MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

CIA: IS imepanga mashambulizi mengine


Image result for isil terrorist group


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani-CIA, John Brennan, ameonya kuwa huenda IS

inapanga mashambulizi mengine ya kigaidi, achilia mbali yaliyofanyika tu Paris. Amesema leo kuwa vikosi vya usalama na ujasusi vinafanya kazi kubwa ya ziada kuhakikisha vinagundua na kuzikwamisha njama za IS. Brennan amesema mashambulizi hayo yalipangwa vizuri katika kipindi cha miezi kadhaa kuangalia iwapo wana silaha, mabomu na mikanda yenye mabomu. Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema wamefanikiwa kuyapangua kiasi ya mashambulizi saba ya kigaidi kuanzia mwezi Juni, wakati wapiganaji waliorejea kutoka Syria walipoongeza kitisho. Amesema leo kuwa vikosi vya usalama na ujasusi vya Uingereza, vilitumia muda mwingi kukabiliana na mashambulizi kadhaa yaliyopangwa katika mitaa, lakini vinapaswa kurejea na kujizatiti upya baada ya mashambulizi ya Paris, yaliyowaua watu 129.

Subscribe to receive free email updates: