Sheria
ya Mungu Haibadiliki
“Hekalu
la Mungu lilifunguliwa huko mbinguni, ndipo sanduku la agano lake likaonekana
katika hekalu lake”. Ufunuo 11:19. Sanduku la agano la Mungu jipya liko
mbinguni katika patakatifu mno, chumba cha pili cha patakatifu. Katika huduma
ya hema takatifu duniani, ambayo ilikuwa mfano wa kivuli cha ile ya mbinguni,
chumba hiki kilifunguliwa tu wakati wa siku kuu ile ya upatanisho kwa ajili ya
kutakasa patakatifu. Kwa hiyo upatanisho kwa ajili ya kutakasa patakatifu. Kwa
hiyo tamko lile lisemalo kuwa hekalu la Mungu lilifunguliwa, na kwamba sanduku
la ushuhuda likaonekana, lilikuwa utangulizi wa kuonyesha kuwa patakatifu mno
mbinguni palikuwa tayari kufunguliwa katika chumba cha pili ili Kristo, Kuhani
wetu Mkuu yuko tayari kuingia na kuanza kazi hiyo mwaka 1844. Watu ambao
wangefuatana naye katika huduma hiyo, waliona sanduku la agano lake. Kadiri
walivyojifunza juu ya hekalu waligundua kuwa Kristo anabadili huduma na sasa
anahudumu mbele ya agano la Mungu.
Sanduku
lililokuwa katika hema takatifu hapa duniani lilikuwa na mbao mbili za mawe
ambazo zilikuwa zimeandikwa juu yake sheria ya Mungu. Hekalu la Mungu
lilipofunguliwa huko mbinguni, sanduku la agano lake lililonekana humo. Sheria
hii ilionekana katika patakatifu pa patakatifu iliyonenwa na Mungu na kuandikwa
na kidole cha chanda chake juu ya mbao mbili za mawe.
Wale
walioelewa fundisho hili walifahamu vyema maneno ya Mwokozi yasemayo: “Mpaka
mbingu na nchi zitakapoondoka; yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka”
Mathayo 5:18. Sheria ya Mungu ambayo ndiyo mafunuo ya mapenzi yake, na maelezo
ya tabia yake, itadumu milele na milele.
Katikati
ya mpangilio wa sheria ya Mungu, husimama amri ya Sabato, ambayo ni amri ya
nne. Roho wa Mungu aliwaagizia wanafunzi hao Neno la Mungu, wakaona kuwa
wameipuuzia siku takatifu ya Mungu kwa ujinga wao. Wakaanza kuchunguza sababu
za kushika Jumapili, ambayo ni siku ya kwanza ya juma. Hawakuona mahali popote
panapoeleza kwamba Sabato ya siku ya saba imefutwa, wala kubadilishwa. Walikuwa
wakitafuta kwa bidii kufanya mapenzi ya Mungu; na sasa wamegundua kuwa kushika
sabato ni mojawapo ya mapenzi yake, kwa hiyo wakaishika kwa furaha.
Juhudi
nyingi zilifanyika ili kutafuta imani ya watu wa Marejeo. Hakuna mtu aliyekosa
kuona kuwa fundisho la patakatifu huko mbinguni linahusiana na madai ya Mungu
ya kushika sheria yake pamoja na Sabato. Hii ndiyo ilikuwa siri ya upinzani wa
maandiko yaliyokuwa yakionyesha huduma ya Kristo mbinguni, katika patakatifu pa
huko. Watu walijitahidi kufunga mlango uliofunguliwa na Mungu, na kufungua
mlango uliofungwa na Mungu. Lakini Kristo amefungua mlango wa huduma yake
katika patakatifu pa patakatifu. Amri ya nne yaani ya Sabato ilikuwako kati ya
sheria za Mungu ikitunzwa huko. Wale waliouamini ukweli huo unaohusu uombezi wa
Kristo wa sheria ya Mungu, waligundua kuwa huo ndio ukweli wa ufunuo 14, ambao
ni ukweli wa maonyo ya namna tatu utakaowatayarisha wenyeji wa dunia juu ya
kurudi kwake Yesu. Lile tamko kwamba, “Sasa hukumu yake imekuja ni tangazo la
ujumbe wa kweli ambao hauna budi kuhubiriwa mpaka Kristo atakapokoma kuombea
watu, naye atakuja kuchukua watu wake kwake. Hukumu iliyoanza katika mwaka 1844
lazima iendelee mpaka mambo ya watu wote yaamuliwe, wale waliokufa na walio hai
pia. Itaendelea mpaka mlango wa rehema utakapofungwa kwa binadamu wote.”
Makusudi
watu wawe tayari kusimama hukumuni, ujumbe unawaamuru kwamba, “Mcheni Mungu na
kumtukuza” na “Msujudieni yeye aliyefanya mbingu na nchi na bahari, na
chemichemi za maji” Matokeo ya kuukubali ujumbe huu yamesemwa: “Hapa ndipo
penye subira ya watu washikao amri za Mungu na imani ya Yesu” Ufunuo 14:7-12.
Ili
kujitayarisha kwa hukumu, watu ni lazima wazishike amri za Mungu, ambazo ndiyo
kipimo cha tabia katika hukumu. Paulo asema, “Wote waliokosa wenye sheria,
watahukumiwa kwa sheria … katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za
wanadamu, kwa Kristo Yesu”. “Watendao sheria watahesabiwa haki” Imani ni muhimu
kwa kushika sheria ya Mungu. “Maana pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu”.
Warumi 2:12-16; Waebrania 11:6; Warumi 14:23.
Ujumbe
wa malaika wa kwanza uliwaita watu wamche Mungu na kumtukuza, na kumsujudia
yeye aliye Mwumbaji; wa mbingu na nchi. Kufanya hivyo ni lazima waitii sheria
yake. Bila utii hakuna ibada inayompendeza Mungu. “Huku andiko kumpendeza
Mungu, kwamba tuzishike amri zake” 1 Yoh. 5:3 Mithali 28:9.