Kimsingi kabla hujasoma
au kujifunza BIBLIA TAKATIFU ni mhimu kwanza kujuwa yafuatayo
1. KUOMBA MUNGU AMBAYE
NI MWALIMU MKUU AKUFUNDISHE.
2.KUONDOA MITAZAMO
BINAFISI YA KIMSIMAMO YA KIITIKADI.
3.KAMA HUJUI MWNZO WA
KITU NI VIGUMI PIA KUJUA MWISHO
WAKE NA HATIMA YAKE.
Sabato ilitukuzwa tangu kuumbwa kwa dunia, kama jinsi ilivyo wekwa
kwaajiri ya wtu,mwanza wake ni “wakati
nyota za mbinguni zilipo imba pamoja na wana wa MUNGU waliposhangilia kwa
furaha Ayubu38:7.
Waisrael
walijua Sabato kabla ya kufika Sinai. Njiani huko Sabato ilitunzwa. Sabato
ilipovunjwa, Bwana alisema: “Mtakataa kushika sheria mpaka lini?” Kutoka 16:28.
Sabato haikutolewa kwa ajili ya Waisraeli tu, bali kwa watu wote wa ulimwengu.
Kama sheria yote ya amri kumi ilivyo, haibadiliki wala kufutika. Kristo alisema
kuhusu sheria hiyo. “Mpaka mbingu na nchi zitakapopita, nukta moja ya torati
haitapita.” Mathayo 5:18. Kwa hiyo kadiri mbingu na nchi zitakavyodumu, Sabato
itaendelea kuwa ishara ya uwezo wa Mungu wa kuumba. Edeni itakapotokea tena
duniani, Sabato, itatukuzwa na wote walioko chini ya jua, maana ni siku ya
Mungu ya kupumzika. “Toka Sabato hata Sabato, wenye mwili wote watakuja kuabudu
mbele za Bwana.” Isaya 66:23.
Ili kusudi kutunza Sabato kamili, watu hawana
budi kuwa watakatifu wao wenyewe. Kwa imani lazima wawe wenye kushiriki haki ya
Kristo. Sheria ilipotolewa kwa Waisraeli kwamba “Ikumbube siku ya Sabato
uitakase.” Kutoka 20:6. Bwana alisema pia kuwa, “nanyi mtakuwa watakatifu
kwangu.” Kutoka 22:31.
Jinsi
Wayahudi walivyofarakana na Mungu, wala hawakupata haki ya Kristo kwa imani,
Sabato ilipoteza umuhimu wake kwao. Shetani aliwaongoza kupotosha Sabato, kwa
kuwa ni ishara ya uwezo wa Mungu. Viongozi wa Wayahudi waliiwekea Sabato mizigo
mingi wakaifanya kuwa mzingo mzito kwa watu. Katika siku zile za Kristo
ilionyesha tabia ya ufedhuli na ubinafsi kwa watunzaji wake badala ya tabia ya
upendo wa baba wa mbinguni. Marabi walimwonyesha Mungu kama aliyewapa sheria
isiyowezekana kushikwa, au kutiiwa. Waliwaongoza watu kumdhania Mungu kuwa
asiyekuwa na huruma, na kuona kuwa Sabato ni ya ukatili. Ilikuwa kazi ya Yesu
kusahihisha makosa haya. Kwa hiyo Yesu hakukubaliana na maongozi ya Marabi, ila
aliendelea kuishika Sabato ya Mungu kwa kadiri ilivyo hasa.
Fundisho
la Sabato
Sabato
moja Yesu na wanafunzi wake walipopita katika shamba la nafaka iliyoiva,
wanafunzi walianza kuvunja masuke yake, na kuyapukuchua na kuyala. Katika siku
nyingine ya juma jambo hili lisingekuwa kitu, maana ilikuwa kawaida kwa mtu
yeyote anayepita katika shamba la matunda au shamba la ngano kula kitu cho
chote atakacho. Soma Torati 23:23, 25. Lakini kufanya hivyo siku ya Sabato
ilikuwa haramu. Kupukuchua masuke ilihesabika kama kuvuna au kupura.
Wapelelezi
mara moja walilalamika kwa Yesu wakisema: “Tazama wanafunzi wako wanatenda
tendo lisilo halali kutenda siku ya Sabato.” Marko 2:24.
Wakati
Yesu aliposhitakiwa huko Bethesda kuwa amevunja Sabato, alijitetea kwa
kujithibitishia kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, akisema kuwa anatenda kazi
kufuatana na mapenzi ya Mungu. Na sasa kwa kuwa wanafunzi wake wameshambuliwa,
alitaja mfano katika Agano la Kale, katika siku ya Sabato wakati wale waliokuwa
wakihudumu mbele za Mungu. Katika majibu ya Mwokozi, aliwakemea kwa kutojua
maandiko: “Hamjasoma jinsi Daudi alivyofanya alipokuwa na njaa yeye na wale aliokuwa
nao, jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu akatwaa mikate ya onyesho akala,
ambayo si halali kwa mtu yeyote kuila isipokuwa kwa makuhani pake yao?”
Akawaambia, Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya
Sabato.” Au hamjasoma katika sheria jinsi makuhani walivyo najinsi Sabato na
wanajiona kuwa hawana hatia?” Nawaambia kuwa kitu kikuu zaidi kuliko hekalu.
“Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” Luka 6:3, 4; Marko 2:27, 28; Mathayo
12:5, 6, 8.
Kama
ilikuwa haki kwa Daudi kula mikate iliyotengwa kwa ajili ya matumizi
matakatifu, ilikuwa haki pia kwa wanafunzi kuvunja masuke ya ngano na kuyala
siku ya Sabato. Makuhani pia walitenda kazi kubwa sana hekaluni siku ya Sabato,
kuliko siku nyingine. Kazi ya aina hiyo ikihusu biashara huwa dhambi, lakini
walikuwa wakitenda mambo yanayohusu uwezo wa kuokoa Wakristo, kwa hiyo kazi
yao iliafikiana na Sabato.
Kusudi
la kazi ya Mungu ulimwenguni ni kumwokoa mwanadamu. Kwa hiyo kitu ambacho
kingefanywa kuhusiana na kazi hiyo ya ukombozi, kinapatana na sheria ya Mungu,
na Sabato, wala si uvunjaji wa Sabato. Hivyo Yesu alikomesha majadiliano hayo
kwa kutangaza kwamba, yeye ndiye “Bwana wa Sabato”, yaani ndiye aliye juu ya
yote na juu ya sheria. Mhukumu Mkuu huyu aliwaondolea wanafunzi lawama, kwamba
wamevunja Sabato.
Yesu aliponya kwa
makusudi siku ya Sabato
Dhabihu zenyewe kama
zilivyo hazikuwa na maana yoyote. Zilikuwa njia tu sio mwisho. Kusudi la
dhabihu ilikuwa ni kuwaelekeza watu kwa Mwokozi, ili kuwaleta watu wapatane na
Mungu. Ni huduma ipendezayo kwa Mungu hasa. Huduma hii inapokosa kuwa na
umuhimu wake, huwa machukizo kwa Mungu. Ndivyo ilivyo na Sabato pia. Mawazo ya
watu yanapojawa na wasiwasi na mizigo yenye kuleta mashaka kunabaki tu kuishika
kisheria makusudi ya Sabato hupotoshwa. Kuishika tu kisheria ilikuwa kukufuru.
Siku nyingine ya
Sabato, Yesu aliona katika sinagogi mtu mmoja mwenye mkono umepooza. Mafarisayo
walitazama kwa makini waone jinsi Yesu atakavyofanya. Mwokozi hakusita kuondoa
ukuta wa mapokeo yao ya kuifanya Sabaato kuwa mwiko usiofaa.
Yesu alimwamuru yule
mwenye dhiki kusimama, halafu aliuliza swali: “je ni halali kutenda mema siku
ya Sabato, au kutenda mabaya, kuokoa maisha au kuangamiza?” Marko 3:4. Ilikuwa
kawaida kwa Wayahudi kwamba, mtu anaposhindwa kutenda mema anapokuwa na nafasi
ya kutenda hivyo, ilikuwa vibaya, kutojali kuokoa katika hali yao hasa. “Lakini
wao walinyamaza kimya katika swali lake. Naye aliwaangalia kwa ghadhabu, hali
akisikitika kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akasema: “Nyosha mkono wako.”
Akanyosha mkono wake, akawa mzima” Fungu 5. Yesu alipoulizwa kuwa: “Ni halali
kuponya siku ya Sabato?” Alijibu: “Ni mtu gani wa kwenu akiwa na kondoo
aliyetumbukia shimoni siku ya Sabato asiyemwinua na kumtoa humo? Mtu ana
thamani kubwa kiasi gani kuliko kondoo! Basi ni halali kutenda mema siku ya
Sabato.” Mathayo 12:10-12.
Wanyama walitunzwa sana
Wapelelezi
hawakuthubutu kumjibu Kristo. Walijua kuwa alikuwa akinena yaliyo ya kweli. Wao
badala ya kuvunja mapokeo, walihiari kumwacha mtu ateseke ili kumsaidia mnyama
awapo katika shida. Mnyama alitunzwa zaidi ya binadamu. Hiki ni kielelezo cha
dini zote za uwongo. Huwa zina asili ya kibinadamu ambayo hujitukuza zaidi ya
Mungu, lakini matokeo yake humdhili mtu zaidi ya mnyama. Kila mwalimu wa dini
ya uongo na watu wake hudharau mahitaji ya wanadamu, masumbuko yao na haki zao.
Injili humwinua binadamu juu zaidi kama mtu aliyenunuliwa kwa thamani kuu,
yaani damu ya Kristo, nayo huwafundisha watu kuwajali binadamu na
kuwashughulikia katika mahitaji yao na katika dhiki zao. Soma Isaya 13:12.
Mafarisayo walikuwa
wakimwinda Kristo kwa chuki nyingi, wakati yeye alikuwa akiokoa maisha, na
kuwaletea wafu furaha na burudiko. Je, ilikuwa halali kuua siku ya Sabato kama
walivyokuwa wakipanga kufanya kuliko Yesu alivyoponya siku ya Sabato?
Katika kumponya mtu
mwenye mkono uliopooza, Yesu aliilaumu kawaida ya Wayahudi, na kuiacha amri ya
Mungu ikisimama kama Mungu alivyoamuru. Kristo alisema: “Ni halali kutenda mema
siku ya Sabato.” Yesu aliitukuza Sabato kwa njia ya kufyagilia mbali mapokeo
yote, wakati wale waliokuwa wakilalamika kwa Yesu kuwa anavunja Sabato, wao
wenyewe walikuwa wavunja Sabato ya Mungu.
Wale wanaosema kuwa
Kristo aliiondoa Sabato, hudai kwamba alivunja Sabato na kuwahalalisha
wanafunzi wake kuvunja pia. Hivyo hushika njia ya Wayahudi walianguka. Kufanya
hivyo kutia tofauti kwa maneno ya Kristo, aliyesema, “Nimezishika amri za Baba
yangu, na kukaa katika pendo lake.” Yohana 15:10. Mwokozi, wala wafuasi wake
hawakuivunja Sabato. Akiangalia watu ambao watamshitaki, alisema: “Nani kwenu
anishuhudiaye kwamba nina dhambi?” Yohana 8:46.
“Sabato ilifanywa kwa
ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya Sabato.” Amri kumi za Mungu,
ambazo Sabato ni moja yao, Mungu aliwapa watu wake ili wapate mibaraka. Soma
Torati 6:24. Wote wanaotunza “Sabato wasiinajisi”, Bwana asema, “Watu hao
nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu. nitawafurahisha katika nyumba yangu ya
sala.” Isaya 56:6, 7.
“Mwana wa Adamu ndiye
Bwana wa Sabato.” maana yote hii ilifanywa naye na pasipo Yeye hakikufanyika
chochote kilichofanyika.” Yohana 1:3. Kwa kuwa Kristo alifanya vitu vyote,
alifanya na Sabato pia. Kwa ajili yake ilitengwa kando iwe ukumbusho wa
uumbaji. Humtaja kuwa ni Mwumbaji na Mtakasaji. Sabato hueleza kuwa aliyeumba
vyote ndiye Mkuu wa kanisa, na kwa ajili yake na uwezo wake twapatanishwa na
Mungu. Asema: “Niliwapa Sabato zangu kuwa ishara kati yangu na wao, wapate
kujua kuwa mimi Bwana Mungu niwatakasaye kuwafanya watakatifu.” Ezekiel 20:12.
Sabato ni ishara ya uwezo wa Kristo ututakasao. Nayo ni ishara kwa wote
wanaotakaswa na Kristo.
Wote wanaopokea Sabato
ni ishara ya uwezo wa uumbaji na ukombozi, itapendeza. Isaya 58:13, 14. Angalia
Kristo ndani yake. Hupendeza kwake. Inapomkumbusha mpotevu Edeni iliyopotea,
amani hiyo itarudishwa kwa njia ya Mwokozi. Kila kiumbe kitakariri mwito:
“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao, na wenye mzigo mizito, nami
nitawapumzisha.” Mathayo 11:28
LAMEKI MBOJE BUGOTABULULU |
CHARLES SHIBITA PUNDA WA YESU |
KWA MASWALI NA MAJIBU PIGA SIMU NUMBER 0767341977 AU 0763371047, 0787341977