Waislamu wa mkoani pwani nchini Kenya, wameitaka serikali ya kuratibu upya sheria za kukabiliana na ugaidi
huku wakihisi kwamba, jeshi la nchi hiyo limekuwa likitumia suala hilo kuwanyanyasa. Hayo yamejiri baada ya maafisa wa jeshi hilo wiki hii kuvamia makazi kadhaa ya Waislamu kwa kutumia nguvu kupindukia sanjari na kuwaadhibu kwa kile walichosema kuwa ni msako dhidi ya magaidi ambao hata hivyo ulimalizika bila kumtia mtu mbaroni wala kunasa silaha zozote.