akili sana wameshindwa kueleza
habari za uhai jinsi ulivyo, hata uhai wa vidudu vidogo. Mahali pote pana
maajabu tusiyoweza kuyafahamu. Kwa hivyo mbona tunastaajabu tukiambiwa kuwa
kuna mambo ya kiroho yasiyoweza kufahamiwa na kuelewa na binadamu ? Shida
imekuwa kwa ajili ya udhaifu na akili chache ya binadamu. Katika Maandiko
yenyewe Mungu ametuhakikishia jinsi Maandiko haya yalivyo ya Mungu, tusione
shaka moyoni juu ya Neno lake kwa sababu ya kutofahamu mafumbo yake yote.
Mtume Petro
amesema kwamba katika Maandiko “yamo mambo ambayo ni vigumu kurlewa nayo; na
mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa....kwa upotevu wao
wenyewe.” 2 Pet.3:16. Wengine husema kwamba mafumbo ya Biblia ni sababu ya
kutosadiki maneno yake; lakini kwa kweli mafumbo haya ni ushahidi mkuu kuwa
yametoka kwa Mungu. Kama ingekuwa Biblia haina habari za Mungu ila tu mambo
yawezayo kuelewa kwa urahisi na kufahamiwa na binadamu, Biblia isingekuwa na
hakika kwamba ni ya Mungu kweli.
Mafundisho
ya Biblia juu ya wokofu, yametolewa kwa namna ifaayo kwa mahitaji na matakwa ya
moyo wa binadamu; watu wastaarabu na wenye elimu nyingi wamevutwa na uzuri wa
maneno yake; na hata watu duni waweza kuolowa na kufahamu njia ya wokofu.Hata
hivyo twaweza kuyasadiki hivi tu, kwa kuwa Mungu ndiye anayetujulisha manbo
hayo. Mpango wa Mungu juu ya ukombozi wa wanadamu umebainishwa vizuri kwetu,
ili mtu ye yote ajue la kufanya katika kutubia kwa Mungu, na kuwa na imani kwa
Bwana wetu Yesu Kristo, apate kuokoka kwa njia aliyoiweka Mungu. Walakini ndani
ya mambo haya kuna mafumbo ya Mungu yasiyofunuliwa ila kwa yule anayeyachunguza
kwa moyo na bidii. Na kwa jinsi anavyozidi kuyachunguza naneno ya Biblia,
ndivyo anavyozidi kusadikishwa kwamba ni Neno la Mungu aliye hai.
Wenye
kumkana Mungu hutupia mbali Neno la Mungu kwa sababu hawawezi kufahamu nafumbo
yake yote. Hata na wengine wanaojidai kuwa hisadiki Biblia, huona mashaka
moyoni juu ya jambo hilo. Mtume amesoma, “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika
mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
Waeb.3:12. Ni vizuri kujifunza mafundisho ya Biblia, na kuchunguza “hata
mafumbo ya Mungu,” (I Wakor.2:I0), kwa kadiri yanavyofunuliwa katika Maandiko.
Ingawa ni “kwa Bwana Mungu wetu yaliyo ya siri,” ni kwetu sisi
“yaliyofunuliwa.” Kumbu.29:29. Lakini ni kusudi la Shetani kuipotoa njia ya
binadamu kama anataka ku-yachunguza mambo. Kwa ajili ya ufundi wanaojiona kuwa
nao katika kuchunguza mafundisho ya Biblia, watu wengine huwa wepesi wa
kuchukizwa wasipoweza kueleza maana ya kila sehemu ya Maandiko kwa namna ya
kutosheleza nafsi zao wenyewe. Ni aibu kwao kukiri kwamba hawayafahamu vizuri.
Hawataki kumngo jea Mungu hata atakapowafunulia maana ya hakika. Huona kwamba
akili za kibinadamu zimetosha kuwafahamisha Maneno ya Mungu; nao wakishindwa
kufanya hivi, basi, huyakana kuwa si ya Mungu. Kuna maelezo na mafundisho mengi
ya dini yanayodhaniwa tu ya kuwa asili yake ni maneno ya Biblia, lakini maana
yake ni kinyumo kabisa cha ukweli wa Biblia. Kwa ajili ya mambo haye watu wengi
hushikwa na fadhaa na huona shaka mioyoni mwao. Lakini imekuwa hivyo si kwa
ajili ya Neno la Mungu hasa, ila kwa kuwa wanadamu wamepotoa naneno yake.
Kama
wanadamu wangeweza kupata kufahamu Mungu jinsi alivyo hasa, pamoja na natendo
yake, basi, wasingekuwa na jambo jipya la kuvumbua, wasingezidi kuelinishwa
tena, wasingepata kuzidisha maondeleo yao ya kiroho. Hapo Mungu asingekuwa
Mwenye enzi; tena kwa vile ambavyo binadamu angekuwa amefika mwisho wa elimu na
maarifa yote, asingepata maendeleo yo yote tena. Tumshukuru Mungu kwa kuwa
sivyo hivyo. Mungu ni mwenye uwezo wote, mwenye kujua yote; “ndani yake zimo
hazina zote za hekima na maarifa.” Wekor.2:3. Maisha na nilele wanadanu
watakuwa wenachunguza na kuendelea kufahanu akili za Mungu, wema wake, na enzi
yako, bila nwisho.
Kuna njia
moja tu kwa kupata kuelimishwa na kuendelea ku-fahamu Neno la Mungu, - kama
Roho ya Mungu inanglaa mioyoni nwetu na kutumiliki. “Mambo ya Mungu hakuna
ayajuaye ila Roho ya Mungu;” “maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya
Mungu.” 1 Wakor.2:11,10. Tena Mwokozi aliwaahidia wafuasi wake hivi, “Ajapo
yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli;...atatwaa katika
iliye yangu, atawapasheni habari.” Yoh.16:13,14.
Mungu ataka
binadamu atumie akili zake; na kuchunguza na kujifunza Biblia kutaimarisha na
kuadilisha roho na nia zetu kwa jinsi isivyowezekana katika kujifunza nanbo yo
yote mengine. Ili tupate kufahamu Msandike , na mioyo yetu isifadhaishwe
inetupasa kuwa na imani na moyo mmo ja kama watoto, tayari kufundishwa na
kumwomba Roho Mtakatifu msaada wake. Tukiona uwezo wa Mungu na akili zako jinsi
viliyo kuu zaidi pasipo kiasi, na kuelewa hali yetu ya kutoweza kufahanu namna
ya utukufu wake, hapo basi inetupasa kunyenyekea; na tunapofunua kitabu cha
Neno lake, imetupasa kuwa na heshima na unyenyekevu moyoni kama tulio mbelo
yake hasa.
Kuna nanbo
mengi ya fumbo, ambayo Mungu atawadhihirishia wale watakao kweli kuyafahamu.
Lakini bila uongozi wa Roho Mtakatifu binadamu huelekea kupetoa maneno ya
Biblia na kueleza maana isiyo ya kweli. Masomo nengi ya wanadanu katika Biblia
yanekuwa bure bila faida. Kana kitabu cha Neno la Mungu kinafunuliwa bila
heshima na maombi: mtu asipomkazia Mungu fikara zake na upendo wake na kufanya
napenzi ya Mungu, bila shaka atashikwa na fadhaa. Ndipo Shetani atamtawala
mawazo yake, na kumtia moyoni mwake maelezo ya Biblia yasiyo ya kweli. Kila
mara wanadanu wasipopatana na Mungu katika maneno na matendo yao, ingawa ni
wenye naarifa ya namna gani, bila shaka watakosa kufahanu Maandiko, tena haifai
kuwaamini maelezo yao. Wengi wao walio na mashaka moyoni, asili ya kushuku kwao
ni kupenda dhanbi. Masharti na vizuizi vya Neno la Mungu havipendezi wenye moyo
wa kujisifu, na wale wasiokubali kufanya matakwa ya Biblia lake huwa wepesi
kutosadiki kuwa ni Neno la Mungu halisi. Bali, wote watakao kwa noyo kujua
matakwa ya Mungu na kuyafanya, hao nao watabainishiwa kuwa Biblia ni Maneno ya
Mungu yawezayo kuwapa hekima hata wapate wokofu. Kristo asema,“Mtu akipenda
kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu.”
Yoh,7:17. Badala ya kubishana bure juu ya mambo msiyoweza kuyafahamu, heri
mfanye kila wajibu wenu kwa vile mnavyofahamu na kuelewa navyo, ndipo
mtasaidiwa kuyafahamu na kuyafanya yale ambayo sasa mnayaonea mashaka.
Mungu ataka
tujihakikishie ukweli wa Neno lake na ahadi zake. Asema, “Onjeni mwone BWANA
ndiye mwema.” Zab.34:3. Tusitegemee neno la wengine, ila tuonje sisi wenyewe na
kuona wema wake. Asema tena, “Ombeni, na mtapata.” Yoh.16:24. Ahadi zake
zitatimia. Haziwezi kuwa na upungufu. Wa kwa vile tunavyomkaribia Yesu, na
kufurahiwa na upendo wake, ndivyo nuru yako itakavyong aa mioyoni mwetu, tena
mashaka na giza vitaondolewa. Mtume Paulo asema kwamba Mungu alituokoa “na
nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo
lake.” Wakol.1:13. Kila ambaye “amepita toka mauti hata uzima” anawoza kutia
“muhuri yake kwamba Mungu ni kweli.” Yoh.5:24; 3:33. Aweza kushuhudia,“Nimopata
msaada kwake Yesu; nayo ameniruzuku mahitaji yangu yote, nimetoshewa njaa ya
moyo wangu; tena sasa Biblia inakuwa kwangu ufunuo wa Yesu Kristo. Waniuliza
mbona namwamini Yesu ? - Kwa kuwa ni Mwokozi wangu. Kwa nini nasadiki Biblia ?
- Kwa sababu nimeona kuwa ni sauti ya Mungu moyoni mwangu.” Twawoza kuwa na
ushuhuda ndani yetu kuwa neno la Biblia ni kwoli, tena Kristo ni Mwana wa
Mungu. Twajua kwamba hatufuati hadithi zilizotungwa kwa werevu. 2 Petro 1:16.
Petro
awaamuru Wakristo ndugu zake, “Kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wotu,
Mwokozi wetu Yesu Kristo.” 2 Pet.3:l8. Watu wa Mungu wakikaa katika neema yake,
watazidi kudhihirishiwa Neno lake. “Matembezi yao wenye haki kama nuru nyeupe,
iangazayo ikizidi hata mehana utimiapo.” Methali 4:18.
Kwa imani
twaweza kutazama mbole hata kwa ufalme wa Mungu, na kutumaini ahadi ya Mungu
juu ya kutuzidisha akili, na jinsi uwezo wetu woto utakavyoungamana na, uwezo
wa Mungu. Twaweza kufurahi kwa kuwa yoto ambayo sasa tumeshikwa na fadhaa nayo,
hapo ndipo yatadhihirishwa kwetu; mambo yanayokuwa magumu kufahamiwa, wakati
huo yataelezwa dhahiri. “Wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo;
wakati ule uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua
sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.” 1 Wakor.l3:12.
Kumtegemea
Mwokozi, kwangu tamu kabisa:
Kukubali
Neno lake nina raha moyoni,
Kumtegemea
Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kwake daima
napata uzima na amani.
Nafurahi kwa
sababu nimekutegemoa;
Yosu,
Mpendwa na Rafiki, uwe nami daina.
CHUKUA HATUA .