1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.
2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.
3 Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.
4 Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.
DANIEL 12 :1-4MALAKI 4:1
1 Yesu alitoka Hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake walimwendea, wakamwonyesha majengo ya Hekalu. 2 Yesu akawaambia, “Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.” 3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?” 4 Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu. 5 Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: Mimi ndiye Kristo, nao watawapotosha watu wengi. 6 Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado. 7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi. 8 Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto. 9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu. 10 Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana. 11 Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi. 12 Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia. 13 Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka. 14 Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote. 15 “Basi, mtakapoona Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake), 16 hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani. 17 Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake. 18 Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.19 Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo! 20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato!21 Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.22 Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa
SOMA MATAYO 24:1-22
DALILI ZA DUNIA KUANGAMIA
1. MUUNGANO WA MAKANISA
2.HAKI SAWA
3.UGAIDI ULIMWENGUNI
3;DEMOCRASIA
4. UCHUMI KUDOROLA
5. VITA DHIDI YA MATAIFA
BADILIKO LA HALI YA HEWA ULIMENGUNI
AJARI KWA WAOVU NININI?
MAPIGO SABA YA MWISHO (4-6)
Malaika wa inne akakimimina kitasa chake juu ya jua,nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo, wala hawakutubu wala kumpa utukufu.*pigo la 5*
Na huyu wa tano akakimimina kitasa chake juu ya ya kiti cha enzi cha yule mnyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi za kwa sababu ya maumivu, wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao na kwa sababu ya majipu yao, wala hawakuyatubia matendo yao
*pigo la 6*
Na huyu wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati, maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa ajili ya wafalme watokao katika maawio ya jua.
Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka ktk kinywa cha yule joka, na cha yule mnyama na cha yule nabii wa uongo. hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ili kuu ya Mungu mwenyezi.Ufunuo16:8-14
6.HITIMISHO
Ikiwa wewe na mimi yanatuingia maneno haya tubadilike haraka kabla ya amri ya Jumapili haijatangazwa kule Marekani.
Matukio yanayohusiana na kufungwa kwa mlango wa rehema maandiko yamefunua wazi GC 594. Naam tukijua wakati kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwajia kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuaminiusiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha, za nuru-kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi. Bali mvaeni Bwana Yesu kristo, wala msiangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake Warumi 13;11-14.
Tukijua ya kwamba miaka kadhaa iliyopita dalili zifuatazo zilionekana Msimamo mkubwa ulichukuliwa na chama cha Republican katika kampeni yake ya hivi karibuni wa kushikilia mamlaka ya mwisho ya mahakama kuu katika mambo yote ambayo yatasaidia. Maamuzi kuhusika katika kushikilia. Maamuzi yote ya mahakama hiyo, inaonyesha ni jinsi gani mwelekeo wa chama hicho kinachokaribia kuingia katika madaraka kitakavyokuwa kuhusika na jambo hili la kuwa taifa la kikristo …
Pia ni wazi kwamba Papa, Askofu mkuu wa Ireland na wakatoliki wengine waliokubuhu wamejitangazia wenyewe kuwa upande wa chama cha Republican. Na kwamba katiba, kama inavyotafsiriwa sasa na mahakama kuu, inaaminiwa na wakatoliki kukubaliana na aina ya serikali ya Upapa.
Chama sasa karibu kitaingia katika madarfaka kikiwa na nia ya kuwa na ya serikali ya upapa katika kukubaliana na serikali hiyo ..
Review and Herald Vol. 3 Jan 19, 1897 Page 432.
Pia ni wazi kwamba Papa, Askofu mkuu wa Ireland na wakatoliki wengine waliokubuhu wamejitangazia wenyewe kuwa upande wa chama cha Republican. Na kwamba katiba, kama inavyotafsiriwa sasa na mahakama kuu, inaaminiwa na wakatoliki kukubaliana na aina ya serikali ya Upapa.
Chama sasa karibu kitaingia katika madarfaka kikiwa na nia ya kuwa na ya serikali ya upapa katika kukubaliana na serikali hiyo ..
Review and Herald Vol. 3 Jan 19, 1897 Page 432.
Tukijua kuwa Marekani imeanza kunena kama Joka; kwa sababu sasa hivi Marekani ndiyo taifa pekee lenye nguvu duniani; ni taifa pekee tajiri duniani; ni taifa pekee linaloongoza katika sayansi na teleknolojia katika ulimwengu. Marekani ni taifa pekee lenye mvuto mkubwa ulimwenguni; ndilo taifa pekee ambalo kiongozi wake anazunguka katika ulimwengu kupatanisha mataifa yanayopigana; ni taifa pekee lililopewa jina la polisi wa ulimwengu; ni taifa pekee likitoa kauli ulimwengu unatilia maanani; ni taifa pekee lenye mchango mkubwa katika umoja wa mataifa. Marekani ni kiongozi wa shirika la NATO shirika ambalo likiamua kupiga nchi iliyo kinyume chake unapiga bila kujali umoja wa mataifa unakubali au la! Marekani nchi pekee ambayo katika Bilblia imeatajwa kwa jina kuwa na sehemu kubwa ya kutimiza unabii wa kumaliza historia ya dunia. 5 T 452 maandalio ya amri ya Jumapili sasa yanaendelea gizani. Viongozi wanaficha tatizo halisi, na wengi wanajiunga na mpango huo wa kuandaa amri ya Jumapili hawaoni kama ni jambo lililokusudiwa. Washiriki wake ni wakristo wazuri, itakoponena itafunua roho ya Joka—-
Mwenyezi Mungu atubariki kwa kadri tunavyoendelea kutafakari ujumbe huu mzito unaotufikilia katika miisho hii ya dunia. Na hebu tumwombe Mwenyezi Mungu kutubadilisha udhaifu wetu na kutuwezesha kusonga mbele kuinua bendera ya Mwokozi wetu Yesu Kristo kwa njia ya kupeleka injili ya milele kwa kila mtu haraka kwa kadiri Bwana wetu Yesu Kristo atakavyotuwezesha. Bwana awe nasi sote milele Amina.
SOMO HILI LIMELETWA KWENU NA LAMECK BUGOTA BULULU KWA MASWALI NA MAJIBU PIGA SIMU NUMBER 0787341977/0767341977\0673341977