1Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa
maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na
bahari tena.
2Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya,
ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi
aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
3Nami nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile
kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa
pamoja nao.
Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe
atakuwa pamoja nao. 4Atafuta kila chozi, kutoka katika macho yao.
Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana
mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
”
5Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, “Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!” Kisha akasema, “Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli.
5Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, “Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!” Kisha akasema, “Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli.
Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila
gharama yo yote. 7Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, Nami
nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji,
wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika
lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Mwisho wa
miaka 1000 Kristo anarudi duniani akifuatana na waliokombolewa na jeshi la
malaika. Anawaita waovu waliokufa waamke ili wapate malipo yao ya ajali.
Wanatokea wengi sana wasiohesabika, kama mchanga wa pwani wakiwa na hali zao za
maradhi na kifo. Tofauti kubwa na wale waliofufuliwa mara ya kwanza.
Kila jicho
linamwangalia Mwana wa Mungu jinsi alivyo mtukufu. Waovu wanapaza sauti kwa
umoja wakisema, “Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana”. Mathayo 23:39. Hasemi
hivyo kwa upendo, ila tu ukweli wa mambo unawalazimisha kusema hivyo bila
kutaka.
Jinsi waovu walivyokufa wakiwa na hali ya ukafiri, ndivyo watafufuka
wakiwa na hali hiyo. Hakuna nafasi ya kurekebisha tabia zao.
Nabii asema,
“Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizietuni …. Nao mlima wa
mizeituni utapasuka katikati yake” Zekaria 14:4.
Mji wa Yerusalemu unaposhuka
chini, kutoka mbinguni, utatua juu ya mahali palipotayarishwa na Kristo pamoja
na watu wake na jeshi la malaika, wanaingia mjini.
Wakati
shetani alipofungwa asipate mtu wa kudanganya alikuwa katika hali mbaya sana,
lakini sasa aonapo waovu wamefufuka jeshi kubwa, matumaini yake yanamrudia.
Anakusudia kuendelea na mapambano tu, wala asisalimu amri. Atalipanga jeshi
lake vema, maana wote hao ni waasi kama yeye, wako tayari kufanya kama
apendavyo.
Hajitaji kuwa yeye ni shetani, bali ajitaja kuwa mtawala wa
ulimwengu kihalali. Anatumia hila zake ili kuwahadaa.
Kwamba ni yeye mrithi wa
ufalme ila ananyang'anywa haki yake kwa dhuluma. Anajidai kuwa yeye ni
mkombozi, anao uwezo wa kushinda vita, kwamba uwezo wake ndio umewatoa
makaburini. Shetani anawatia nguvu wote walio dhaifu, na kuwachochea kwa bidii
ili wakauteke mji wa Mungu.
Anaona jeshi kubwa la watu waliofufuka na kusema
kuwa yeye kama kiongozi wao atashinda na kutwaa enzi yake.
Katika jeshi
hilo yamo majitu ya zamani yaliyoishi kabla ya gharika, majitu makubwa yenye
akili na uwezo mwingi kimawazo, ambao walikuwa waasi waliosababisha gharika.
Pia kulikuwamo na wafalme na majemadari wakuu ambao siku zao hawakushindwa vita
kamwe. Watu hawa hawakubadilika, maana katika kifo hakuna kubadilika.
Walipofufuka walikuja na hali yao ile ya vita na ukatili.