Jina kamili: Judas Iscariot
Historia
ya Yuda huonyesha mwisho wa huzuni wa maisha ya mtu ambaye angeheshimiwa katika
kazi ya Mungu. Kama yuda angalikufa kabla ya safari yao ya mwisho ya kwenda
Yerusalemu angalihesabiwa kuwa mtu mashuhuri sana kati ya mitume kumi na
wawili, ambaye angeacha pengo kubwa sana. Chuki ambayo imemfuata katika karne
zote isingekuwako. Lakini tabia yake imedhihirishwa kwa ulimwengu kama onyo kwa
wote wale watakaosaliti dhamana takatifu.
Tangu
siku ile ya karamu nyumbani kwa Simon Yuda alikuwa amepata nafasi ya
kukitafakari kitendo alichokuwa ameagana kukitekeleza, lakini kusudi lake
lilikuwa halijabadilika. Kwa bei ya mtumwa akamuuza bwana wa utukufu.
Yuda
kwa asili alikuwa na tabia ya kupenda fedha sana, lakini siku zote hakuwa
mpotovu kiasi cha kutenda tendo baya kama hili. Aliilea roho ya uchoyo wa fedha
mpaka ikapita upendo wake kwa Kristo. Kwa tendo moja ovu akajitolea mwenyewe
kwa Shetani, kutumiwa katika kiwango cho chote kile kutenda dhambi.
Yuda
alijiunga na wanafunzi wakati watu wengi walipokuwa wakimfuata Kristo.
Alishuhudia matendo makuu ya Kristo ya kuponya watu, na kufukuza pepo wachafu,
na kufufua wafu. Aliyatambua mafundisho ya Yesu kuwa bora zaidi ya yote yale
aliyopata kusikia. alitamani kubadilishwa tabia na alitegemea kuwa hivyo kwa
kujihusisha na Yesu. Mwokozi hamkukataa Yuda, alimpatia nafasi miongoni mwa
wale kumi na wawili na alimjalia uwezo wa kuponya wagonjwa na kuwatoa pepo
wachafu. Lakini Yuda hakujitoa moyo wake kwa Kristo kikamilifu. Hakuacha tamaa
zake za ulimwengu wala kuzipenda fedha. Hakujiweka chini ya mvuto wa mbingu,
bali alijitafutia tabia ya kukosoa na kushutumu.
Yuda
alikuwa na mvuto mkubwa sana kwa wanafunzi wenzake. alijiona sana kutokana na
sifa zake na aliwadharau ndugu zake kama walio duni. Alijisifu kuwa kanisa
lisingestawi kama isingekuwa kwa sababu ya uwezo wake kama msimamizi. Machoni
pake alijiona kuwa muhimu na kila mara alipenda mwonekano huo.
Kristo
alimweka mahali ambapo angeona udhaifu wake na kujirekebisha, lakini Yuda
alijiendeleza katika tamaa. Fedha chache alizokuwa akitunza kila mara zilikuwa
zinamtia majaribuni. alipotenda kazi ndogo kwa ajili ya Kristo, alijilipa
kutoka katika fedha hizo kidogo. Machoni pake hivi visababu vilitumiwa kama
udhuru kwa vitendo vyake, lakini machoni pa Mungu alikuwa mwizi.
Yuda
alichagua njia ambayo alitegemea Kristo aifuate katika kazi, alikuwa amepanga
kuwa yohana Mbatizaji afunguliwe kutoka gerezani. Lakini Yohana aliachwa akatwe
kichwa. Na Yesu, badala ya kulipa kisasi kwa ajili ya kifo cha Yohana aliondoka
kwenda mahali pengine. Yuda alitaka hatua za ukakamavu zaidi zichukuliwe.
Alifikiri kuwa kama Yesu asingaliwazuia wanafunzi kutekeleza mipango yao kazi
ingefanikiwa zaidi. aliona kuwa madai ya viongozi wa kiyahudi hayakupata
changamoto wakati walipodai Kristo atoe ishara kutoka mbinguni. Moyo wake
ulikuwa wazi kufuata hisia za kutoamini na adui akaujaza uasi. Kwa nini Yesu
alitabiri mateso na mashataka dhidi yake mwenyewe na kwa wanafunzi wake?
Matumaini yake ya kupata cheo kikuu katika ufalme ujao yakatishwe tamaa?
KUMBUKA HILI MAAMUZI YAKO YA LEO NDIO MATOKEO YAKO BAADAYE.