Ndipo Yesu alipoongozwa na Roho mpaka jangwani, ili apate
kujaribiwa na shetani. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, baadaye aliona
njaa.”
Yesu hakujitia majaribuni mwenyewe. Alikwenda jangwani ili
akae peke yake, apate kutafakari juu ya kazi yake Alikuwa akijifikiria na
kujikaza kuhusu njia ngumu ya hatari, ambayo ataiendea. Lakini Shetani alidhani
kuwa huo ndio wakati mzuri wa kumkabili.
Matokeo makubwa yalikuwa hatarini. Shetani alidai kuwa dunia
hii ni mali yake, na yeye mwenyewe hujiita “Mtawala wa ulimwengu.” Husema kuwa
watu wamemchagua awe mtawala wao. Kwa ajili hiyo amepata utawala wa ulimwengu.
Kristo alikuja ili kuyakanusha madai hayo. Kristo atadumu kuwa mwaminifu kwa
Mungu, akiwa katika hali ya binadamu. Hivyo itaonyesha kuwa Shetani hakuutawala
ulimwengu kamili, na madal yake kuwa ni mfalme wa ulimwengu, ni uongo. Wote
wanaotamani kutolewa mikononi mwake watafunguliwa.
Shetani aliiua kuwa hakuutawala ulimwengu kamili. Ulionekana
uwezo katika wanadamu unaoupinga utawala wake. Soma Mwanzo 3:15. Katika kafara
iliyotolewa na Adamu na wazao wake, ilionekana alama ya kuongea kati ya dunia
na mbingu. Shetani alijitia kati kuzuia mawasiliano haya. Alimtaja Mungu vibaya
na kueleza kinyume juu ya mifano iliyokuwa ikimwelekeza mwokozi. Watu
walimwogopa Mungu kama mwenye kufurahia maangamizi yao. Kafara ambazo
zingalionyesha upendo wake, zilipotoshwa na kufanya kuwa kumfurahisha Mungu ili
awahurumie. Sura hii imeandikwa katika Mathayo 4:1-ll; Marko 1:12, 13; Luka
4:1-13, Wakati Neno la Mungu lilipotolewa, Shetani alijifunza unabii. Toka
kizazi mpaka kizazi, alijitahidi kuwapofusha watu ili wamkane Kristo na kuja
kwake.
Wakati wa kuzaliwa kwa Kristo, Shetani alijua kuwa amekuja
atakayepinga utawala wake. Kwamba Mwana wa Mungu angekuja ulimwenguni kama mtu
mwenye uwezo wa kukamata na kuangamiza. Roho yake ya ubinafsi isingeweza
kufahamu upendo huo. Kwa kuwa mwenyewe amekosa kuishi mbinguni, aliazimia
kuwapotosha wengine, ili washiriki ajali yake. Alitaka kuwafanya watu wadharau
mambo ya mbinguni, ila wathamini mambo ya dunia tu.