na charles shibita
Tuesday, October 13, 2015
Christopher Ole Sendeka Akerwa na Tabia ya Vijana Kupiga Deki Barabara Ili LOWASSA Apite.......Asema Huo ni Sawa na Utumwa
Mjumbe wa kamati ya kampeni ya chama cha Mapinduzi, Christopher Ole Sendeka amelaani kitendo cha mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kuruhusu vijana kusafisha barabara ya lami ili msafara wake upite akidai kuwa huo ni utumwa. Ole Sendeka alitoa kauli hiyo jana wakati akiwa katika mkutano wa kumnadi mgombea mwenza wa CCM,...
Magufuli Kasema Chanzo cha Mgao wa Umeme Nchini ni Wagombea Urais wa Upinzani Ambao Wamepiga Dili na Kampuni za Umeme
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kuwa tatizo la umeme linaloendelea nchini limesababishwa na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani. Mgombea huyo wa CCM aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana mkoani Lindi na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho, ambapo alisema kuwa baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani ndio chanzo cha tatizo...
Membe Amtaka Lowassa Aache Kujifananisha na Yesu.......Asema Hana Ubavu wa Kumfufua Balali
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia anaungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, hana uwezo wa kumfufua aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daud Balali. Membe ambaye jana alionekana kwa mara ya kwanza katika kampeni za mgombea...
Wizara ya Nishati yakanusha habari zinazodai mitambo ya Umeme inamilikiwa na Kampuni binafsi
TAARIFA KWA UMMA Hivi karibuni zimeibuka taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimnukuu Waziri wa Nishati na Madini, George B. Simbachawene akisema kuwa mitambo yote ya uzalishaji umeme nchini inamilikiwa na Kampuni binafsi. Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa taarifa hizi ni za uongo kwani Waziri Simbachawene hajawahi kutoa tamko la kuwa mitambo ya kuzalisha Umeme yote nchini ni...
Pendeza na Markson Products......Wanadawa za Asili za Kuongeza Uuume, Kurefusha Nywele,Kusimamisha Maziwa Yaliyolala n.k
Katika kusherehekea miaka kumi na nne ya kampuni hii tumetoa punguzo kubwa la bei kama shukran kwa wateja wetu. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na hazina kemikali wala madhara. TUNAZO ZA:- 1.Kerefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @80,000/= 2.Kuongeza shepu (hips na makalio) @120,000/= 3.Kuondoa mvi milele zisirudi @100,000/= 4.Kupunguza unene...
Monday, October 12, 2015
Sad News: Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Abdalah Kigoda Afariki Dunia
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda amefariki dunia leo saa 10 jioni nchini India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.Kwa mujibu wa kaka wa marehem Sadiki Kigoda aliyezungumza na Mpekuzi siku...
Kijana kotini kwa kuwakashifu wafanyakazi wa TCRA kwenye Facebook
Sheria Mpya ya Makosa ya Mtandaoni ya 2015 imeendelea kuonyesha meno yake kufuatia kijana Israel William (20), kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, akishitakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Akisoma mashitaka dhidi ya mtuhumiwa huyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Renatus...
Je,CCM Watakubali Matokeo Iwapo Watashindwa??.......Majibu Yote Yako Hapa
Moja kati ya kitendawili kigumu kwa vyama vya siasa nchini ni iwapo watakubali matokeo kama watashindwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu, swali hilo limekutana na majibu ya CCM. Akijibu swali hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba alisema kuwa chama hicho hakina wazo la kushindwa kwa kuwa uwezekano huo haupo. “Tangu...
Magufuli Akabidhiwa 'Faili' La Wasaliti Awashughulikie
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameombwa kuwafuta kazi baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamebainika kuwa wanakihujumu kwa kumsaidia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa. Katika hali inayoonesha kuwa kuna mchwa wanaokitafuna kwa kificho chama hicho, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM mkoani Arusha, Victor Njau alimuomba Dk. John Magufuli kuwafukuza kazi mara...
Mkapa Awataka WanaCCM Wavunje Makundi......Asema Mtu Anayehama Chama ni Msaliti na Hafai kuwa Kiongozi
RAIS mstaafu Benjamin Mkapa amewaasa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuacha kambi ambazo ziliweza kusababisha majimbo mawili kuchukuliwa na Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Lindi katika uchaguzi wa mwaka 2010. Rais Mkapa aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Mpilipili...
Makamba Ampa Makavu Kingunge
KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph Makamba amemshangaa Kingunge Ngombale-Mwiru kutamka kwamba chama hicho hakijafanya chochote wakati ndiye aliyeshiriki kuandika vitabu kadhaa vya mipango ya chama hicho.Katika hali ya kumsuta Kingunge aliyetangaza kuachana na CCM hivi karibuni, Makamba alisema mwanasiasa huyo amekosa hofu ya Mungu kwa kusema uongo dhidi ya chama hicho...
Dk Reginald Akana Kujitoa kwa Lowassa
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi amesema kuwa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye amejitoa kwa Lowasa si za kweli. Alisema hayo kwa waandishi wa habari, aliokutana nao jijini Dar es Salaam, jana. Alikutana na waandishi hao ili kufafanua kuhusu taarifa, aliyosema inaenezwa kupitia mitandao ya kijamii, yenye kichwa cha habari ‘Mengi ajitoa...
Sunday, October 11, 2015
Magufuli Aanza Kuunda Serikali......Taarifa Iliyotolewa na CCM Kwa Vyombo vya Habari LEO Imelitaja Jopo la Serikali ya Magufuli na Majukumu yake
Taarifa kwa Vyombo vya Habari Mwenendo wa Kampeni za CCM Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mgombea Mwenza, Ndugu Samia Hassan Suluhu, wameendelea kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini.. Hadi jana, tarehe 10.10.2015, Dkt. Magufuli alikuwa amekwishatembelea Mikoa 22 na Majimbo 203. Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi.
..
..