TAMBUA CHANZO CHA CRISMASI
Leo nimeona ni vema nitoe majibu ya swali lililoulizwa na wakristo wengi juu ya chanzo cha sikukuu ya Krismas ya tarehe 25 Desemba.
Swali:
Ni nini Chanzo cha sikukuu ya Krismass ya tarehe 25 Desemba? Je ni kweli Yesu alizaliwa tarehe hiyo?
Jibu:
Wakristo wengi wanaamini kuwa Yesu hakuzaliwa tarehe 25 December, kwa sababu Mariamu alipata uja uzito kati ya Mwezi wa sita (Juni) mwishoni – Hivyo kama kawaida ya binadamu, uja uzito unachukuwa miezi tisa ili mtoto azaliwe, hivyo ni wazi Yesu alizaliwa majira ya mwezi wa Februali. Ila hakuna Andiko la Biblia wala Historia iliyoweka kumbukumbu ya tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Kwenye Biblia tunaikuta tarehe 25 December, kuwa ni sikukuu iliyokuwa inasherehekewa na wapagani wa Babeli ambako Waisraeli walichukuliwa mateka. Hivyo sikukuu ya 25 Desemba ilikuweko kabla ya Kuzaliwa Yesu, na ilikuwa sikukuu ya wapagani wa Babebli wakisherehekea kuzaliwa kwa Mtoto wa Mungu JUA aliyeitwa TAMUZ.
Kulikuwa na Mfalme wa babeli aliyeitwa Nimrodi, na mke wake Nimrodiambaye pia aliitwa Malkia wa Mfalme jina lake aliitwa Semiramis, baada ya Mfalme Nimrudi kufariki, Mke wa mfalme akabeba mamba nje ya Ndoa. Ili kuficha kitendo hicho cha mke wa mfalme kubeba mimba wakati mume wake amefariki, akatunga UONGO kuwa Mume wake HAKUFA ila alibadilika kuwa Jua (SUN), hivyo mionzi ya Jua wanayoiona ndiyo iliyomdunga Mimba. Wababeli kwa kuwa walikuwa waabudu mizimu waliamini Uongo huo na kuanza Kuliheshimu Jua (SUN) kama Mungu wao.
Usiku wa kuamkia Tarehe 25 Desemba, Semiramis akazaa Mtoto aliyemwita TAMUZ, ambaye baba yake ni Mungu Jua. Imani yao ilienda mbali zaidi hadi kuamini kuwa tendo la Semiramisi kuzaa na Mungu jua yeye pia ni Mungu Mke na Mtoto wao Tamuz akaitwa Mungwa Mwana. Kuanzia kipindi hicho wapagani wa Babeli tarehe 25 mwezi wa 12, waliweka sherehe kubwa ya kuzaliwa kwa Mungu Mwana Tamuz.
Biblia inatoa maelezo juu ya jambo hilo la kufanya sherehe ambayo mfalme aliitumia kufungua baadhi wafungwa, kama msamaha wakati wa sikukuu - Yeremia 52:31 “Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-Merodaki,mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.”
Nabii Yeremia aliandika kitabu hicho zamani kabla ya Yesu kuzaliwa, taifa la babeli lilikuwa na Desturi ya kuweka huru wafungwa katika siku hii ya Kuzaliwa kwa Tamuz tarehe 25 Desemba. Enzi hizo haikuwa inaitwa Krismass huenda iliitwa Tamuz–Mass.
Baada ya Yesu kuzaliwa, hapakuwa na Sikukuu ya Krismass hata mitume hawakuwahi kusherehekea sikukuu hii, bali tunaona baada ya miaka mingi kupita karibia zaidi ya miaka 300 Mfalme Constatino wa Dola ya Kirumi aliyekuwa anaabudu JUA alimua kuwa Mkristo, lakini hakutaka kuacha Desturi za kuifanyia sherehe miungu yake. Hivyo akaamuru sherehe ya kuzaliwa Mungu Mwana Tamuz iendelee kusherehekewa ila wakristo waambiwe kuwa ni siku ya kuzaliwa Yesu Kristo. Kulingana na kitabu cha Historia ya kanisa la RC, ambacho hata mimi ninacho, kinachoitwa “The Compact History of Roma cathoric church” kinaeleza juu ya tangazo la Mfalme Constantino kwa wakristo kuanza kuadhimisha sikukuu za kipagani ikiwemo Ibada ya JUA ya siku ya Kwanza (SUN-DAY) badala ya Ibada ya Siku ya SABA,historia inaeleza kuwa alitoa maagizo hayo akiwa bado mpagani (Kabla ya kubatizwa), tangazo hilo lilitolewa mwaka 325AD.
Historia inasema, ilikuwa ni mwaka 336AD, ndipo kanisa lilipoamua kwamba, badala ya kuwa na sikukuu ya kipagani mjini Rome iliyojulikana kama “Natalis Solis Invincti” au The Birthday of theinvincible/unconquered Sun, iliyosherekekewa tarehe 25 Desemba, sasa tarehe hiyo iwe si kwa kuzaliwa jua, bali iwe siku ya kuzaliwa mwana (son) wa Mungu – Yesu Kristo. Kwa mara ya kwanza kanisa lilikuwa linaendesha Misa tu, lakini baadaye mtindo wa sherehe za kipagani ikaingizwa hadi leo inaendelea – ikitawaliwa na Vinywaji (Vileo), Vyakula na starehe za kila namna.
MASWALI YA CHANGAMOTO:
1. Kwa nini Mungu hakuona haja ya kuwa na siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo? Hata hakuiweka wazi tarehe na siku ya kuzaliwa kwa Yesu?
2. Ilikuwaje Mitume na Kanisa la awali hawakuwa na wazo hilo la sherehe ya Krismasi?
3. Kwanini wakristo walazimishwe kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa Yesu katika tarehe ya Kuzaliwa Mwana wa Mungu JUA? Na mfalme ambaye wala hakuwa Mkristo wakati huo?
4. Kwa nini wakristo wasiweke Tarehe ya kwao ambayo inaendana na mwezi hata kama Tarehe haijulikani? Make miezi tisa kutoka June ni February / March.
MUNGU AWABARIKI WOTE MNAPOENDELEA KUTAFAKARI JUU YA UKWELI HUU UNAOTUSAIDIA KUKUA KIROHO.