MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

LEO TENA KATIKA HISTORIA(SODOMA NA GOMOLA)

 Miaka 2000 kabla ya KRISTO na miaka 4000 tangu leo  karibu na bonde ya jorodan, tunapata  historia za kusisimua katika historia ya mwanadamu na historia hii ni kisa halisi cha sodoma na gomora, kilichotokea karibu na mji wa Yeriko katika Israel ya sasa ambapo mwanzo palijulikana kama nchi ya KANANI, nchi ambayo MUNGU alimwambia Ibrahim kuwa uzao wake utalisi.

                                               mwazo 12:6-7

Abramu akapita katikati ya nchi mpaka Shekemu, mahali patakatifu, penye mti wa mwaloni wa More. Wakati huo, Wakanaani walikuwa ndio wenyeji wa nchi hiyo. 7Ndipo Mwenyezi-Mungu akamtokea Abramu, akamwambia, “Wazawa wako nitawapa nchi hii.” Basi, Abramu akajenga madhabahu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu aliyemtokea. 

Ibrahim na Lutu walikuwa ni ndugu na udugu wao unaanzia kujulikana kupitia GHARIKA ambapo ukoo wa Ibrahim na Lutu uanapatikana kupitia uzao wa SHEMU mtoto wa kwanza wa NUHU ambaye kupitia SHEMU  ndo tunakuja kupata IBRAHIMU hivyo Ibrahimu alizaliwa na TERA na baadaye wakazaliwa watoto wengine akiwemo HARANI ambaye ndiye baba yake na LUTU hivyo Lutu ni mtoto wa Harani, kwa maana hiyo LUTU alimuita Ibrahim baba yake mkuwa soma    mwanzo  12:25-30  

Kisa cha Sodoma na Gomolah kinaanza kuelezewa kupitia kitabu cha mwanzo  sura ya 13, 18 na mwanzo sura ya 19, eneo hili lilikuwa ni eneo ambalo lilikuwa zuri kiasi cha kufananishwa na bustani ya EDENI, Mwanzo 13:10 “Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. 11 Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao”. 

baada ya mafanikio kuwa makubwa katika miji ya SODOMA,GOMOLAH na SIDIMU dhambi tatu zikatawala katika miji hiyo yaani dhambi ya ushoga,ushilikina na wizi.ukisoma

           mwanzo sura ya  19 na pia soma Ezekieli 16: 49-50 

inasema, " Tazama, uovu wa umbu lako, Sodoma, ulikuwa huu; kiburi, na kushiba chakula, na kufanikiwa, hayo yalikuwa ndani yake na binti zake; tena hakuutia nguvu mkono wa maskini na mhitaji. Nao walijivuna, wakafanya machukizo mbele zangu.. . "Neno la Kiebrania linalotafsiriwa" chukizo "linamaanisha kitu kinachochukiza kimaadili na ni neno lile lile linalotumika katika Mambo ya Walawi 18:22 ambalo linaelezea ushoga kama" machukizo. Vilevile, Yuda 7 inasema, "... Sodoma na Gomora na miji iliyozunguka walijitoa kwa asherati na uovu." Kwa hiyo, tena, wakati ushoga sio dhambi pekee ambayo miji ya Sodoma na Gomora ilijiingiza, inaonekana kuwa sababu kuu ya uharibifu wa miji.

Katika miaka ya 1980, mgunduzi wa kiakiolojia wa maeneo ya Kibiblia, Ron Wyatt, na Wana historia pamoja na Wanasayansi wanathibitisha hili kwamba lilitokea mwaka miaka 4000 tangu leo kama ifuatavyo,  mifupa ya binadamu inayokadiliwa kuwa ya watu takribani milioni 5 na zaidi iliyoko eneo hilo chini ya aridhi, bahari mufu iliotokea baada ya tukio hilo ambayo ipo hadi leo, nguzo ya chunvi ya mke wa LUTU iliyopo ukanda huo na pia milima ya mawe iliyobadilishwa kuwa ya salfa kwa sababu ya moto mkali  ambayo hadi leo mawe hayo ukiyawasha moto yanawaka na kulipuka. 

MOTO ULIOTEKETEZA SODOMA, GOMOLA NA SIDIMU NDIO UTAKAO ANGAMIZA WADHAMBI WA KIPINDI HICHI CHA KWETU MAANA DHAMBI HIZO HIZO ZA KIPINDI KILE NDIZO ZILIZOPO LEO

LUKA 17:27-30

Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa  kuja kwake Mwana wa Adamu. 27Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote. 28Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; 29lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. 30Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile.

                WITO WA MUNGU LEO NI HUU( yeremia 51:6-9)

6Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo. 7Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu. 8Babeli umeanguka na kuangamia ghafula; mpigieni yowe; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.

9 Tungependa kuuponya Babeli,Lakini haukuponyeka;
Mwacheni, nasi twendeni zetu,Kila mtu hata nchi yake mwenyewe


Mungu alishatuasa watoto wake tutoke huko, tujitenge nao mambo ya ulimwengu.. (Ufunuo 18:4)..Tusiyakaribia hata kidogo…Tutoke Sodoma wala tusiikaribie hata kidogo…Tukae nayo mbali sana maelfu ya Maili…Kumbuka sio tu Sodoma na Gomora pekee yake ndio ziliteketezwa wakati wa Nuhu..Biblia inasema hata ile miji iliyokuwa kando kando ya Sodoma na Gomora iliteketezwa pia (kasome Yuda 1:7)..Haikuwa na maasi kama Sodoma na Gomora..lakini kitendo tu cha kuwa karibu na miji hiyo tayari ilikuwa imeshanajisika nayo pia..Kadhalika leo..tunaaswa tukae mbali na uchafu wa dunia hii, wala tusifungwe nira na wasio amini kwa jinsi isivyo sawasawa.
MUNGU AWABARIKI ZAIDI TUKIMBIE KUTOKA SODOMA NA GOMOLAH, kama una swali uliza mda wowote kupitia 0763371047 au 0675355220. masomo haya yapo mengi sana kupitia UFUNUO WA MATUMAINI "TUPO HEWENI."

Subscribe to receive free email updates: